Teslarati
JF-Expert Member
- Nov 21, 2019
- 2,621
- 10,466
Amani iwe nanyi wapendwa.
Miaka ya zamani kidogo kipindi nasoma, pale mtaani kwetu kulikuwepo na mzee mmoja alikua anajua mambo mengi sana, yaani alikua anakukuta dukani akihisi wewe ni mwanafunzi tu basi utaanza kuulizwa maswali na anakupa darasa palepale, alikua anajua kiingereza kile chenyewe cha kimalkia, alikua anaongea pia kijerumani lakini sina uhakika kama ilikua ni kijerumani kweli sababu muda huo nilikua sina exposure na ujerumani.
Cha kushangaza muonekano wa yule mzee alikua ni kama kichaa hivi, alikua na nguo pair mbili tu tulizozoea kumuona nazo, na alikua anafanya kazi ya kupalilia kwenye maboma na mashamba ya watu pale mtaani, hakuwa na familia yoyote, alikua anakaa peke yake. Na alikuja kupotea tu pale mtaani kila mtu hajui alienda wapi na niliuliza sana kama bado mzima au amefariki lakin sijawahi kupata jibu.
Binafsi napenda sana story, yule mzee nilizoeana nae akinikuta kijiweni hata kama nimetumwa nitakaa kumsikiliza anisimulie cha muhimu tu mwishoni uwe na mia mbili ya kumpa. Yule mzee alikua anadai yeye alipigana kwenye vita kuu ya pili ya dunia, alikua ni mtu anaeonekana ana memories nyingi sana za vita na harakati za kimaisha.
Kati ya mengi yule mzee alokuaga anasema moja wapo aliloniambia hadi leo nalifanyia utafiti ni hili jambo kuhusu Tanga.
Alisema wajerumani walikua wachawi balaa, waafrika na uchawi wetu ni cha mtoto kwa wajerumani kipindi kile.
Kwenye kunipa story kuhusu uchawi wa wajerumani aliwahi kuniambia kwamba huko Tanga kuna pango moja ndipo walikua wanafanyia mambo yao pamoja na mazindiko, waliacha uchawi mwingi sana kule na procedure mbalimbali za kuufanya uchawi huo kiasi kwamba hata kama mtu wa kawaida akizipata hizo procedures nae ataweza kuufanya huo uchawi.
Moja ya uchawi alioongelea ni kwamba kuna ibada moja ya kumtumia bundi akuambie kinachoenda kutokea ndani ya siku zijazo, kuna maneno unamtamkia huyo bundi na kisha unaanza kumkata kiungo kimoja kimoja na kusema tena maneno hayo maalum, yaani mfano unaanza na kidole kimoja, unamtamkia bundi hayo maneno maalum nae anaanza kukwambia nini kinaenda kutokea kutokana na maswali utakayoyaambatanisha.
Na lugha inayotumika pale ni lugha maalum ya kichawi ambayo inabidi uwe unaifahamu ili kufanikisha zoezi hilo. Alisema sharti ni kwamba huyo bundi ukimsikiliza hadi akasema kila kitu basi na wewe utakufa, hivyo inabidi ufanye timing umsikilizie akianza kuelekea mwisho umuwahi umchinje kichwa afe.
Najua jamiiforum kuna wajuvi wa mambo, na mzee wangu, mwanahistoria nguli Mohammed Said yupo humu ukiachilia mbali Mshana Jr na wataalam wengine. Je hayo aliokuwa anasema huyo mzee ni kweli au zilikua stori tu.