Mzee Jangala aenziwe akiwa hai

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,358
Reaction score
10,976
1. Msanii maarufu wa Sanaa za Maonyesho, almaarufu Mzee Jangala apewe heshima yake kabla ya umauti.

2. Miaka ya 1990 Mzee Jangala ametikisa sana RTD.

NB: Aenziwe na kupata stahiki zote - ikiwemo BIMA ya afya akiwa hai. Tusisubiri yamkute ya King Majuto.
 
Kwanini mzee jangala pekee yake na sio wazee wote 🤔 Au unafikiri hapa tanzania sector ya Utamaduni na sanaa ndo imegusa zaidi jamii?
 
Apewe stahiki zake na nani mkuu?

Kipindi anaigiza RTD na kina mzee Pwagu, je alikuwa ni mwajiriwa wa RTD au alikuwa 'deiwaka' tu?
 
Sio yeye peke yake, akina Abdallah Kibaden, King Kikii Muimbaji, Ahmed Kipozi Mtangazaji(If he still alive)....na wengine wengi

Isije kuwa kama King Majuto aliyekuwa anamlilia Rais njaa

Hii nchi huwa inawajali tu Wanajeshi Wastaafu kada zingine hapana
 
Ipo haja kuwepo Sheria
 
Huyu Mzee mbona nilisikiaga tetesi kuwa aliisha tangulia?.
 
Nakumbuka miaka ileeeeee…. RTD idhaa ya Biashara, zile siku za kipindi cha "MCHEZO WA RADIO", mdhamini pombe ya CHIBUKU, watu wanaizunguka Radio, kusikiliza hayo maigizo.
Kwangu mimi, mchezo wangu uliokuwa ndiyo ni the best, ni ule ulioitwa "NIACHIENI MWENYEWE"! Mtoto wake, aitwaye MSHAMU (yeye alikuwa anamuita "NSAMU")alikuwa hataki shule, akajiunga na kundi la vibaka akina Coster. Mzee aliuza mpaka shamba, ambalo mkewe alipinga sana, ili asome shule nzuri, Mzee kila akiambiwa tabia ya mtoto wake, anawaambia NIACHIENI MWENYEWE! Ikafika siku, akaja kukabwa yeye mwenyewe, kuporwa, na kupigwa!
Walikuwa wanafurahisha sana, akiwa na wenzie, akina GONGA, IGUNANILO, KARUMEKENGE nk.
 
Matuga alikuaga Ni Nani Mkuu? Nimesahau nafasi take katika igizo
 
Huyu mzee alitufurahisha enzi zetu wakati huo hakuna tv wala kitu kingine cha kuburudisha.
Nafurahi bado yupo hai hivyo hata RTD wenyewe wafanye kila kitu ili mzee Jangala apate heshima zote.
 
Pacha wake Mundu yuko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…