Mkuu Udadisi,
Nimekusoma na pia nakubalina nawe kwa hoja/wazo hilo!
Nafikiri hivi sasa ni wakti muafaka umefika kwa Serikali yetu nayo kujifunza na kujaribu kuonyesha nia na dhamira za kuwaenzi na kuwathamini Wanataaluma wetu khasa Historians!?
Pia viongozi/wanasiasa wetu ifikie wakti wajaribu kukubali ukweli mchungu wa kihistoria na kuuweka bayana kwa Watanzania woote...khasa vizazi vijavyo!?
Kwa mfano kiduchu...inatia simanzi mno kuona yakua mpaka kesho wanafunzi wetu woote pale nchini,hata walioko kwenye vyuo vya juu,bado wanasoma/wanakarishwa history ambazo hata hao ma-Lecturers/Waalim wao na pia viongozi/wanasiasa woote...wanafahamu yakua ni history iliyochakachuliwa/iliyopotoshwa kwa makusudi!? Daah!
Kwa kifupi,tunaishi katika Taifa ambalo tumekubali sisi wenyewe na hata vizazi vyetu vijavyo wawe misukule/waliokaririshwa upotoshwaji wa kihistoria!? Daah!
Kwa mfano kiduchu,nasikia mpaka leo ati pale Mlimani-UDSM...ati wanakataa kufundishia/kutumia maandiko ya Maalim Mohamed Said kwa kisingizio/kigezo cha "udini" uliomo kwenye maandiko yake!? Daah!
Je kwa mfano pamefanzika jitihada zipi za kitaaluma ku-challenge au kujaribu kurakabisha hayo "makosa" ya "udini" tunayoaminishwa yakua yametamalaki ndani ya maandiko ya Maalim Mohamed Said!?...jibu ni hakuna kabisa! Daah!
Sasa badala ya Wanataaluma kujaribu kuwa mfano wa ku-encourage dialogue among themselves...lakini unakuta vyuo vyoote muhimu hapo nchini na hata serikali/wizara husika...wooote kwa pamoja wameamua kumbeza na kumweka kando Mwanahistoria/Mwanataaluma mwenzao,kwa visingizio vya kitoto na vya kipuuzi kabisa!? Daah!
Tuko pamoja Kaka!