Mzee Muta alivyomfunga miguu Saida Karoli

Mzee Muta alivyomfunga miguu Saida Karoli

Jiraniyetu

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
350
Reaction score
333
Wana jamvi naomba tuweke michango yetu hapa..kwayeyote mwenye uelewa kuhusu hili jambo..Kama mambo tunayoyasikia ni ya kweli hivi inawezekanaje mtu unaimba nyimbo halafu unakosa haki ya kuzitumia na wakati sauti ni yako na kila mtu analitambua hilo,mfano nasikia SAIDA KAROLI hawezi kutumia nyimbo zake popote pale kama MZEE MUTA akigoma,hebu nipeni ufafanuzi kidogo hapo maana bado niko 3G kuhusu hilo.
 
Mzee Muta ametumia uelewa mdogo WA Saida kumsainisha mkataba hovyo,kwa jinsi alivyomtumia na kufaidika kwa kazi za Saida angempa haki tu ya kutumia kazi zake Ili ajikimu kimaisha..
 
Ukishakuwa chini ya record label hayo ya Saida yanatokea sana! Wewe kama msanii unakuwa huna mchango wowote kwenye utengenezaji kazi zaidi ya talent yako ya uimbaji na labda uandishi na kutengeneza melody! Kinyume chake, unakuta label ndiyo inakugharamia wewe kwa kila kitu... kuanzia na kazi zako hadi maisha yanayoambatana na kazi zako! Unakua "hujui" hata gharama ya kurekodi wimbo wala gharama ya kufanya video! Inakuwa hujui gharama ya mavazi ya kazi wala gharama za hotel unapoenda kufanya show!!!

Kutokana na hilo na ukikosa entertainment lawyer, kuna uwezekano mkubwa sana kazi unazofanya zisiwe mali yako bali zitakuwa copyrighted kwa kampuni uliyopo! Hili likitokea, haki zako zinaweza ku-include % ya mauzo ya album, shows, singles n.k! Hata kama mkataba wenu umeshaisha, utakuwa na haki ya kupata mrabaha/royalty inapotokea matumizi ya nyimbo zako kwa namna moja au nyingine... kwa mfano, kv Diamond ame-sample Salome, yeye kama yeye amemlipa mwenye hati miliki lakini Saida nae anastahili kupata % ya malipo yaliyofanyika! And for what I know, Saida amepata 25% wakati Mzee Mutta kakomba kilichobaki!!!

Anyway, nilichosema sio standard bali hiyo ni moja ya aina za contracts unapokuwa chini ya label!

Ubaya mkubwa zaidi wa mikataba ya aina hii ni pale wakati unaingia msanii unaweza kudhani umelamba dume manake kila utakachotaka, utapewa tu! Utahudumiwa kwa kila kitu huku ukidhani unapewa bure kumbe wenzako wanaweka kumbukumbu kwa kila kitu! Hapa ndipo huwa inaanza migogoro mingi kati ya wasanii na mabosi wao! Siku ya siku album imenunuliwa au umepiga show ya pesa ndefu, unakuta jamaa anakata hadi pesa ulizokuwa unakunywa soda! Mwisho wa siku unakuta unapiga mark time tu cuz' baada ya gharama zote kutolewa, mgao wako unakuta imebaki pesa mboga tu!!!
 
Kama yale Maneno ni yeye aliandika basi kwa haki miliki za miziki duniani ambazo hata sisi Tanzania chini ya BASATA kama sikosei tumeweka sahihi, Saida karoli anastahili pia kupata pesa yake bila kujali yeye na Muta waliweka sahihi vitu gani.

Wimbo kuna Instruments na Lyrics. Inategemea unachota wapi. Kama Saida aliimba tu na hayo maneno aliandikiwa basi hana haki yoyote katika huo wimbo wa Diamond. Kama Mama ndiye aliandika na anapewa fedha kidogo basi inabidi aende BASATA na bila kujali mikataba ilikuwaje, itabidi haki yake apewe. Haki miliki ziliwekwa ili kulinda Wasanii wasiojua sheria.

Mfano wimbo wa Mbumbe au The Lions Sleeps Tonight, ulitungwa na Solomon Linda wa South Africa. Akaja Mmarekani mmoja na kuununua haki miliki. Baada ya sheria kubadilika ilibidi haki miliki airudishe kwa Binti Mtoto wa Linda na hakurudishiwa fedha yake kwani walimwambia huwezi kununua HAKI MILIKI ya mtu hata utowe fedha gani.

The Lion Sleeps Tonight - Wikipedia, the free encyclopedia

Solomon Linda - Wikipedia, the free encyclopedia
 
'Ukipewa Kipaji lakini ukakosa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu'

Hicho ndicho kimemkuta Saida Karoli. Hakuna wa kumlaumu, wakujilaumu ni Saida Karoli mwenyewe.

Muta ni mtu mwenye Upeo na Akili, alikuwa anajua anachokifanya wakati ule akitumia muda na rasilimali zake ili kumtoa kimuziki Saida Karoli. Bahati mbaya sana Saida Karoli hakutaka kujua matokea ya Athari za kisheria katika mkataba wake na FM Studio(Muta) wakati ule.
Kilichomkuta Saida Karoli kimewahi kuwakuta pia Nakaaya(katika mkataba na Sonny), The Comedy (Katika mkataba na EATV), Hadija Kopa(Katika mkataba na TOT). Na ndicho hicho hicho huenda kikaja kuwakuta Ya moto Band(Katika mkataba wao na Saidi Fella), Dogo Janja(Na Tip Top Connection), Harmonize, Raymond, nk(Katika mkataba wao na Wasafi Classic..)

Ushauri:
Kwa sasa Saida Karoli akubali tu kuwa alikosea na ujinga wake umemgharimu. Tukio hilo alione kama ni darasa kwake na kwa wasanii wengine katika mambo ya mikataba.
 
Hao niliowawekea alama nyekundu waache wafurahie kutuzwa magari sahivi, nna wasiwasi kwamba baadae wataanza kulia
 
'Ukipewa Kipaji lakini ukakosa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu'

Hicho ndicho kimemkuta Saida Karoli. Hakuna wa kumlaumu, wakujilaumu ni Saida Karoli mwenyewe.

Muta ni mtu mwenye Upeo na Akili, alikuwa anajua anachokifanya wakati ule akitumia muda na rasilimali zake ili kumtoa kimuziki Saida Karoli. Bahati mbaya sana Saida Karoli hakutaka kujua matokea ya Athari za kisheria katika mkataba wake na FM Studio(Muta) wakati ule.
Kilichomkuta Saida Karoli kimewahi kuwakuta pia Nakaaya(katika mkataba na Sonny), The Comedy (Katika mkataba na EATV), Hadija Kopa(Katika mkataba na TOT). Na ndicho hicho hicho huenda kikaja kuwakuta Ya moto Band(Katika mkataba wao na Saidi Fella), Dogo Janja(Na Tip Top Connection), Harmonize, Raymond, nk(Katika mkataba wao na Wasafi Classic..)

Ushauri:
Kwa sasa Saida Karoli akubali tu kuwa alikosea na ujinga wake umemgharimu. Tukio hilo alione kama ni darasa kwake na kwa wasanii wengine katika mambo ya mikataba.
Duh!!!mambo mazito haya,,kumbe shule inahitajaka sana bongo..kwamaana hiyo ndo imeshakula kwake na hakuna wakutengua??mfano akikata rufaa ya kuukataa mkataba inawezekana?..
 
Back
Top Bottom