Asanteni kwa mchanganuo wenu wa hoja hii. Ukitaka kujua kwa undani malalamiko ya wasanii naomba pata muda wa kusikiliza mashairi ya Solo Thang katika wimbo wa "
MTAZAMO" wa Afande Sele/Prof. Jay, na wimbo wake mwenyewe Solo Thang wa "
KILIO CHANGU". Afande Sele kwenye wimbo wake wa
"Karata Dume" kagusia suala la kahimiliki, ingawa anaogopa kuwataja wahusika. Suma G pia kuna wimbo wake mmoja kalalamikia kupewa laki kwenye mauzo ya milioni!
*****************************************************
Kuna wakati nilikuwa nasikiliza redio moja maarufu ya kwa vijana hapa mjini, producer wa AY na Mwana FA bwana Hermy B aliliongelea kwa undani sana suala la copyright (hakimiliki). Kwa aina ya umbumbumbu walio nao wasanii wetu, si rahisi sana kukwepa maswaibu kama ya dada Saida. Hermy B alisema kwamba, kwa kila kazi inayotoka studio kwake, yeye lazima achukue asilimia fulani (hakuweka wazi ni % ngapi anachukua) kila kazi ya msanii aliyemrekodi inapotumika popote pale, iwe kwenye show, matangazo ya redio, tv ama magazetini.
Hapo bado meneja wa msanii nae hajachukua mgao wake. Hii ina maana kwamba, kama msanii ana kipaji na hana pesa za kumrekodi, studio nyingi wako tayari kumrekodia na kumtafutia meneja wa kumsambazia kazi zake, provided atasaini mkataba wa kuachia haki za kazi zake zimilikiwe na hao wanaomtoa, Nadhani hata ugomvi wa Hermy B dhidi ya AY na FA ulitokana na vipengele hivi kandamizi. Huenda hata ile kesi ya Tigo dhidi ya Mwana FA/AY kuna mtu aluchukua mgao wa zile ringtones bila wahusika FA na AY kupewa chochote.
Kuna haja kwa washauri wa kisheria kupitia upya mikataba kandamizi ya wasanii wetu ili angalau waishi kutokana na jasho lao, na si jasho lao kufaidisha mameneja wao ama ma-producer wao. Ugomvi wa Muumini Mwinjuma/Ally Choki na African Stars Band una harufu za masuala hayahaya ya hakimiliki. Ally Choki/Muumini anakuwa mwajiriwa wa African Stars Band na kulipwa pesa kulingana na show, ingawa Asha Baraka mmiliki wa bendi hajaimba wala kupiga kinanda.
Mwisho wa siku album zinamilikiwa na ASET. Ndicho kilichotokea kwa Marehemu Banza Stone, nae kapitia bendi hii na kuishia TOT, nadhani mpaka kifo kinamkuta alikuwa fukara wa kutosha tu, hata pesa za kununulia dawa mpaka watu wapitishe bakuli. Mauzo ya album za TOT na Twanga Pepeta hayakumsaidia kwa sababu yalichukuliwa na wamiliki, ingawa nyimbo katunga yeye. Kwa maana hii, Choki na wenzie wasipojiongeza basi wataishia kulipwa mishahara huku album walizoimba tangu 2000 zikiwa zinauzwa sokoni na mauzo yanaenda ASET, ihali walioimba wanaishi kuwa maskini.
Nini kifanyike?
- Wasanii wana umoja HEWA ambao unawasaidia kwenye kuzikana tu, wajiongeze na kutafuta mwanasheria wa kuwasaidia ku negotiate mikataba yao.
- Wasanii hawapendani kabisa, hata ukisikia nyimbo zao wanatukanana sana. Waamke na kupambana na wanyonyaji wao pale inapobidi, sio lazima wafanikiwe wao, hata watoto wao wanaweza kufaidika huko mbeleni.
Samahani kwa kuandika gazeti refu, ila nimejifunza mengi sana