Mzee Leo, anasema zamani waliotaka kuja IKULU waliwafanya hivi, siku hizi IKULU ni sawa na Kariakoo shimoni?

Mzee Leo, anasema zamani waliotaka kuja IKULU waliwafanya hivi, siku hizi IKULU ni sawa na Kariakoo shimoni?

Sifi Leo

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
6,408
Reaction score
12,100
Huyu Mzee Mimi namwita Mzee Leo maana umri wake analingana na Baba yangu mzazi,

Lazima niseme maana kuficha Haina Tija, Mzee wangu huyu niliyembatiza Jina la Mzee Leo yeye na Baba Sifileo wote waliishi pamoja maeneo ya wazito na makapuku.

Binafsi sikuwai ipenda KAZI ya Mzee Leo hasiye Baba yangu maana nilikuwa kwenye MAKAZI yangu yote namwona kama Mzee mbea sana.

Niyaache haya sio MUHIMU sana.

Mzee Leo katika pita pita zangu Leo hii nikakutana nae kwenye kijiwe Cha kahawa hapa Namanga pahala alipokuwa anapapenda Mzee wa msoga kabla ya kuwa Rais akiwa waziri wa mambo ya nje.

Mzee Leo Sasa ni mstaafu, watu mnajidanganyaga heti Hawa uwa hawastafu😂🤣 wanastafu na wanachoka sana mithili ya mbaraluju.

Mzee Leo anahoji.kwani siku hizi IKULU imekuwa kama kariakoo shimoni hata hasiyevaa chupi anaweza ingia?

MZee Leo anadai yakuwa enzi zao mtu aliyeitaji kwenda IKULU alijikuta kwanza anapangiwa siku ya kwenda, anasema shida yake, na baada ya hapo kama mwenye shida kulikuwa na umuhimu wa kumwona raisi basi, mtu huyo alichunguzwa sana sana na mpaka inafika siku ya kumwona raisi basi Wana idara wanakuwa well informed Sasa siku hizi ikoje?


Huyu mzimbabwe nani aliyemchunguza mpaka akaridhia aingie IKULU akapige picha na Rais wa nchi yetu akiwa amevalia kanga ?

Je IKULU imekuwa kariakoo shimoni?
 
Back
Top Bottom