'Ukipewa Kipaji lakini ukakosa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu'
Hicho ndicho kimemkuta Saida Karoli. Hakuna wa kumlaumu, wakujilaumu ni Saida Karoli mwenyewe.
Muta ni mtu mwenye Upeo na Akili, alikuwa anajua anachokifanya wakati ule akitumia muda na rasilimali zake ili kumtoa kimuziki Saida Karoli. Bahati mbaya sana Saida Karoli hakutaka kujua matokea ya Athari za kisheria katika mkataba wake na FM Studio(Muta) wakati ule.
Kilichomkuta Saida Karoli kimewahi kuwakuta pia Nakaaya(katika mkataba na Sonny), The Comedy (Katika mkataba na EATV), Hadija Kopa(Katika mkataba na TOT). Na ndicho hicho hicho huenda kikaja kuwakuta Ya moto Band(Katika mkataba wao na Saidi Fella), Dogo Janja(Na Tip Top Connection), Harmonize, Raymond, nk(Katika mkataba wao na Wasafi Classic..)
Ushauri:
Kwa sasa Saida Karoli akubali tu kuwa alikosea na ujinga wake umemgharimu. Tukio hilo alione kama ni darasa kwake na kwa wasanii wengine katika mambo ya mikataba.