Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Salam!
Moja kwa moja napenda kumpongeza Mzee Juma Magoma kwa ushujaa wake wa kusimama mbele ya utawala wa Farao wenye lengo la kupora hazina ya wanachama wa Yanga. Inahitaji utulize kichwa kuelewa hoja za mzee wetu Magoma dhidi ya utawala wa Farao na mhabeshi.
Ni wazi kwa kizazi hiki cha yanga hiphop (kina Nalia ngwena ,Labani na wengineo) hawawezi kuelewa maslahi yanayopiganiwa na mzee Magoma. Mzee Magoma analilia hazina za Yanga zisiporwe na farao. Ambaye anaitumia Yanga ili kufanikisha biashara zake.
Hivi Yanga ni ya kupewa sh 1300 kama malipo ya jezi zinazouzwa 35000? Farao anavuna mali za mabilioni huku akiwahadaa wana yanga kwa supu ya nyama ya ng'ombe, Chapati mbili na show za Diamond. Wazee wanaoijua Yanga na kujua uchungu waliopitia kuifikisha yanga katika mafanikio wamestuka na kuamua kupigania ukombozi wa Klabu yao.
Moja kwa moja naungana na mzee wangu Magoma na kukitaka kizazi cha kukurupuka cha mitandaoni kukaa chini na kusikiliza historia ya klabu yao ya Yanga. Kisha watajua janja janja za utawala wa Farao na msomali.
Chanzo: Jembe sports
View: https://m.youtube.com/watch?v=C4SeZ-F13ow