Mzee Lowassa alipotuambia tunaandaa bomu (vijana) tulidharau; Bomu lenyewe ndilo Gen Z sasa linalipuka

Mzee Lowassa alipotuambia tunaandaa bomu (vijana) tulidharau; Bomu lenyewe ndilo Gen Z sasa linalipuka

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Ashukuriwe na kukumbukwa Mzee wetu Lowasa. Aliwaza kitajiri na hakuwahi kuabudu umaskini.

Alianzisha shule za kata lakini alipofaulu kwenye Mradi huu alitoka adharani akatueleza madhara ya matokeo ya kizazi cha shule za kata kwa siku za mbele.

Alituambia tusiweka misingi ya kuwaingiza vijana wanaozaliwa na kukua katika soko la ajira watageuka bomu.

Sasa tumeona Kenya bomu limelipuka, Uganda linalipuka na Tanzania litalipuka kwenye sanduku la Kura

Nchi isipoacha kuamini kwamba koo zile zile chache zitatoa viongozi ipo hatarini kuangamia. Taifa lina watu wengi wenye vipaji na maarifa lakini siyo watoto wa wakubwa.

Hadi pale tutakapoelewa kiwanda cha kutengeneza Gen Z kipo wapi ndipo tutaelewa kwamba Gen Z inaweza kuhatarisha uchumi na mipango ya waendesha V8
 
Ni suala la Muda tu! Kama wanaishi kimazoea kitakacho wakuta hawatoamini
 
Hii ya Tz siku ikitokea itakuwa maafa makubwa zaidi maana ni kama inatafutwa sehemu ya kutokea nafasi 10,000
Watuma maombi 200,000.
 
Ashukuriwe na kukumbukwa Mzee wetu Lowasa. Aliwaza kitajiri na hakuwahi kuabudu umaskini.

Alianzisha shule za kata lakini alipofaulu kwenye Mradi huu alitoka adharani akatueleza madhara ya matokeo ya kizazi cha shule za kata kwa siku za mbele...
Lowasa hakuanzisha shule za kata Kama ambavyo mkapa hakuanzisha TRA,acheni kusingizia watu wasiyotenda,lowasa hakuwa na maono yoyote zaidi ya tamaa ya Mali na kuona kiti Cha urais tiketi ya kuvuna Mali, ukosefu wa ajira kuwa bomu limeimbwa Sana duniani kabla hata lowasa hajawa Waziri mkuu,sokoine alizungumzia vijana kuwawezesha kujiajiri kwa kuwa serikali haiwezi ajiri wote,sokoine alifariki 1984
 
Back
Top Bottom