Pole kwa Watanzania kuelewa isivyo kauli "upumbavu na ulofa". Nami mwanzo nilielewa kama maneno hayo ni matus. Lakini maana halisi ya "mpumbavu" ni mtu asiyetumia busara katika maamuzi yake. Mara nyingi ni watu ambao hufuata upepo. Kwa mfano katika hali ambayo mtu anapita kuomba udhamini wa kutaka uongozi, watu badala ya kuendelea na shughuli zao za maisha wanakesha kumsubiri na hata kudiriki kuingia uwanja wa ndege au kupiga deki barabara, hakuna jina linalowafaa hawa watu zaidi ya "upumbavu". Mbaya zaidi ya aina hii ya watu kwa kufanya matendo kama hayo ni katika hali inayoonyesha si tu ufinyu wa fikra ila ni dalili tosha wamefirisika kimawazo. Neno sahihi ni "ulofa". Tujitahidi kutunza heshima na utu wa kibinadamu kwa fikara kutawala matendo.