bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
hivi kwa akili yenu ndogo mnadhani mtu asiyejua sera za chama wala miiko yake hata mipango yake awe kiongozi mkuu inawezekana kweli! Tafakari, chukua hatua. Magufuli mpango mzima na atawavusha watanzania wala si lowahasa na duniiiRubish
UKAWA ni moto wa mabua
Wenye kutafakari mambo kwa kina tumekuelewa sana na kifupi uko sahihi,Nliwah kusema mapema sana suala la UKAWA kujipanga na kuangalia sana wanaohamia UKAWA toka CCM wengi walisema mimi ni chizi kama ambavyo jija langu lilivyo. Nliwaambia Muogope sana CHIZI ANAYEJITAMBUA KULIKO MTU MWENYE AKILI ASIYEJITAMBUA KUWA ALIPEWA AKILI HALAFU HATUMII.
Juzi hapa nlisema kuwa MKAPA aliwaita UKAWA/WAPINZANI ni WAPUMBAVU NA MALOFA. nikataka kusikia watajibu nini nashukuru kwa ASILIMIA 95 WALIKUBALI. Nikaanza tena kuwa na hofu. OGOPA SANA WAPUMBAVU NA MALOFA Wanaojikubali kuwa ni kweli ni wapumbavu na laofa kuliko wale wanaokataa. LEO naleta mambo kadhaa ya kuangalia kwa makini sana UKAWA.
1. UKAWA inaweza kuvunjika mara baada ya UCHAGUZI au hata kuwa na migogoro Mingi sana Tunapoelekea kwenye Uchaguzi. sababu kuu ni kuna wana UKAWA wanaohujumu chama kwa kiasi kkubwa wakiwa wanafanya kazi kwa maelezo toka CCM usalama wa taifa
2. Kuna watu waliokuja UKAWA kwa kutafuta MADARAKA/ hasira za CCM. kulikuwa hakuna haja kumpokea na kumpa nafasi ya Kugombea Ubunge(nisahihishwe kama si kweli) mtu kama Said Nkumba kwa sababu Nkumba alikuwa ni mmoja wa tu wenye upeo mdogo sana wa kufikiria na kuamua mambo muhimu, akina nkumba wengi bado wapo CDM.Waangaliwe watu kama Akina Tambwe Hiza hawa si wanasiasa ni wanamaslah... Tambwe Hiza alikuwa wapi miaka yote hii aje kuibukia leo Mkutano wa Ukawa? Ni rahisi tu.. CCM walimtema tambwe hiza baada ya Kumtumia sana na baadaye akakosa matumizi. huyu alichoka sana kimaisha... sasa anarudi kupitia Ukawa na kuna siku atarudi tena CCM kiukweli hana mchango wowote kwa Harakati hizi za Ukombozi awe ni mtu wa kawaida tu.
3. UKAWA jipangeni kuzungumzia ADHA WALIZO NAZO WANANCHI msijishahau mkaingia kwnye siasa chafu za CCM. huko CCM watawashinda kwa kuwa wana uzoefu mkubwa wa siasa chafu kwa kutumiw watu wake mbumbumbu wasiojilewa. inabid mjitofautishe nao. ni muhimu sana kujitofautisha na CCM. maana wanawavuta muelekee uelekeo wao kwa kutaka kuwatoa kwenye mambo ya muhimu ya wananchi.
4. Haya majimbo mawili ambayo hamjayatolea maamuzi mpaka sasa yatawathiri hasa jimbo la segerea ambalo ningeshauri abaki nalo Mtatiro huyo dada mngemtafutia kazi nyingne but jimbo la segerea haliwezi hata kidogo.
5. Mmejipanga vipi ikiwa CCM WATAIBA KURA NA KUJITANGAZA WASHINDI? hapa ndipo mtakapopoteza wanachama wengi sana ikiwa hamtakuwa makini katka hili. na baada ya hapa UPINZANI utakufa maana hakutakuwa na WATU WENYE KUAMINI TENA UPINZANI. WENGI wataacha SIASA au kurudi CCM.
haya mtayakataa, mtayapinga kwa ukali na kebehi na kunidhihaki. tuombe uzima maana mtakuja kuyakumbuka.
Mzee candidate wa Ukawa hajatulia kabisa ndio maana ni lofa na ...
View attachment 281703View attachment 281704View attachment 281623
View attachment 281705
Shamsa Ford,Aunty Ezekiel,Jacq Wolper,Joyce Kiria na Halima Mdee
View attachment 281768
View attachment 281708
View attachment 281717
View attachment 281740View attachment 281741View attachment 281742View attachment 281743
View attachment 281766View attachment 281767
View attachment 281776
tulia dozi ikuingie
jana wapumbavu na malofa tumemuonesha kazi
Hio ndio busara yako mkuu? Tumia cs (common sense),wengine tulienda kuvinjali. Lowasa hafai na pumbavu kubwa.
View attachment 281703View attachment 281704View attachment 281623
View attachment 281705
View attachment 281768
View attachment 281708
View attachment 281717
View attachment 281740View attachment 281741View attachment 281742View attachment 281743
View attachment 281766View attachment 281767
View attachment 281776
Heee! Huyu ni huyu huyu Benjamin William Mkapa ninayemjua - basi mawili, anazeeka vibaya au alipanda jukwani akiwa amelewa viroba kama wafuasi wa upinzani amabao huwa indaiwa wanapewa viroba. Vile vile yawezekana ni ulevi wa kuvimbiwa baada ya kumlisha kwa kodi zetu sasa zinaturudia kwa matusi na si kejeli kama wengi wanavyojaribu kuipooza lugha kali aliyotumia tena kwa kurudia.
Yatosha kumshauri, bila kuona kama anadhalilika atuombe radhi watanzania, ambao ndio tunamlisha kwa kodi zetu mpaka hii leo, kwani amedhalilika zaidi kwa kauli yake hii. Lakini pia ningekuwa mimi ni mwenyekiti wa CCM ningejitenga na kauli ile kwa kuutangazia umma kuwa yale aliyoyasema Bwana Mkubwa Mkapa ni yake na si sera ya CCM kuwatusi wadau wake kwani nayo inapata ruzuku zitokanazo na kodi za hawa hawa wanaotukanwa.
Vile vile nashangaa tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa na Bwana Mkubwa wa Polisi na vyombo vingine havijatamka neno licha ya kuwa lugha za kuudhi hazikubaliki na zinaweza kuzua hasira kwa upande wa pili na kupelekea machafuko.
Nchi hii ni yetu sote, tusikubali hawa waliovimbiwa kutuharibia nchi yetu ni lazima kuwakemea kwa umoja wetu.
tulia tena kidogo
dozi itakutosha sasa hivi, vipi nikupatie aspirin pia?
Wewe unawaza ya chini na sio ya juu. Kaa pembeni.
tulia tu boss
dozi itakutosha muda sio mrefu
Kukusaidia usiwe unasema hivyo kwa mwelewa kwani "hicho ni kivuli chako", ya usoni mwako unajitahidi kuyaficha kisogoni wakati ni yako. "Mgombea wenu fake.juma2 njema.
asante
au ungependelea kikombe cha babu
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.
Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli, alisema.
Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.
Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.
Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.
Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!
Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.
BURIANI CCM!