Mzee Kikwete anatakiwa kuelewa kuwa Dini ni Siasa na Siasa ni Dini

Nje ya mada

Unawezaje kusema dini ni serikali na serikali ni dini ikiwa hapo kabla serikali zilikuepo kabla ya dini kuepo?

Kuna nchi zinaendeshwa kidini hizi mamlaka ya dini na ya serikali yanaingiliana, Afhanistan etc.

Kuna nchi unaona kabisa dini na mamlaka za kiserikali haviingiliani.

Tunaweza kubaliana na kauli kwamba Dini ni serikali na serikali ni dini ikiwa kuna hizo facts zote?
 
Wanufaika wa mchongo wa bandari,wanajitoa hadharani kutetea ugali wao,alianza bwana Rostam na sasa BT
 
Yeye bado anatuona watanzania wote mazuzu kama 2005 alipochukua kijiti.
Anashindwa kuelewa kwamba Tanzania ya sasa sio ile ya old school!
Sio ya zama zile za kusema na hili nalo litapita. ??!! πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Hawa ndio wanaoleta udini kwenye suala la bandari
hakuna udini katika suala la bandari kwa maana katika ya nchi imeorodhesha vifungu, kanuni na Sheria zake.
Kwa msisitizo katiba Ina jumuisha Imani ya watu wote bila kubagua rangi, kabila.
 
DINI KWENYE ELIMU SAWA,NDIO MAANS WANAJENGA SHULE.DINI KWENYE AFYA ZA WANANCHI SAWA, NDIO MAANA WANAJENGA HOSPITAL. DINI KWENYE SIASA ETI NO NO NO NO NO KWANINI???? ILI UHUBIRIWE UELEWE, INABIDI UWE NA UELEWA MZURI( ELIMU) NA AFYA NJEMA. LAKINI PIA LAZIMA IWEPO AMANI. AMANI INATOKANA NA SIASA SAFI. HAPO DINI UTAITENGAJE NA SIASA.MBONA BUNGENI KUNA MAASKOFU NA WACHUNGAJI?
 
Tangu maaskofu Wakatoliki (TEC) walipotoa waraka kuhusiana na ishu ya Bandari, watu mbalimbali wamejitokeza na kusema eti hao Maaskofu wanachanganya siasa na dini. Wamesahau kwamba siku zote wanasiasa ndio wamekuwa wa kwanza kuchanganya siasa na dini. Hebu chukulia kwa mfano Rais anapoapishwa, ni lazima atumie kitabu cha dini ili kuthibitisha kiapo chake. Hapo hapo utakuta amewaalika viongozi wa dini wamfanyia sala au wamuombee dua. Nchi inapokumbwa na matukio kama ya ukame, wanawaita tena hao hao viongozi wa dini waombe. Wao wenyewe pia wamekuwa wakipenda wapewe majukwaa kwenye nyumba za ibada ili wanadi sera zao. Je, huko sio kuchanganya siasa na dini?
 
Ujumbe wa Pope
 

Attachments

  • IMG-20230903-WA0014.jpg
    47.3 KB · Views: 1
Kama dini na sasa havichangamani basi wakati wa kuapishwa washike vitambi vyao badala ya biblia na msaafu
 
Duh.... Kweli JF ina archives
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…