Elections 2010 Mzee Malecela atakuwa "Tingatinga" kuipigia debe CCM yake?

Si kweli kwamba vijana hawana uchungu na nchi yao kwani yeye alianza kugombea akiwa mzee si na yeye alikuwa kijana.
 
kuwasalimia na kuwapa warning ya kuanza kampeni kabla ya muda
Siku CCM wanamtambulisha Kikwete pale Dodoma kwani Malecela hakuwepo kuwapa warning ya kuanza kampeni mapema.
 
Churchill hakuwa mashuhuri na kwenye peak 1945 aliposhindwa?sidhani.....JCM aliposhindwa 1985 ilikuwa CCM tu na hakukuwa na media strength kama sasa...lakini si alirudi 1990 na kuwa Pinda wa wakati huo...replacing Warioba in the process....
Kwa vile hujui kuwa baada ya Churchill kushindwa mwaka 1945, bado alishinda tena mwaka 1951 na kuendelea kuwa waziri mkuu hadi alipostaafu kwa hiari mwaka 1955. Nilichosema ni kuwa kushindwa katika siasa ni jambo la kawaida, ila kushindwa wakati wa peaka yako na kukosa nafasi ya kuandika historia upya ni pigo kubwa sana. Malecela ana nafasi ndogo sana ya kupata mwanya wa kurudi na kufuta doa hilo alilolipata, ingawa inawezekana; Tanzania's political landscape is unpredictable.
 
Tumemuongelea sana JSM. Kuna thread moja aliianzisha Balantanda humu Mods waliifuta nadhani. Tulijaribu kumshauri Mzee wetu huyu kupitia kwa wafuasi wake sugu humu hatukueleweka. Tukakejeliwa sana.
Utumishi wa Mzee wetu huyu kwa nchi yetu unatosha sana. Angepumzika tu. Akawa mshauri mzuri tu kwa waliopo madarakani. Bado akifa atazikwa kwa bendera ya Taifa na mizinga 19 kama Makamu wa Rais mstaafu.
 

Hayo yote nayajua ndio maana nikaleta mfano huu wa Churchil rejea sentensi yangu ya kwanza.....Kwani Churchill hakuwa mashuhuri na kwenye peak 1945 aliposhindwa?...na ya kwako....Nilichosema ni kuwa kushindwa katika siasa ni jambo la kawaida, ila kushindwa wakati wa peak yako na kukosa nafasi ya kuandika historia upya ni pigo kubwa sana....1945 mpaka 1951 ni muda wa haja
 

Baada ya "Go to hell"episode ya mwaka 1985 ambapo Mzee Cigweyemis aliwajibu wakazi wa Jimbo lake la Chilonwa baada ya wananchi wake kumuomba awasaidie kutatua tatizo sugu la maji.Kauli hiyo iliwakera sana wana Chilonwa na kusababisha kuangushwa kwenye uchaguzi wa Bunge na mwanasiasa asiyefahamika kabisa Mzee Yonah Mazengo,ambaye kabla ya kujitosa kugombea Jimbo la Chilonwa alikuwa anafanya kazi Wizara ya Maji kama fundi-bomba!

Hata mimi kwa sasa sijui mwanasiasa huyu kwa sasa yupo wapi?
 

Asante sana kwa kuweka rekodi sawa, nilidhani ni Kusupa kwa vile nina kumbukumbu kuwa mtu huyu aliwahi kuvurugana na waziri fulani pale Dodoma ila sina uhakika kama ndiye alishinda Malecela. Nakumbuka sana jina la KUSUPA kwa vile alikuwa akitaniwa mitaani eti KASUPA
 

Lakini watu wa Usangi waliendelea kumchagua Msuya ingawa na yeye aliwahi kutoa kauli kama hiyo ''Kila mtu atabeba mzigo wake....'' ingawa sikumbuki ilikuwa juu ya nini but there was an uproar over it...
 
Lakini watu wa Usangi waliendelea kumchagua Msuya ingawa na yeye aliwahi kutoa kauli kama hiyo ''Kila mtu atabeba mzigo wake....'' ingawa sikumbuki ilikuwa juu ya nini but there was an uproar over it...
Kama sikosei Msuya alisema kauli hiyo wakati anasoma bajeti akiwa waziri wa fedha, unajua ukilewa madaraka utafikiri hakuna siku utakaa benchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…