Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Mengine ni team za mafisadi kutumia watu wenye akili za kucheza na akili za watanzania kuwapa mtazamo wa upotoshaji mnao urudia-rudia..

Uhalisia ni kwamba JK alijaribu kulinda gas na hakutaka mkataba uwe kipindi chake; mengine ni kuamini fake news tu na hata Muhongo sheria zake zilikuwa ni kulinda rasimali.

Shida ya JK ni kudandia mafanikio ya wenzake kujifanya na yeye anahusika.
Miswada ya dharura aliyopeleka bungeni kuhusu gas ilihusu nini, na kwanini wasomi wengi waliipigia kelele
 
Huu mradi wa SGR baada ya miezi sita tu chali. Hao hao wakina kikwete wanaomiliki makampuni ya usafirishaji ndio watakao kuwa mstali wa mbele kuihujumu, raisi Samia aangalie asiwachekee hata kidogo
Humo kwenye SGR amesafiri ili atengeneze mbinu za kuidhoofisha
 
Miswada ya dharura aliyopeleka bungeni kuhusu gas ilihusu nini, na kwanini wasomi wengi waliipigia kelele
Wasomi gani waliopinga zaidi ya Zitto Kabwe (ambae clue less) aliekuwa anapiga makelele kwa mshiko wa wazungu kuishinikiza serikali.

Na humu JF watu kama BAK na sasa hivi sampuli ya watu kama ChoiceVariable ndio wanaolazimisha hiyo miradi.

Wasomi gani wewe unaowajua waliopiga kelele zaidi ya wabunge wa CDM, chawa wa marehemu Mzee Mengi na wahuni wa JF wanaojua kusukuma upepo.

Jumlisha na tabia zetu watanzania kuwaamini watu wasio na nitty gritty knowledge ya maswala ya investment.

Mtu kama Zitto anaweza kuja hapa na kuandika upupu wake asilimia 90 ya members wakazani kaongea mambo ya maana.

Akija mtu ku counter argue hoja za Zitto ata kana argument zake zina merit, kwa sababu hana jina kwenye jamii yetu basi anaonekana mpuuzi tu mwingine.

Ndio shida ya jamii yetu, sheria za hati ya dharura za Dr Muhongo ilikuwa kulinda nchi. Mengine ni ujinga tu wapuuzi.

Ngoja niende ni Google kukuletea response ya wazungu walivyokuwa hawazitaki zile sheria za hati ya dharura na kusema haziwahusu makampuni yenye vitalu tayari.

Halafu huku sisi wananchi sheria hizo hizo tunamshutumia nazo JK na Muhongo kuuza nchi.

Salaleh mtihani kweli kuongoza Tanzania
 
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete Leo amesafiri kwa TREN ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na kusema safari yao wametumia muda wa saa 1 na dakika 49 tu

Mzee Kikwete amesema mradi wa SGR iliasisiwa na hayati Mkapa na ilipofika awamu ya Shujaa Magufuli ndio alianza Kuutekeleza lakini kwa bahati mbaya hakushuhudia matunda ya Juhudi zake

Mzee Kikwete amemshukuru Sana Mpendwa Wetu Mh Rais Samia kwa kuendelea kuukamilisha mradi huu ambapo Kesho Treni ya SGR itatoka DAR ES SALAAM hadi Dodoma ambayo ni mafanikio ya kihistoria

Source: ITV Habari
Mtajuana wenyewe kama vipi uaneni tuu 🤣🤣
 
Huyu mzee ni tapeli haswa
 
Huyu mzee ana matatizo makubwa. Atulie ale Pensheni.
Yeye miaka 10 alishindwa hata kuanza mchakato wowote
 
Mzee Kikwete amesema mradi wa SGR iliasisiwa na hayati Mkapa na ilipofika awamu ya Shujaa Magufuli ndio alianza Kuutekeleza lakini kwa bahati mbaya hakushuhudia matunda ya Juhudi zake
Hapo alitaka kusema iliasisiwa na yeye ila akajishtukia akatelezeshea kwa mtangulizi wake kwakuwa hawezi kupinga ametangulia mbele za haki,

Ni kawaida yake kusingizia marehemu kama siku ile ya mazishi ya Mwendazake pale Chato
 
Kikwete kumtaja Mkapa kafanya diplomasia tu kama kawaida yake. Ukweli ni kuwa Kikwete alikuwa tayari kishamaliza mapatano na China na alikuwa anangoja financing tu.

Hata hapa JF liliwahi kuandikwa kuwa mkataba ulikuwa uwe wa 7.4 billion Dollars, alipoingia magufuli akabadili na kuwapa Waturuki, lakini ukweli ni kuwa hata Upembuzi yakinifu ulikuwa tayari umeshafanywa.

Jikumbushe:

Kwa maana hiyo hata mradi wa Steiglers gorge ulikuwa tayari ufanywe na Brazil. Mradi wa Magufuli na wa eyapoti ya Chato na Daraja la mwanza kuelekea kwao.
Hakuna raisi bora kuwahi kutokea nchi hii kumzidi kikwete,kwasababu hata uhuru ni yeye ndie alifunga safari hapa mpaka uingereza kuomba uhuru ila ndio hivyo tu mzee ni mwanadiplomasia mno akaamua tu amchomekee nyerere
 
Hpo unasema uongo. Uhuru wetu haukwenda kudaiwa Uingereza.

Soma kijana, wacha kubadili mada kijinga. Aliyoyafanya Kikwete na anaoendelea kuyafanya Tanzania ni hadithi njema.
 
Nakubali. Ni kweli.kabisa Kuna miradi mingi sana iliasisiwa na Mkapa, Kikwete pia. Tena hii miradi inayokwenda na wakati mingi ni ya Kikwete...framework ziliwekwa na hayati Ally Mwinyi...
Ni vile tu wakati huo haukuwa kama siku hizi, Rais alikuwa akifanya kitu hasemi sana .

Na pia Kuna watu inawauma sana Samia kufanikiwa kumaliza miradi. Walijua hataweza, Alhamdulilah ameweza
Ofcoz,wengi wanapenda kuona SAMIA anafeli ili wapate cha kusema na kumwangusha...

Miradi ambayo Magufuli kaanza nayo yeye hajataka kabisa kuisusa na kuanzisha yake,bahati mbaya wao wanataka Credits ziende kwa JPM peke yake na kusahau KAZI HII KUBWA INAYOENDELEA.
 
Back
Top Bottom