mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Kupata faida ni kosa?Ndiyo maana Bakhresa alipoona figisu figisu kuifadhili Simba akajiweka pembeni na kuanzisha Azam yake. Hawa matajiri kuna faida wanapata katika hizi timu za Kariakoo.
Hiyo mali kubwa inaonekana baada ya GSM kuichukua Yanga? Kama mlikuwa na pesa ilikuwaje timu inapitisha bakuli kabla ya GSM? Kama timu ilikuwa na pesa, ilikuwaje mishahara hailipwi hadi wachezaji wanagoma? Kama timu ilikuwa na pesa ilikuwaje usajili ni wachezaji wa viwango vya chini? Kama mlikuwa na pesa ilikuwaje hadi kocha Zahera anachanga changa pesa kuisaidia timu isafiri? Kama mlikuwa na pesa ilikuwaje timu za Tanzania zilishindwa kushindana kwenye mechi za kimataifa, Gormahia tu alikuwa anawatoa jasho Yanga. Leo hii mnajifanya fyoko fyoko mnaibiwa. Mlikuwa na nini hapo kabla hadi leo muone mnaibiwa? Timu masikini wa kutupwa leo mnarefusha domo kama vile kuendesha timu ni jambo jepesi wakati mmepitia kwenye magumu yasiyoelezeka. Acheni undezi na akili zenu za kimagoma.Mzee Magoma yupo sawa kabisa,kinachosumbua Wanayanga ni uoga wa Umasikini tu.
YANGA yenyewe tu ni MALI kubwa sana.GSM sio mjinga kuwekeza Hela za Baba yake hapo.Anajua faida anazopata kwa kuwa mdhamini Mkuu wa YANGA.
Mzee Magoma anachotaka ni WIN-WIN situation baina ya YANGA na GSM.
Haiwezekani GSM aiteke YANGA yote kwa sababu eti anatoa Hela ya usajili,au timu imepata makombe chini yake!
Mchango wake unaheshimiwa,lakini Je maslahi ya YANGA kama Entity yako wapi?
Au maslahi ya klabu ya YANGA ni furaha tu ya Ubingwa?
Magoma amewaza mbali,GSM akiondoka Leo,Je YANGA wanabaki na nini?
Kama Ubingwa YANGA hawajaanza kuchukua Leo!
Hersi anakaa na wahasibu wanatengeneza hasara za kwenye makaratasi,Mashabiki wanatangaziwa wanakubali tu!
Mjomba yetu MAGOMA ameonyesha tofauti kubwa kati ya Wakereketwa,Mashabiki,Mashabiki mandazi,Wanazi na WANACHAMA.
Leo Hii 2024,Kuna watu ni wapenzi wakubwa wa YANGA lakini hawaoni umuhimu wala sababu ya kuwa Wanachama wa klabu hii Kongwe yenye Historia iliyotukuka.
Magoma yeye aliuona umuhimu na maana ya kuwa mwanachama,muacheni aipiganie haki ya YANGA.
Sisi wengine tuendelee kusubiria Furaha tu,maana ndio tunachokitaka.
Alikuwa anafurahia matatizo ya Simba SASA yamepiga hodi mlangoni kwake ama kweli ' kulia kupokezana'. Dunia inazunguka. Kila siku sio Jumatatu.Labani hawezi tokea hapa 😀 😀
Ndezi Dada yako,Kolo wewe.Hiyo mali kubwa inaonekana baada ya GSM kuichukua Yanga? Kama mlikuwa na pesa ilikuwaje timu inapitisha bakuli kabla ya GSM? Kama timu ilikuwa na pesa, ilikuwaje mishahara hailipwi hadi wachezaji wanagoma? Kama timu ilikuwa na pesa ilikuwaje usajili ni wachezaji wa viwango vya chini? Kama mlikuwa na pesa ilikuwaje hadi kocha Zahera anachanga changa pesa kuisaidia timu isafiri? Kama mlikuwa na pesa ilikuwaje timu za Tanzania zilishindwa kushindana kwenye mechi za kimataifa, Gormahia tu alikuwa anawatoa jasho Yanga. Leo hii mnajifanya fyoko fyoko mnaibiwa. Mlikuwa na nini hapo kabla hadi leo muone mnaibiwa? Timu masikini wa kutupwa leo mnarefusha domo kama vile kuendesha timu ni jambo jepesi wakati mmepitia kwenye magumu yasiyoelezeka. Acheni undezi na akili zenu za kimagoma.
CCM wanataka crooked thinkers,mtoto wa town kama Magoma hawezi kufit in.Magoma anatosha kupeperusha bendera ya CCM 2025
Kabla ya GSM hiyo Yanga ilikuwa na hali gani? Almasi huwa inagombaniwa, ila cha ajabu Yanga imeanzishwa mwaka 1935 lakini tokea ianzishwe mpaka sasa ni miaka 89 je katika hiyo miaka 89 imebahatika kupata hata wawekezaji wanaofika 5? Kama ingekuwa ni mali ingekuwa inagombaniwa hapo kabla. Ukweli uliopo ni kwamba hizi Simba na Yanga zimepandishwa thamani na watu wawili 1) Azam tv kwa kufanya branding ya ligi kuu na mpira wa miguu kwa ujumla. Na pili ni hawa GSM na Mo. Kiufupi Yanga na Simba hawana tofauti na mwanamke wa kijiji aliyekuwa mshamba mshamba, boss kamchukua kampeleka mjini kamrembesha saivi anamdharau aliyempeleka mjini. Kwavile kaishapendezeshwa, anajiona hata akiachwa wapo watakaomtaka. Tuliona kabla ya ujio wa GSM na Mo Simba na Yanga zikinyanyasika sana kimataifa.Ndezi Dada yako,Kolo wewe.
Almasi kabla haijakatwa na kutiwa nakshi si unaweza ukadhani ni jiwe tu!
GSM Kuona umuhimu wa YANGA sio jambo la ajabu,lilikuwa suala la Muda tu.Hata asingekuja yeye,wangekuja wengine.
Mpira ni Biashara ya pesa nyingi wewe,Umasikini haudumu Milele.
Unaongea utadhani YANGA ni liability,YANGA bonge la asset.
Huu ubwege wenu wa kuwafanya watu miungu unashusha mpaka thamani zenu kama Binadamu.
Nakuhakikishia hata GSM aondoke Leo,YANGA itapata Wawekezaji Tena wa maana sana.
Sisi hatuabudu hao warangirangi wa Upanga,zamani Narung'ombe.Kinachotakiwa Maslahi yazingatiwe.
Msituletee Ubepari.
Kila kitu kina muda wake,mchumba hasomeshwi.Kabla ya GSM hiyo Yanga ilikuwa na hali gani? Almasi huwa inagombaniwa, ila cha ajabu Yanga imeanzishwa mwaka 1935 lakini tokea ianzishwe mpaka sasa ni miaka 89 je katika hiyo miaka 89 imebahatika kupata hata wawekezaji wanaofika 5? Kama ingekuwa ni mali ingekuwa inagombaniwa hapo kabla. Ukweli uliopo ni kwamba hizi Simba na Yanga zimepandishwa thamani na watu wawili 1) Azam tv kwa kufanya branding ya ligi kuu na mpira wa miguu kwa ujumla. Na pili ni hawa GSM na Mo. Kiufupi Yanga na Simba hawana tofauti na mwanamke wa kijiji aliyekuwa mshamba mshamba, boss kamchukua kampeleka mjini kamrembesha saivi anamdharau aliyempeleka mjini. Kwavile kaishapendezeshwa, anajiona hata akiachwa wapo watakaomtaka. Tuliona kabla ya ujio wa GSM na Mo Simba na Yanga zikinyanyasika sana kimataifa.
Na ndio maana inapokuja swala win win maanake kila upande unufaike. Mchumba kusomeshwa ni makubaliano ya wachumba. Kinachotakiwa kwa Yanga ni mafanikio na mwekezaji yeye anachotaka ni kupata faida. Sasa ni ajabu kama mnataka GSM awape tu mafanikio halafu mnaona wivu yeye kupata faida. Hakuna shabiki anayefurahia timu yake ina ela nyingi kwenye akaunti kwasababu hakuna siku ela zitagaiwa kwa mashabiki bali shabiki anafurahia timu yake inavyopata mataji na kufanya vizuri hadi ngazi ya kimataifa. Tatizo la watu masikini ni wivu, husda na roho mbaya, mnataka msikie timu inapata mafanikio huku wakina Mo na GSM msikie wanapata hasaraKila kitu kina muda wake,mchumba hasomeshwi.
Tusifike mbali Mkuu,Dream ya YANGA ni kubwa sana.Na ndio maana inapokuja swala win win maanake kila upande unufaike. Mchumba kusomeshwa ni makubaliano ya wachumba. Kinachotakiwa kwa Yanga ni mafanikio na mwekezaji yeye anachotaka ni kupata faida. Sasa ni ajabu kama mnataka GSM awape tu mafanikio halafu mnaona wivu yeye kupata faida. Hakuna shabiki anayefurahia timu yake ina ela nyingi kwenye akaunti kwasababu hakuna siku ela zitagaiwa kwa mashabiki bali shabiki anafurahia timu yake inavyopata mataji na kufanya vizuri hadi ngazi ya kimataifa. Tatizo la watu masikini ni wivu, husda na roho mbaya, mnataka msikie timu inapata mafanikio huku wakina Mo na GSM msikie wanapata hasara
Magoma hakuanzisha Yanga; aliikuta.Hao matajiri au wasomi wanaopigiwa debe kwanini wasianzishe timu zao badala yake wanabaki kugombania timu na wazee au Wala mihogo Kama wanavyowaita.pamoja na kuwadharau Wala mihogo lakini wao ndio wamepambana mpaka timu zao zikawa na majina.
Unatuuliza sisi Au ?Muulizeni Mzee Magoma alitoa bei gani si Yanga mwenzenu huyo Au?😂😂Kipindi kile cha bakuli magoma alitoa shilingi ngapi?
Yanga haina mapato yake ya kufanya yote hayo, ingekuwa imejitosheleza kimapato basi ungeona kabla ya ujio wa hawa wakina Manji, GSM na Mo timu zingekuwa zipo vizuri kiuchumi. Kitendo cha kushindwa kujiendesha wakati ule ni funzo tosha kujua pesa za hivi vilabu havitoshi tu kuendesha timu tu achana mambo ya ziada kama uwanja, majengo ya kisasa, n.k. Mambo yangekuwa rahisi hivyo, vitu vingeshafanyika kitambo kabla ya hawa wawekezaji kuchukua timu.Tusifike mbali Mkuu,Dream ya YANGA ni kubwa sana.
Tunataka mapato yetu yafanye kazi kwa niaba ya klabu.
YANGA klabu kubwa,tunataka Uwanja wa Kisasa na Makao makuu yenye hadhi ya YANGA.
Hakuna anayetaka Hela ya kuishi YANGA,hatulishwi na YANGA.
Acha Dharau.
Magoma hakuanzisha Yanga; aliikuta.
Hivi unachoshindwa kuelewa nini?Yanga haina mapato yake ya kufanya yote hayo, ingekuwa imejitosheleza kimapato basi ungeona kabla ya ujio wa hawa wakina Manji, GSM na Mo timu zingekuwa zipo vizuri kiuchumi. Kitendo cha kushindwa kujiendesha wakati ule ni funzo tosha kujua pesa za hivi vilabu havitoshi tu kuendesha timu tu achana mambo ya ziada kama uwanja, majengo ya kisasa, n.k. Mambo yangekuwa rahisi hivyo, vitu vingeshafanyika kitambo kabla ya hawa wawekezaji kuchukua timu.
Jambo la kupongeza ni kwamba hawa wawekezaji wanabuni vyanzo vya ziada vya mapato kama vile kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ilimradi kuifanya timu iwe stable kiuchumi. Na hata swala la kujenga viwanja ni mipango ambayo itatekelezwa kwa kutumia wahisani na wala usijidanganye eti klabu zina ela ya kufanya hivyo.