Ni Quruani Biblia tu ndio haiwezi kuvadilika. Hapa ndio haki za bibadamu wanatakiwa kuingilia badala ya kimchangia mtukana Rais!dah hilo swala limeniumiza sana jana kwa kweli, yn inamana saida hana haki kwny kazi zilizotengenezwa na kipaji chake, sijui mkataba wao ulikaaje kaaje mi sijaelewa kabsa.
Ngoja watu wachangie, nadhani Mh. Nauye ataupata huu mkataba, na kumsaidia Dada yetu atoke kwy kifungo hiki cha Bwana MuttaNauye s aiinglie kati jaman
Yes, Saida Karoli anaweza kufanya attempts zozote za kisheria kuuvunja au kuupitia upya(Review) huo mkataba. Milango hiyo ipo wazi. Japokuwa ni gharama na pia ni pata potea kama Mzee Muta alilifanya hilo kwa weredi mkubwa(Which I think so, kutoka na kariba yake!)Duh!!!mambo mazito haya,,kumbe shule inahitajaka sana bongo..kwamaana hiyo ndo imeshakula kwake na hakuna wakutengua??mfano akikata rufaa ya kuukataa mkataba inawezekana?..
Je anatokaje apo, tunatakiwa kumsaidia na sio, kumponda maana maswala ya kisheria sio wote tunayajua kwa asilimia zote'Ukipewa Kipaji lakini ukakosa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu'
Hicho ndicho kimemkuta Saida Karoli. Hakuna wa kumlaumu, wakujilaumu ni Saida Karoli mwenyewe.
Muta ni mtu mwenye Upeo na Akili, alikuwa anajua anachokifanya wakati ule akitumia muda na rasilimali zake ili kumtoa kimuziki Saida Karoli. Bahati mbaya sana Saida Karoli hakutaka kujua matokea ya Athari za kisheria katika mkataba wake na FM Studio(Muta) wakati ule.
Kilichomkuta Saida Karoli kimewahi kuwakuta pia Nakaaya(katika mkataba na Sonny), The Comedy (Katika mkataba na EATV), Hadija Kopa(Katika mkataba na TOT). Na ndicho hicho hicho huenda kikaja kuwakuta Ya moto Band(Katika mkataba wao na Saidi Fella), Dogo Janja(Na Tip Top Connection), Harmonize, Raymond, nk(Katika mkataba wao na Wasafi Classic..)
Ushauri:
Kwa sasa Saida Karoli akubali tu kuwa alikosea na ujinga wake umemgharimu. Tukio hilo alione kama ni darasa kwake na kwa wasanii wengine katika mambo ya mikataba.
Ushauri pekee wa kumsaidia Saida Karoli ni huu.Je anatokaje apo, tunatakiwa kumsaidia na sio, kumponda maana maswala ya kisheria sio wote tunayajua kwa asilimia zote
Sasa saida wa watu hayo mambo enzi hizo angeyajulia wapi, ukizingatia elimu yenyewe ndio vile tena!! Hadi huruma.Ukishakuwa chini ya record label hayo ya Saida yanatokea sana! Wewe kama msanii unakuwa huna mchango wowote kwenye utengenezaji kazi zaidi ya talent yako ya uimbaji na labda uandishi na kutengeneza melody! Kinyume chake, unakuta label ndiyo inakugharamia wewe kwa kila kitu... kuanzia na kazi zako hadi maisha yanayoambatana na kazi zako! Unakua "hujui" hata gharama ya kurekodi wimbo wala gharama ya kufanya video! Inakuwa hujui gharama ya mavazi ya kazi wala gharama za hotel unapoenda kufanya show!!!
Kutokana na hilo na ukikosa entertainment lawyer, kuna uwezekano mkubwa sana kazi unazofanya zisiwe mali yako bali zitakuwa copyrighted kwa kampuni uliyopo! Hili likitokea, haki zako zinaweza ku-include % ya mauzo ya album, shows, singles n.k! Hata kama mkataba wenu umeshaisha, utakuwa na haki ya kupata mrabaha/royalty inapotokea matumizi ya nyimbo zako kwa namna moja au nyingine... kwa mfano, kv Diamond ame-sample Salome, yeye kama yeye amemlipa mwenye hati miliki lakini Saida nae anastahili kupata % ya malipo yaliyofanyika! And for what I know, Saida amepata 25% wakati Mzee Mutta kakomba kilichobaki!!!
Anyway, nilichosema sio standard bali hiyo ni moja ya aina za contracts unapokuwa chini ya label!
Ubaya mkubwa zaidi wa mikataba ya aina hii ni pale wakati unaingia msanii unaweza kudhani umelamba dume manake kila utakachotaka, utapewa tu! Utahudumiwa kwa kila kitu huku ukidhani unapewa bure kumbe wenzako wanaweka kumbukumbu kwa kila kitu! Hapa ndipo huwa inaanza migogoro mingi kati ya wasanii na mabosi wao! Siku ya siku album imenunuliwa au umepiga show ya pesa ndefu, unakuta jamaa anakata hadi pesa ulizokuwa unakunywa soda! Mwisho wa siku unakuta unapiga mark time tu cuz' baada ya gharama zote kutolewa, mgao wako unakuta imebaki pesa mboga tu!!!
Akuna cha A-Town wala wapi? Mikataba aiangalii upuuzi wa A-Town wala wapi. Yoyote anapigwa uwe popote mbona kuna wasanii kibao wanapelekwa pelekwa katika matamasha ya Fiesta. Wanapewa mikataba ya kijinga na wanakubali ili mradi wasikose icho kidogondio maana huwa nawakubali sana watoto wa A town,wao wanaona ni bora kuuzia album kwenye rasket hata ukipata wateja watano hainanoma,kuliko kuwa chini,alafu chini ya rofa mwenzio,Saida anapakwa mchuzi uliotiwa maji,supu na nyama ya kweli wamekula wajanja
hahahahahaSaida karoli ni dadangu na Muta Mutahba ni kak yangu....hawa ndugu zangu ni wajinga pengine kuliko wajinga wote Tanzanania niliowai kuwashuudia.
Yaani haya mambo ni zaidi ya kuwa na elimu!! Unaweza kuwa na elimu na bado ukadhulumika vile vile ingawaje udhulumikaje wake utakuwa ni tofauti na ule wa wenzangu mimi! Na ndio maana wenzetu lazima wahusishe Wanasheria... na sio ili mradi Mwanasheria tu bali entertainment lawyer vinginevyo unaweza kupoteza haki zako bila kutarajia! Kuna makorokoro mengi sana yanayohusiana na masuala ya hatimiliki ambayo mwanasheria wa kawaida anaweza asiyajue au akayajua juu juu na matokeo yake akashindwa kukupatia kile ambacho ulistahili kupata!Sasa saida wa watu hayo mambo enzi hizo angeyajulia wapi, ukizingatia elimu yenyewe ndio vile tena!! Hadi huruma.
Sijakataa,ila fuatilia wasanii wa zamani wa Atown walianza vipi kujitegemea ki muziki hasa masula ya production na distribution,kitu kilichowapa heshima mpaka leo,achana na akina Nick watoto wa juzi,wapo akina Xplastaz na wengine,hii ili create awareness sana kwa wanamziki wa chuga,kwa mshabiki wa juziwa mziki hawez kunielewa,njaa zipo na ujeuri wa mwenye njaa upo piaAkuna cha A-Town wala wapi? Mikataba aiangalii upuuzi wa A-Town wala wapi. Yoyote anapigwa uwe popote mbona kuna wasanii kibao wanapelekwa pelekwa katika matamasha ya Fiesta. Wanapewa mikataba ya kijinga na wanakubali ili mradi wasikose icho kidogo
Mfano mzuri awo Weusi wanapewa pesa ya kawaida na wanaimba katika Fiesta na Niki wa pili ni msomi ulaghai upo kila kona inategemea una njaa ya kiasi gani
Awo Mapacha wenyewe walisanda kwa awo clouds media.
Haya mambo ya mikataba yanategemea yamekukuta na njaa ipi?
GoodUshauri pekee wa kumsaidia Saida Karoli ni huu.
1/Akubali kwanza kuwa alikosea mwenyewe.
2/Aache kulalamika ovyo kwenye mitandao.
3/Aende Kwa Muta na Kumshawishi ule mkataba upitiwe Upya ili uwe na maslahi mapana kwa pande zote(Na kama ikishindikana basi achukue hatua ifuatayo..)
4/Atafute wataalamu wa sheria za mikataba ili afungue shauri kwenye Vyombo husika(kama mahakamani, BASATA, COSOTA, Wizarani nk)
Nini weusi, hata mbele wasanii wanapigwa sana! Hadi akina Jiggar hadi wanakuwa akina Jiggar, washapigwa sana huko walikotoka!!! Hadi akina 50 Cents leo hii wanakuwa executive producers wa show kubwa kama Power, wamekula vitasa sana humu njiani!!! Hata kama sina ushahidi lakini naweza kusema with confidence kwamba hakuna msanii duniaani ambae hajapigwa sana kwenye safari yake ya muziki!! Na wakati mwingine wala sio kwa sababu ya njaa... wengi wanavyotafuta kutoka wanakuwa tayari kwa lolote lile!Akuna cha A-Town wala wapi? Mikataba aiangalii upuuzi wa A-Town wala wapi. Yoyote anapigwa uwe popote mbona kuna wasanii kibao wanapelekwa pelekwa katika matamasha ya Fiesta. Wanapewa mikataba ya kijinga na wanakubali ili mradi wasikose icho kidogo
Mfano mzuri awo Weusi wanapewa pesa ya kawaida na wanaimba katika Fiesta na Niki wa pili ni msomi ulaghai upo kila kona inategemea una njaa ya kiasi gani
Awo Mapacha wenyewe walisanda kwa awo clouds media.
Haya mambo ya mikataba yanategemea yamekukuta na njaa ipi?
Asanteni
Nini kifanyike?
- Wasanii wana umoja HEWA ambao unawasaidia kwenye kuzikana tu, wajiongeze na kutafuta mwanasheria wa kuwasaidia ku negotiate mikataba yao.
- Wasanii hawapendani kabisa, hata ukisikia nyimbo zao wanatukanana sana. Waamke na kupambana na wanyonyaji wao pale inapobidi, sio lazima wafanikiwe wao
Pamoja sana mkuu. Ndo waamke sasa
Mkuu gazeti ni refu sana lakini nime kusoma uko sahihi asilimia 100000000000