Watu wanashindwa kujua kuwa mageuzi ni Process ndefu. Kuna wapinzani hawakumbuki kwamba huko Zanzibar walishamaliza mbinu zote za kistarabu kutaka kuleta mageuzi. Kama ni kufa watu wamekufa zaidi kuliko sehemu yoyote ya Tanzania hii. Kama ni migomo na kususia ndio usiseme. Kama ni kufungwa ndio wamefungwa zaidi, kama ni kubambikiziwa huko ndiko kuna chuo cha kubambikizia watu, kama ni unafiki wa watawala huko ndiko kuna chuo kikuu kabisa lakini hao wanaoponda ACT na iliyokuwa CUF kuingia SUK walitaka nini?
Walitaka hata hio fursa ndogo ya kuendeleza mapambano ya ndani nayo ipotee na wapinzani wapotee kwa ujumla wake? hivi hao wanaopinga kuna walau anayefika robo ya siasa za akina maalim Seif?
Unapoishutumu ACT kisa eti Imekubali kushiriki GNu na CCM ni kushindwa kuwaheshimu Wazanzibari na madhila yao waliyopitia katika kudai mabadiliko.
Halikuwa jambo dogo hata kidogo kwa CCM kukubali kubadilisha katiba ya Zanzibar na kuwafanya wahafidhina watambjue kwamba huwezi kuongoza Zanzibar bila kuwa na Ushirikiano na wengine. Walau angeulizwa mh Aman Karume na iko siku atasema ukweli. Heshima kwa wapinzani wa zanzibar (akina Maalim Seif na wenzake mh Duni) kwa kutotoka kswenye mstari. Watu wanajuwa wanachokifanya.
Mimi nadhani kulitakiwa kuongezwe spidi tu na mikakati ya kudai mabadiliko kwa kuongezwa mbinu wakati unashikilia hicho kidogo. Wanaobeza hawajui historia ya kweli ya Zanzibar na hawajui siasa. ACT imeheshimu Muktadha wa zanzibar katika safari ya mabadiliko ya Tanzania. Kongole kwenu ACT.
Watu walishasahau maridhiano na miafaka 3 iliyofeli, kuleta mabadiliko si jambo dogo. Hapo ACT ilipofika Zanzibar ni kituo kidogo kuelekea mabadiliko kamili. Its a matter of Time. Msichojua hao wahafidhina hawataki hata kusikia Wapinzani kuwemo Serikalini na kujua mipango ya Serikali. wanaumia vibaya lkn katiba haiwaruhusu. Kwa nini usiwasifu ACT walau kwa hilo?
Nyinyi hebu nyamazeni bwana.........