Mzee Cleopa Msuya naye ataka Katiba Mpya

Mzee Cleopa Msuya naye ataka Katiba Mpya

Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya , leo amefika kwenye Kikosi Kazi cha Rais cha kukusanya maoni yanayohusu Katiba Mpya , Ambapo Mzee huyo HAKUMUNG'UNYA MANENO , AMEWAPASULIA WAZI WAJUMBE WA KIKOSI KAZI HICHO KWAMBA KATIBA MPYA NI SASA HIVI .

Mzee Msuya amesema kwamba ifike wakati sasa tuhitimishe jambo hili ili tuendelee na mambo mengine , badala ya kila mwaka kuzungumzia jambo hilohilo tu.

Chanzo: Mwananchi.

Ujumbe: Kama hawa Wazee wamechoshwa na danadana hizi za akina Pinda na Mukandala, WEWE NI NANI HATA UPINGE KATIBA MPYA?
Nyakati ni sasa.
The end of wicked
 
WAZEE wanapenda uzee mzuri, wakitengeneza na Mungu.

Tupate KATIBA mpya Ili tuondokane na Utumwa Kutoka MKOLONI mweusi.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Ameeeeen.
Well said
 
Wakati mwingine maoni ya hawa vigogo wastaafu yanaangalia utashi wa rais anataka nini? Kama hataki katiba mpya na wao hawataki kusema kinyume na mwenyekiti wao wa chama ambaye pia ni rais. Haya maoni ni ya kinafiki tu wala hayana uhalisia

..karibuni mtamsikia Dr.Mwakyembe naye anataka Katiba mpya.

..wakati wa utawala wa Jpm Mwakyembe alisema katiba mpya haileti chakula mezani.
 
..karibuni mtamsikia Dr.Mwakyembe naye anataka Katiba mpya.

..wakati wa utawala wa Jpm Mwakyembe alisema katiba mpya haileti chakula mezani.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Hawa wazee wanatengeneza tu mambo yao ila kama bado ndio zama katu wasingetoa kauli kama hizi.

After all kamati hizi kwakweli ni kwa ajili ya watu fulani tu.

Sidhani kama wananchi wa kawaida wanashirikishwa?

Ila kwakweli bila elimu katiba mpya ni makaratasi yasiyokuwa na msaada wowote.

Kama mwananchi hatakuwa na elimu ya kumpa ufahamu basi atashindwa kumuwajibisha kiongozi wake kutimiza matakwa ya katiba.

Elimu kwanza katiba ifuate.
Acha kuropoka, tuliza akili yako
 
Looo Mzee Msuya naye he got his voice back, kweli tulikuwa tunapita kipindi cha giza, ushetani, ukatili etcetera
Mipango ya Mungu Aliletwa ili afungue akili za watu zilizokuwa zimefungwa na lakiri ya ukiritimba wa kushika hatamu !! Unaona hata wale waliokuwa hawataki kusikia habari ya katiba mpya kuzungumzwa na wananchi hivi sasa wameona umuhimu wa hiyo katiba mpya !! Unajua ni kwanini wamebadilika ?? Ni kwa sababu ya yule mheshimiwa unayemchukia ndiye aliyewafungua akili zao na kujua kumbe katiba mpya ni ya muhimu sana !! " everything is happening for a reason "
 
Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya, leo amefika kwenye Kikosi Kazi cha Rais cha kukusanya maoni yanayohusu Katiba Mpya, ambapo mzee huyo hakumung'unya maneno, amewapasulia wazi wajumbe wa kikosi kazi hicho kwamba Katiba Mpya ni sasa hivi.

Mzee Msuya amesema kwamba ifike wakati sasa tuhitimishe jambo hili ili tuendelee na mambo mengine, badala ya kila mwaka kuzungumzia jambo hilohilo tu.

Chanzo: Mwananchi

Ujumbe: Kama hawa wazee wamechoshwa na danadana hizi za akina pinda na mukandala, wewe ni nani hata upinge Katiba Mpya
Wangeaminika zaidi kama wangesema haya kabla ya chama chao kukubali agenda ya Katiba Mpya. Sasa hivi wanaunga mkono tu msimamo wa chama chao.

Amandla...
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
Je huoni kwamba yule jamaa ndiye amefungua akili za watu ili katiba mpya ipatikane ?? Kila MTU sasa hivi anakubali kuwa upo umuhimu wa kuandikwa katiba mpya !! Yule jamaa amewaonyesha kuwa katiba iliyopo ina mapungufu makubwa sana !! Bila mijeledi wengine huwa hawaendi !! Mungu ana shani zake za kufanya mambo yafanyike !!
 
Wangeaminika zaidi kama wangesema haya kabla ya chama chao kukubali agenda ya Katiba Mpya. Sasa hivi wanaunga mkono tu msimamo wa chama chao.

Amandla...
Mwamba aliwanyoosha wenye kujidai chama ni chao !!
 
Mipango ya Mungu Aliletwa ili afungue akili za watu zilizokuwa zimefungwa na lakiri ya ukiritimba wa kushika hatamu !! Unaona hata wale waliokuwa hawataki kusikia habari ya katiba mpya kuzungumzwa na wananchi hivi sasa wameona umuhimu wa hiyo katiba mpya !! Unajua ni kwanini wamebadilika ?? Ni kwa sababu ya yule mheshimiwa unayemchukia ndiye aliyewafungua akili zao na kujua kumbe katiba mpya ni ya muhimu sana !! " everything is happening for a reason "
Nimekuelewa mkuu, President wa awamu ya 5 ndiye aliyezibua umuhimu wa kuwa na katiba mpya!
 
Propaganda tu! hawa wazee hawakuwahi kupinga katiba iliyopo, na hata wakati wa jiwe wote walioona katiba sio tatizo na walikuwa madarakani miaka dahali na hawakufikiria kuona katiba ni tatizo.

Tume inawapa nafasi watu wale wale wenye mawazo yale yale
 
Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya, leo amefika kwenye Kikosi Kazi cha Rais cha kukusanya maoni yanayohusu Katiba Mpya, ambapo mzee huyo hakumung'unya maneno, amewapasulia wazi wajumbe wa kikosi kazi hicho kwamba Katiba Mpya ni sasa hivi.

Mzee Msuya amesema kwamba ifike wakati sasa tuhitimishe jambo hili ili tuendelee na mambo mengine, badala ya kila mwaka kuzungumzia jambo hilohilo tu.

Chanzo: Mwananchi

Ujumbe: Kama hawa wazee wamechoshwa na danadana hizi za akina pinda na mukandala, wewe ni nani hata upinge Katiba Mpya
Katiba mpya tutapata baada bi mkubwa kushinda muhula wake wamwisho hata kama nini Mimi ningefanya hivyo nimawazo yangu lakini
 
Back
Top Bottom