Mzee Juma Duni Haji kwanza Shikamoo , waendeleaje na hali yako mzee wangu ?
Nimekusikia Mzee ukizungumzia sakata la Freeman Mbowe , umesema ukipata nafasi ya kusaidia Mbowe kutoka gerezani utafanya hivyo bila kujali kama UTATUKANWA , na ukaenda mbali kwa kudai kwamba wanaotaka Mbowe aendelee kusota jela wao wako Ulaya wakitumbua maisha mazuri .
Tunakushukuru sana Mzee wetu kwa huruma yako uliyoionyesha kwa Mbowe , kwa kujitoa kwako kutaka "usaidie" atoke jela , Tunakuombea kwa Mungu akulipe kwa moyo wako huo , Amina .
Bali tunachokutaarifu ni kwamba Freeman Mbowe hatotoka jela kwa kujidhalilisha , hatotoka gerezani kwa kumpigia magoti yoyote kwa TUHUMA ZA UONGO ZA UGAIDI ALIZOBAMBIKWA NA WATAWALA WAOGA wanaoogopa Katiba mpya , wewe Mzee Duni unawafahamu waliombambikia kesi ya Uongo Mbowe , hao ndio wanaotaka Mbowe afie jela , hawa ndio waliokubambikia wewe mwenyewe na wenzako KESI YA UHAINI miaka ya nyuma , usisahau Baba yako mzazi alivyopigwa Kibao Mahakamani hadi akaanguka alipokuwa anakuja kukusalimia , na tangu siku hiyo hukumuona tena Baba yako hadi alipokufa na kuzikwa , Mzee hawa ndio ambao hawataki Mbowe atoke jela , usiwasingizie walio Ulaya .
Wasiotaka Mbowe awe Huru ni hao CCM ambao wewe na chama chako cha ACT mmeunda serikali ya Mseto Zanzibar , kwamba wewe na wenzako ni sehemu ya serikali inayomkandamiza Mbowe , na sasa mmekubaliana kudanganya Dunia kwamba Mtaunda TUME HURU BILA KATIBA MPYA , Yaani bila Katiba Mpya Mahera au Jecha watakuwa wanaongoza TUME HURU ZA UCHAGUZI ! Hiki ni kituko cha Karne ! yaani Katiba ile ile inayomruhusu Mwenyekiti wa ccm kuteua na kufukuza atakavyo eti leo tuiundie Tume Huru !
Japo nimeandika mengi lakini lengo langu ni kukumbusha kwamba WANAOTAKA MBOWE AFIE JELA NI HAO HAO WASHIRIKA WENU WA MADARAKA , WALA SI WALE UNAODAI WAKO ULAYA , Kwa Umri ulionao na madhira uliyopitia hatukutegemea upotoshaji wa namna hii kutoka kwako , BADO NAAMINI ULINUKULIWA VIBAYA .
Wabillah Tawfiq