MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimetazama clips za hotuba ya Kikwete na Makamba kwa umakini nikaona hawa wazee safari hii walikuwa wana hasira hatari. JK huwa yuko soft kwenye hotuba zake ila jana alikuwa wa moto mno. Neno mpuuzi, wapuuzi kalitaja mara kadhaa. Yaani hakuwa na masikhara hata kidogo. Makamba alikuwa na hisia kali toka juzi akihojiwa na waandishi. Mzee Makamba ndo alishindwa kabisa kuji-control. Bado sijaelewa kabisa sababu za wazee kucharuka hivi. Halafu mbona Bashiru alikuwa ka-relax kabisa? Nitafuatilia vizuri.