Msiomjua huyo mwenye t-shirt ya kijani kwenye picha ya juu ndiye kijana Lusinde,aliyembwaga Mzee Tingatinga kwenye uchaguzi wa kura za maoni-Mtera.
Ikumbukwe kuwa mapema mwaka huu kijanas Lusinde alimuonya Mzee Malecela ili kutunza heshima yake ajitoe mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge-Mtera tena akisisitiza kwa kusema kama Mzee Tingatinga atang'ang'ania kugombea itamkumba aibu kubwa.Lkn watu wa upande wa Mzee Malecela walifikia hatua ya kumuita majina yasiyofaa kijana Lusinde;na wengine walimkosea adabu zaidi kwa kumuita kijana Lusinde kama mlevi wa gongo asumbuliwaye na njaa!
Kwa wale waliokejeli kwa majina yasiyofaa kijana Lusinde,je sasa sio wakati wao wa kuja hapa jamvini na kumuomba msamaha?