Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
1,585
Reaction score
1,073
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majato ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.

Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company (TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.

Mei 2 mwaka 2016 alitangaza rasmi kuachana na kazi ya uigizaji na kwamba anataka kumtumikia Mungu na kurudia tena kutangaza nia hiyo mwaka 2018 alipotoka nchini India kwa matibabu.

Alhaji Amri Athuman 'King Majuto' kufariki dunia siku ya jana, Agosti 8 2018 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kudaiwa kuugua ugonjwa wa henia na baadaye tezi dume.






NA HIZI NDIZO MOVIE ALIZOCHEZA KING MAJUTO, PIA UNAWEZA KUBONYEZA KILA JINA LA MOVIE NA UKANUNUA ONLINE.
· Ndoa ya Utata |
· Daladala |
· Nimekuchoka |
· Mbegu |
· Zebra |
· Shikamoo Mzee |
· Tabia |
· Utani |
· Tikisa |
· Trouble Maker |
· Gundu |
· Kizungunguzu |
· Shoe Shine |
· Street Girl |
· Faithful |
· Mtego wa Panya |
· Boss |
· Back with Tears |
· Sikukuu ya Wajinga |
· Nyumba Nne |
· Chips Kuku |
· Kitu Bomba |
· Ndoto ya Tamaa |
· Lakuchumpa |
· ATM |
· Bishoo |
· Tupo Wangapi |
· Moto Bati |
· Varangati |
· Out Side |
· Pusi na Paku |
· Juu kwa Juu |
· Swagger |
· Oh Mama |
· Jazba |
· Mke wa Mtu Sumu |
· Mbugila |
· Kidumu |
· Mkali Mo |
· Mpela Mpela |
· Utanibeba |
· Babatan |
· Mjomba |
· Msela wa Manzese |
· Karaha |
· Mpango Sio Matumizi |
· Mume Bwege |
· Shuga Mammy |
· Embe Dodo |
· Nakwenda Kwa Mwanangu |
· Seaman |
· Naja Leo Naondoka Leo Tanga |
· Mgeni Njoo |
· Kuwadi |
· Kulipa Tabu |
· Uso wa Mbuzi |
· Machimbo |
· Fundi Feni |
· Mwizi wa Kuku |
· Mtu Mzima Hovyo |
· Vituko Show Vol. 10 |
· Bettery Low |
· Brothers |
· Alosto |
· Back from New York |
· Kipofu |
· Koziman Vol 21 |
· After Money |
· Talaka Yangu |
· Gereji |
· Welcome Back |
· Mshamba |
· Pedeshee |
· Waiter |
· Inye Plus |
· Inye Gwedegwede |
· Inye Vol.1 |
 
Last edited by a moderator:
leo nimecheka mpaka yaani mbavu zinauma, nilikuwa sijaiona hii, majuto kweli kiboko, huyo jamaa angekuwa huko kwa wenzetu yani pesa angezikimbia haki ya mungu jamaa anachekesha sijaona.
 
Huyo jamaa ni noma ndugu zanguni...
Akilia utacheka
Akicheka utacheka
Akitembea utacheka
Akiwa anachambana na mwanamke utacheka,
Akiongea kingereza kama cha kanumba utacheka,
Sura yake na meno yake yalivyokaa mbalimbali utacheka,
Akitongoza utacheka
Akifoka utacheka....
Kutoka moyoni Alshamshuudin Amri Athuman ni noma.
 
Halafu sasa yeye sio kama hao wababaishaji weengine wanaokwenda kufanya shooting kwenye mahoteli na kwenye majumba yenye hadhi...

Mzee majuto anaweza akamaliza shughuli zake zote chini ya mti na akawaacha mmeshika matumbo kwa vicheko.
 
Huyo jamaa mwengine kafanana na Mpoki vile au ndugu yake?
 
jamaa wala hatumii misuli na kujikakamua kuchekesha.

nlicheka sana last week alipokuwa akihojiwa na bonge wa clouds fm akiwa tanta.

jamaa alidomonate interview kiasi kwamba bonge ndio akageuzwa mwalikwa na kupigwa maswali ya ukweli mno.
 
dah anaangalia mazingira, hajakosea yuko right haaaa haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…