MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
- Thread starter
- #41
huyo mzee waliokuwa wanamshabikia ni wanayanga
Na ndiyo wamemponza kwani kinachoenda Kumpata very soon hata hao wana Yanga wanaompa Kiburi hiki na Jeuri hii leo watamkimbia na kumuacha peke yake. Ukweli ni kwamba tayari Serikali kupitia Wizara husika ( Waziri Mwakyembe ) imeshajua kuwa imewatibua wana Simba SC kwa yale Maamuzi yake ya Hisa za Kiuwekezaji ( wakimlenga Kipenzi chetu Mo Dewji ) na sasa wana Simba SC wamekuwa na Chuki na Serikali kiasi kwamba kuna Mpango ulikuwepo kwa wana Simba SC wote leo kutokwenda Uwanja wa Taifa Kuishangilia Timu ya Taifa na hata kama wangeenda basi wangeishangilia Timu ya Kenya na pia wana Simba SC walikuwa wameshaanza Kujipanga Kutoishabikia Serikali ya CCM hali ambayo kwa Kupima Serikali ikagundua kuwa yenyewe ndiyo itaathirika kwakuwa Tanzania nzima ni Simba na Yanga hivyo basi Serikali Kiujanja imeamua Kujikosha kwa wana Simba SC kwa Kuamua Kumbana huyu Mzee Kilomoni ili ionekane kuwa inaipambania Simba SC na iko nao sambamba katika Mipango yao ya Kiuwekezaji chini ya Mo Dewji huku pia ikimnusuru Waziri husika ( Mwakyembe ) ambaye kama isingekuwa ile Taarifa ya Mwekezaji Mo Dewji aliyoitoa jana basi Waziri Mwakyembe Siku ya Simba Day ndiyo angetujua ( angewajua ) vyema wana Simba SC na angeweza hata Kupoteza huo Uwaziri wake na Kujuta. Kwa Tanzania hii Simba na Yanga ni zaidi ya CCM na CHADEMA!