Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Chombo kilichokusanya mapato effectively ni TRA,ambayo ni kazi ya mwinyi,baada ya kuwajenga watz kuwa wafanyabiashara Sasa ikaja hatua ya kukusanya Kodi,so no,kwa msingi huo mwinyi ndiye aliyewawekea waliofuata msingi mzuri wa uchumi
 
Yapo documented,hata humu jf ukiyasachi utayapata,brt,sgr,jhp ni mipango ilikuwepo,vipindi vya urais vingekua miaka 15,hayo yangefanyika na mkapa na kikwete
akili za kuambiwa changanya na zako,,,,,!!!!

ni wakati wake ndiyo RICHMOND, EPA ESCROW zilisikika, kama angekuwa mthubutu kweli basi ingekuwa kinyume.

He neither better not best, he just puffing himself no more.
 
SGR ni ya MAGUFULI. Miradi ya kikwete ni RICHMOND, DOWABS, EPA, tezi dume nk.
Magufuli kaanza kuujenga lakini halikuwa wazo lake wala haukuanzia na yeye.

Nimeweka video ya mwaka 2014 juu hapo, kabla hata Magufuli hajaota kuwa rais wa Tanzania tayari SGR ilikuwa imeshajadiliwa na Kikwete na China.
 
akili za kuambiwa changanya na zako,,,,,!!!!

ni wakati wake ndiyo RICHMOND, EPA ESCROW zilisikika, kama angekuwa mthubutu kweli basi ingekuwa kinyume.

He neither better not best, he just puffing himself no more.
Hujui hata EPA ni kazi ya lini!!.. kikwete huwezi mlinganisha na yeyote kwenye ujenzi miundombinu na kuukimbiza uchumi,itakua ilianza fuatilia mambo kipindi Cha smartphone
 
Mbona hakutuambia makati huo nia hiyo. Aache uongo, yeye na mwanae na mkewe wamekuwa busy kuididimiza nchi kwa faida zoo binafasi. Ila mama alifadhiliwa na sasa ana fadhili... mwanae kutoka kuuza madawa ya kulevyia na Kinjakitile Ngombale Mwiru mpaka kuwa waziri . Nchi inawenyewe wachache ila wengine sisi niwapangaji kulipa. kodi na tozo
 
Chombo kilichokusanya mapato effectively ni TRA,ambayo ni kazi ya mwinyi,baada ya kuwajenga watz kuwa wafanyabiashara Sasa ikaja hatua ya kukusanya Kodi,so no,kwa msingi huo mwinyi ndiye aliyewawekea waliofuata msingi mzuri wa uchumi

..Mwinyi naye aliweka misingi yake ambayo ilikuja kumsaidia Mkapa.

..lakini tuwe wakweli kwamba Mwinyi aliunda Tume ya Mtei na baadae TRA baada ya kuwa na mgogoro na wafadhili kuhusu uzembe ktk kukusanya mapato, na kulipa madeni.

..Mwinyi angeendelea na nidhamu aliyokuwa nayo kati ya 1985 to 1990 Tanzania tungeweza ku-qualify kusamehewa madeni kabla Mkapa hajaingia madarakani.

..Mwinyi na Mkapa walianza vizuri na kuja kujaribu ktk kipindi cha mwisho cha tawala zao.
 
Hatua za miradi mikubwa kwa mtazamo wa project management.

Kabla mradi aujaanza unafanya feasibility study na kugawa tasks za mradi (scheduling) hatua kwa hatua.

Mkandarasi ana assess ‘human resources’ needs za mradi, gharama za phases za mradi (na kukubaliana bei ya jumla, watalipwa kiasi gani baada ya kila phase). Mwenye mradi ana jukumu la kukaguwa hatua za kazi kama zipo sawa na quality.

Kwa miradi ya bongo inabidi turuke hatua za pili kama viability ya project na hasara za kuchelewa mradi (kwa sababu kwetu muhimu kujenga) hasara za kutojipanga na fines zake sio issue (hizo lawama tunarushiana wenyewe). As well as payback period ya mradi directly or indirectly maana management uwa tunampa poyoyo yeyote halafu baadae tunampa ruzuku kwa sababu hakuna faida.

Ukirudi kwenye concerns za paragraph one mkandarasi na mwenye mradi wanafikia vipi maamuzi ya bei, muda na quality. Mradi unakuwa ‘systems and procedures’ wanazokubaliana ambazo kila upande unatakiwa kuzingatia.

Ndio maana kila mradi una ‘project initiating document (PID) yenye analysis ya hatua za mradi. Humo kuna document mbili ambazo mksndarasi ana propose ‘project charter’ anaelezea hatua za mradi na kiwango cha kazi atakachofanya na jinsi ya kukaguana, kupima quality na kulipana. Kabla mradi aujaanza inabidi pandę ziafiki project charter.

PID pia ina ‘project concept’ ni work book ambayo ina detail explanation namna watakavyofanya kazi labda sehemu fulani tutachimba handaki, machine hii itahitajika, namna watakavyo usimamia mradi team yao, hela itakavyotumika, risk management ya mradi and so forth (haya makubaliano ndio CAG anafuata kwenye kukagua mradi).

Halafu sasa ndio mkandarasi na team yake wanaingia kwenye plans zao majukumu ya watu ndani ya mradi, wataalamu wanaohitaji na mlolongo mwingine ambao kuelezea ni mrefu kwa kweli.

Ni ujinga kusema wewe ulianzisha mradi wakati mpaka unaondoka hakuna mkarabdasi; it’s impossible kusema wewe unshusika kwenye mradi.

Huyo babu anahitaji psychological help, his narcissistic issue is very serious, kama unaelewa taratibu za ‘project management ya miradi mikubwa hawezi kuwa na mchango zaidi ya idea. Samia ndio anajenga SGR hilo halina ubishi.

Kwa kifupi ni kwamba kusema unahusika kwenye mradi kabla ya PID kusainiwa lazima una shida mahala.
 
Aache uongo, gesi aliyoahidi iko wapi
 
Mpuuzi sana, angezungumzia faida za gas aliyopora Mtwara
Kwenye gas Kikwete alicheza kama Pele lawama mnazompa ni za kumsingizia tu.

Sheria za Muhongo za hati za dharura ziliweka majedwali ya mgawanyo wa mapato wa floor income in PSA contracts (kutokana na ujazo wa kisima) jambo ambalo lilifanya wawekezaji kukataa kuingia mikataba ya LNG kupitia hizo sheria (zilikuwa zina favour nchi).

Na Kikwete aliishia hapo, Magufuli nae akabakia hapo hapo. January yeye ndio akataka kuleta ubunifu wake.

Jakaya swala la gas aliliona ni kaa la moto akutaka watanzania wamkumbuke kwa kuuza nchi, Na approach ya Professor Muhongo ilikuwa sahihi ndio maana wazungu awakupenda zile sheria.

Mengine ni team za mafisadi kutumia watu wenye akili za kucheza na akili za watanzania kuwapa mtazamo wa upotoshaji mnao urudia-rudia..

Uhalisia ni kwamba JK alijaribu kulinda gas na hakutaka mkataba uwe kipindi chake; mengine ni kuamini fake news tu na hata Muhongo sheria zake zilikuwa ni kulinda rasimali.

Shida ya JK ni kudandia mafanikio ya wenzake kujifanya na yeye anahusika.
 
..kuna UPIGAJI mkubwa na UCHELEWESHAJI katika mradi SGR.
Sgr inapaswa kufika Mwanza na Kigoma ili kuleta faida kwa nchi, kuishia Dom haina faida wala maana yoyote.

Halafu lengo mama la SGR ni kubeba mizigo ya nchi jirani na kuvuna pesa zao kuijenga tz kiuchumi na kuwapunguzia raia mzigo wa tozo na kodi ili tusihamie Burundi, lengo mama sio kubeba abiria kina Mr Tabasamu, kubeba Abiria hiyo ni bonus tu na ni ujuha na ushamba kushangilia vitu vidogo maana tukibweteka reli ikaishia njiani kilio na kusaga meno viko mbele kama wenzetu wa Kenya!!

SGR Ikiishia Dodoma au Mwanza tu bila kufika Kigoma yanayoendelea Kenya yatafika huku maana Reli yao ya SGR iliishia njiani Naivasha kutokana na ufisadi wa kutisha na sasa mkopo waliokopa kuijenga unadaiwa na China huku wananchi wakitakiwa kuulipa kwa kukamuliwa tozo na kodi kubwa wakati SGR haileti faida iliyotarajiwa na si wao walioiba pesa za mradi.

Huu si wakati wa kupongezana na kusifia yaani ngoma bado mbichi sana, hadi siku ile SGR imefika Mwanza na Kigoma na kubeba mizigo ya nchi jirani, hapo ndo sasa Bimkubwa apewe maua kedekede, mgolole, mkuki, ngao, shuka, nyimbo na mapambio.
 
Kama mabasi ya mwendokasi yametushindwa kuendesha,tutaweza treni?
Huu mradi wa SGR baada ya miezi sita tu chali. Hao hao wakina kikwete wanaomiliki makampuni ya usafirishaji ndio watakao kuwa mstali wa mbele kuihujumu, raisi Samia aangalie asiwachekee hata kidogo
 
Kuna makapi bado yanadunda tu na kucheka kinafki na iko siku yatambwaga Bimkubwa kama ilivyo desturi yao kuhujumu miradi mikubwa kwa maslahi binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…