Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 301,221
- 1,172,274
Taarifa iliyoripotiwa January 25, 2018 ni kuhusu King Majuto ambapo ilisemakana kuwa amelazwa Muhimbili, sasa Masoud aliyetoa taarifa hiyo ambaye ni Afisa habari wa Chama cha waigizaji ameelezea kuhusu Majuto kukosa kitanda Muhimbili na kurudishwa nyumbani.
Masoud amesema kuwa kwa sasa Majuto anaishi Vingunguti kwa ndugu zake ila January 26, 2018 anaripoti hospitali kwa ajili ya vipimo na kinachomsumbua kikubwa ni Presha kwani mwili wake ulikuwa umechoka sana na bado Madaktari wanampima ilikujua tatizo kubwa ni nini.?
"Mzee wetu majuto anaumwa na anaumwa kwa muda mrefu tulifanya utaratibu wa kutoka kwakwe kuja dar ili kutibiwa muhimbili alitakiwa kulazwa ila tukapewa taarifa na madaktari kuwa vitanda vimejaa tukarudi saa nane usiku" Masoud.
Updates
Mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani alimaarufu kama 'Mzee Majuto' amefunguka na kuweka wazi ugonjwa ambao unamsumbua kwa sasa kuwa ni tezi dume na kudai kuwa atafurahi sana endapo atafanyiwa upasuaji na kuondolewa maradhi hayo. Mzee Majuto ambaye kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam na tayari ameanza hatua za awali kuhakikisha kuwa anafanyiwa upasuaji kuondolewa tezi dume amesema kuwa kutokana na umri wake hashangazwi yeye kupata ugonjwa huo na kudai ni ugonjwa tu kama yalivyo magonjwa mengine