Mzee Muta alivyomfunga miguu Saida Karoli

Mzee Muta alivyomfunga miguu Saida Karoli

'Ukipewa Kipaji lakini ukakosa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu'

Hicho ndicho kimemkuta Saida Karoli. Hakuna wa kumlaumu, wakujilaumu ni Saida Karoli mwenyewe.

Muta ni mtu mwenye Upeo na Akili, alikuwa anajua anachokifanya wakati ule akitumia muda na rasilimali zake ili kumtoa kimuziki Saida Karoli. Bahati mbaya sana Saida Karoli hakutaka kujua matokea ya Athari za kisheria katika mkataba wake na FM Studio(Muta) wakati ule.
Kilichomkuta Saida Karoli kimewahi kuwakuta pia Nakaaya(katika mkataba na Sonny), The Comedy (Katika mkataba na EATV), Hadija Kopa(Katika mkataba na TOT). Na ndicho hicho hicho huenda kikaja kuwakuta Ya moto Band(Katika mkataba wao na Saidi Fella), Dogo Janja(Na Tip Top Connection), Harmonize, Raymond, nk(Katika mkataba wao na Wasafi Classic..)

Ushauri:
Kwa sasa Saida Karoli akubali tu kuwa alikosea na ujinga wake umemgharimu. Tukio hilo alione kama ni darasa kwake na kwa wasanii wengine katika mambo ya mikataba.

Mkuu hayo yote ya kuwa alikuwa mjinga mara hana akili ni sawa.....ila kipindi akiwa mjinga ndo alikuwa anashine,leo kawa na akili ila tiyari keshafulia.....sasa itamsaidiaje?
 
Ndio maana mnasisitizwa Elimu Elimu Elimu, Mutta aliweza kuutumia ujinga wa Saida kama fursa
Hata angekuwa kasoma si ajabu bado angesaini huo mkataba.
Wajua mtu akiwa desperate kupata kitu au kufanikisha jambo flani baada ya msoto hawazi mbali.
Ndiyo maana kila siku utasikia msanii aliyetolewa na label flan baada ya kuvuma kagombana na aliyemtoa kisa maslahi coz wakati hajatoka yeye alikuwa analojali ni kusikika tu apate kujulikana na kupata laki kadhaa.
Lakini akishajulikana ndipo akili inaanza kufanya kazi.
Same applied kwa graduates mfano ukiona mikataba wanayowapa halotel na mtu anasaini coz hana jinsi ana njaa ila in the long run anaona kuwa japo nina njaa nanyonywa
 
Hivi kumbe kina Rich Mavoko, Raymond na Harmonize wameliwa na WCB! Sijui kama wanalifahamu hili kwa undani kama ulivyoeleza.
Inategemea terms & Conditions za mikataba yao inasemaje. (Sijui sana kuhusu haya mambo) wadau watafafanua zaidi. Japo sio mikataba yote ni ya kinyonyaji.
 
Upo sawa Mkuu. Hii habari niliisoma zamani na kama sikosei kipindi hicho ndiyo walikuwa wahusika. ila kwa sasa ni hao COSOTA. Nina imani huyu dada anaweza kwenda huko na kudai haki zake miliki kama yeye ndiyo mwandishi wa huo wimbo wa Maria Salome.
Upo sawa Hakuna kiasi cha pesa kinachotosha kununua haki bunifu yoyote. Wanaohusika na haya ni Cosota siyo Basata Kama ulivyoandika ingawa mengi uliyosema ni sahihi sana.
 
Ni Quruani Biblia tu ndio haiwezi kuvadilika. Hapa ndio haki za bibadamu wanatakiwa kuingilia badala ya kimchangia mtukana Rais!
Biblia inabadilika kuna agano la kale na agano jipya. Tukirudi kwenye mada husika ningeomba wanasheria waliomo humu JF watupe utaalam wao kama kweli huu mkataba alioingia Saida unaweza kubwa terminated.
Ukishakuwa chini ya record label hayo ya Saida yanatokea sana! Wewe kama msanii unakuwa huna mchango wowote kwenye utengenezaji kazi zaidi ya talent yako ya uimbaji na labda uandishi na kutengeneza melody! Kinyume chake, unakuta label ndiyo inakugharamia wewe kwa kila kitu... kuanzia na kazi zako hadi maisha yanayoambatana na kazi zako! Unakua "hujui" hata gharama ya kurekodi wimbo wala gharama ya kufanya video! Inakuwa hujui gharama ya mavazi ya kazi wala gharama za hotel unapoenda kufanya show!!!

Kutokana na hilo na ukikosa entertainment lawyer, kuna uwezekano mkubwa sana kazi unazofanya zisiwe mali yako bali zitakuwa copyrighted kwa kampuni uliyopo! Hili likitokea, haki zako zinaweza ku-include % ya mauzo ya album, shows, singles n.k! Hata kama mkataba wenu umeshaisha, utakuwa na haki ya kupata mrabaha/royalty inapotokea matumizi ya nyimbo zako kwa namna moja au nyingine... kwa mfano, kv Diamond ame-sample Salome, yeye kama yeye amemlipa mwenye hati miliki lakini Saida nae anastahili kupata % ya malipo yaliyofanyika! And for what I know, Saida amepata 25% wakati Mzee Mutta kakomba kilichobaki!!!

Anyway, nilichosema sio standard bali hiyo ni moja ya aina za contracts unapokuwa chini ya label!

Ubaya mkubwa zaidi wa mikataba ya aina hii ni pale wakati unaingia msanii unaweza kudhani umelamba dume manake kila utakachotaka, utapewa tu! Utahudumiwa kwa kila kitu huku ukidhani unapewa bure kumbe wenzako wanaweka kumbukumbu kwa kila kitu! Hapa ndipo huwa inaanza migogoro mingi kati ya wasanii na mabosi wao! Siku ya siku album imenunuliwa au umepiga show ya pesa ndefu, unakuta jamaa anakata hadi pesa ulizokuwa unakunywa soda! Mwisho wa siku unakuta unapiga mark time tu cuz' baada ya gharama zote kutolewa, mgao wako unakuta imebaki pesa mboga tu!!!
 
Upo sawa Hakuna kiasi cha pesa kinachotosha kununua haki bunifu yoyote. Wanaohusika na haya ni Cosota siyo Basata Kama ulivyoandika ingawa mengi uliyosema ni sahihi sana.
Mambo ya haki miliki ni magumu ndugu, popote pale na ndio maana ili mtu afaidike na kazi zake anatakiwa kuwa na Mwanasheria ambae atahakikisha mtu anafaidika na kazi zake hata kama ownership itakuwa kwa mtu mwingine! Nitakupa mfano mdogo sana unaotokea huko huko kwa wenzetu lakini nazungumzia upande wa filamu.

Chukua mwandishi wa script kwa mfano... huyu ndie msingi wa filamu na bila shaka ndie anayefanya kazi inayochukua muda mrefu zaidi pengine kuliko any production crew member (usichukulie mfano wa Bongo Movie ambao wanaandika hata kwa wiki 2). So what happen ukishaingiza script sokoni na kupata mnunuzi?

Ownership, narudia OWNERSHIP inakuwa transferred to the buyer... anaweza kuwa producer/production company/studio n.k! Ukishapewa chako; script hiyo si mali yako tena!! Sasa ukiwa na mwanasheria ambae anafahamu masuala ya filamu... hawa ni entertainment lawyers... atakachokusaidia huyu wala si kwamba "don't sell your copyright!" Atakachofanya ni kuhakikisha unapata benefits associated with your script... mosi, CREDIT, kwamba hata kama mabadiliko makubwa yatafanyika basi lazima filamu ikitengenezwa na kuoneshwa; jina lako litokee! Kingine ni ku-negotiate issue za bonus ikiwa filamu itafanya vizuri zaidi (mnaweza kuweka range kwamba iki-exceed kiasi fulani, unapata bonus ya kiasi fulani)! Vile vile lawyer ata-negotiate nini utapata in case script unayouzwa kesho au kesho kutwa itatengenezwa tv series na watu wengine...!! Au nini utapata ikiwa huyo huyo unayemuuzia baaada ya kutengeneza filamu; atatengeneza bidhaa zingine associated na hiyo filamu... kwa mfano, ikiwa atatengeneza t-shirt, how much original writer atapata na mambo mengine kama hayo lakini kuhamisha ownership ni mambo ya kawaida sana... tatizo linakuja pale ownership transfer inapofanyika wakati upande mmoja haujui ana haki ya negotiate nini!

Hata tukirudi kwa Saida Karoli, wale ambao walimvuta masikio kwamba ananyonywa; badala ya kumshawishi avunje mkataba walitakiwa kumsimamia kuhakikisha mkataba unapitiwa upya ili kuhakikisha who gets what in all stuff!!!
 
Biblia inabadilika kuna agano la kale na agano jipya. Tukirudi kwenye mada husika ningeomba wanasheria waliomo humu JF watupe utaalam wao kama kweli huu mkataba alioingia Saida unaweza kubwa terminated.
Nilikuwa naandika post nyingine wakati wewe unaandika haya! Naomba usome post yangu hapo juu lakini kwa kifupi tu ni kwamba, issue kama hizi ni zaidi ya kuwa na mwanasheria bali kuwa na mwanasheria anayeijua vizuri tasnia ya burudani.. wenzetu wana wale wanaoitwa Entertainment Lawyers!! Unaweza kuwa na mwanasheria lakini akaishia kushughulika na yale mambo basic peke yake!

Kuhusu kuwa terminated unaweza kufanya hivyo kukiwa na grounds za kuu-terminate!
 
Biblia inabadilika kuna agano la kale na agano jipya. Tukirudi kwenye mada husika ningeomba wanasheria waliomo humu JF watupe utaalam wao kama kweli huu mkataba alioingia Saida unaweza kubwa terminated.
There you are . Sasa sembuse mkataba wa binadamu?!?!?!
 
Mambo ya haki miliki ni magumu ndugu, popote pale na ndio maana ili mtu afaidike na kazi zake anatakiwa kuwa na Mwanasheria ambae atahakikisha mtu anafaidika na kazi zake hata kama ownership itakuwa kwa mtu mwingine! Nitakupa mfano mdogo sana unaotokea huko huko kwa wenzetu lakini nazungumzia upande wa filamu.

Chukua mwandishi wa script kwa mfano... huyu ndie msingi wa filamu na bila shaka ndie anayefanya kazi inayochukua muda mrefu zaidi pengine kuliko any production crew member (usichukulie mfano wa Bongo Movie ambao wanaandika hata kwa wiki 2). So what happen ukishaingiza script sokoni na kupata mnunuzi?

Ownership, narudia OWNERSHIP inakuwa transferred to the buyer... anaweza kuwa producer/production company/studio n.k! Ukishapewa chako; script hiyo si mali yako tena!! Sasa ukiwa na mwanasheria ambae anafahamu masuala ya filamu... hawa ni entertainment lawyers... atakachokusaidia huyu wala si kwamba "don't sell your copyright!" Atakachofanya ni kuhakikisha unapata benefits associated with your script... mosi, CREDIT, kwamba hata kama mabadiliko makubwa yatafanyika basi lazima filamu ikitengenezwa na kuoneshwa; jina lako litokee! Kingine ni ku-negotiate issue za bonus ikiwa filamu itafanya vizuri zaidi (mnaweza kuweka range kwamba iki-exceed kiasi fulani, unapata bonus ya kiasi fulani)! Vile vile lawyer ata-negotiate nini utapata in case script unayouzwa kesho au kesho kutwa itatengenezwa tv series na watu wengine...!! Au nini utapata ikiwa huyo huyo unayemuuzia baaada ya kutengeneza filamu; atatengeneza bidhaa zingine associated na hiyo filamu... kwa mfano, ikiwa atatengeneza t-shirt, how much original writer atapata na mambo mengine kama hayo lakini kuhamisha ownership ni mambo ya kawaida sana... tatizo linakuja pale ownership transfer inapofanyika wakati upande mmoja haujui ana haki ya negotiate nini!

Hata tukirudi kwa Saida Karoli, wale ambao walimvuta masikio kwamba ananyonywa; badala ya kumshawishi avunje mkataba walitakiwa kumsimamia kuhakikisha mkataba unapitiwa upya ili kuhakikisha who gets what in all stuff!!!
Mkuu nimekupata vizuri, tatizo watanzania wengi ni watoaji wazuri Wa dosari lkn si watoa solution. Tangu miaka ile watu walijua mkataba wa Saida ni wa kinyonyaji lkn hakuna aliyejitolea kumsaidia.
Nakumbumbuka huyo manager wa Saida alishawahi kuhojiwa na radio moja zamani kidogo akawa anajitetea eti Saida alijifilisi mwenyewe. Jamaa alidai eti Saida alipolijua jiji akawa naye anaishi kusupastaa, kipindi chote alichokuwa DSM bidada alikuwa anaishi hotelini.Huyo manager a.k.a Carl Peters alidai eti Saida alikuwa anatumia pesa kwa fujo matumizi yake kwa siku yalikuwa karibia laki 5 na kipindi hicho laki tano ilikuwa kubwa kwa mtu kuitumia kwa siku. Carl Peters alidai mara kwa mara alikuwa akimshauri Saida kupunguza matumizi lkn bidada hakusikia kwani jiji lilimlevya.Hivyo umasikini wa Saida alijitakia.
Kwa hiyo tukiacha kuwa mkataba ulimnyonya Saida lkn hata hicho kidogo alichopata bidada alikitumia vibaya.
 
Kisheria hasa sheria namba 7 ya mwaka 1999 ambayo ndyo inasimamia masuala ya hakimiliki ni kwamba kazi ya msanii Ina haki mbili... moja inaitwa Economic rights ambayo ni haki za kiuchumi. Hizi zinahamishika na mtu anaweza kumuuzia mwingne..Kama alivyouza Saida. Saida aliuza haki zake zote za kiuchumi. Haki ya pili ni Moral Rights huitwa Haki ya kimaadili.. hii haiuziki na Wala huwezi ibadilisha.. mfano Jina la mtunzi.. ndyo maana nyimbo za Saida zinatambulika kama za Saida lakini mwenye haki za kiuchumi nazo ni Muta..
Wasanii wengi wa Tanzania hasa wa Filamu wamekuwa wakiuza Haki zao za kiuchumi zote.
 
100% RIGHT... na hizo Haki zisizoamishika ndo hizo hapo juu kwenye filamu wanaita CREDIT... kwamba, kwa mfano mwandishi wa script anaweza ku-transfer ownership na aliyeinunua hata kama ataifanyia mabadiliko makubwa, bali kweney filamu itakayotengenezwa jina la huyu original writer lazima litokee as a Writing Credit!!
 
Mkataba wowote ule ili uwe halali lazima uwe una vitu kadhaa,kimoja wapo ni consent(ridhaa),consent ili iwe halali lazima iwe imetolewa bila kutumia force,coercion,fraud,misrepresentation, mistake au undue influence.tukizungumzia undue influence,hii maana yake ni mtu unakuwa katika nafasi ya kuweka mazingira ya mkataba yawe katika kukufavour wewe na hivyo basi kuleta unfair advantage juu ya mtu mwingine kwenye huo mkataba,na hii position kwa mujibu wa sheria yetu inapatikana pale ambapo (a) unapoingia katika mkataba na MTU ambae akili yake ipo affected temporary au permanent kwa sababu ya umri,ugonjwa,bodily distress nk.
(B) mnapokuwa katika fiduciary relationship,ikimaanisha mahusiano ambayo mtu anakuwa amekuamini Wewe kudeal na masuala yake yoyote yale iwe kibiashara au suala lolote lile.hatujauona mkataba wa siada karoli na huyo muta,but mazingira yanaonyesha kuwa walikuwa na fiduciary relationship,na kwamba saida karoli pindi anasaini huo mkataba alikuwa ameweka trust yote kwa huyo muta kuwa pengine labda atamtoa katika umasikini kutokana na kumsimamia kwenye muziki au any other reason,kitu kilichopelekea huyo muta kuexert undue influence over saida karoli kwenye huo mkataba.na mkataba wowote ule ambao consent imetolewa kutokana na undue influence or factors ambazo nimeshazitaja then,huyo mkataba unaweza kuvunjwa kabisa,so naamini saida akipata wakili mzuri anaweza fanikiwa.
 
Mkuu nimekupata vizuri, tatizo watanzania wengi ni watoaji wazuri Wa dosari lkn si watoa solution. Tangu miaka ile watu walijua mkataba wa Saida ni wa kinyonyaji lkn hakuna aliyejitolea kumsaidia.
Nakumbumbuka huyo manager wa Saida alishawahi kuhojiwa na radio moja zamani kidogo akawa anajitetea eti Saida alijifilisi mwenyewe. Jamaa alidai eti Saida alipolijua jiji akawa naye anaishi kusupastaa, kipindi chote alichokuwa DSM bidada alikuwa anaishi hotelini.Huyo manager a.k.a Carl Peters alidai eti Saida alikuwa anatumia pesa kwa fujo matumizi yake kwa siku yalikuwa karibia laki 5 na kipindi hicho laki tano ilikuwa kubwa kwa mtu kuitumia kwa siku. Carl Peters alidai mara kwa mara alikuwa akimshauri Saida kupunguza matumizi lkn bidada hakusikia kwani jiji lilimlevya.Hivyo umasikini wa Saida alijitakia.
Kwa hiyo tukiacha kuwa mkataba ulimnyonya Saida lkn hata hicho kidogo alichopata bidada alikitumia vibaya.
Hilo la Watanzania ni sahihi kwa 100%... sisi ni wataalamu wa kukosoa; tena sio kukosoa ni kuponda lakini hatutoi way forward! Na tatizo kubwa kabisa hapa ni kwamba watu huwa tunataka kukosoa hata kwa mambo tusiyoyajua... tunatawaliwa zaidi na ushabiki kuliko weledi!!

Tukirudi kwa Saida na matanuzi... usimkatalie moja kwa moja huyo meneja wake hasa tukizungumzia suala la kufulia mapema kiuchumi! Hicho ndicho nilichokisema kwenye post yangu ya kwanza... kwamba, ukiwa signed kwenye music label unatakiwa kuwa akili kunkichwa!! Aliyekusaini ukimtaka akuweke hotelini na akijua thamani yako inalipa; atakuweka tu hotelini ili uendelee kuwa tegemezi! Ukipata dharura ya kwenda Dodoma ukamwambia umechoka huwezi kupanda gari kwahiyo akukodie helicopter... trust me; atakukodia! Na hata usipomtaka afanye hivyo, si ajabu yeye ndo akakushauri ufanye hivyo! At the end of the day, umeuza album au show ya ile nyingi, anaanza kutungua gharama zake moja baada ya nyingine... hadi ile ambayo alikununulia mishikaki ya kuku! Anajua asipofanya hivyo, anaweza kujikuta katika mkupuo mmoja tu wa malipo anatakiwa kukulipa mamilioni ya pesa kwa sababu hukuchukua chochote in advance... sasa bora akumegee kidogo kidogo! Sasa msanii mwenyewe ukiwa f'ara ukadhani maisha si ndo haya; hesabu umeumia!!!!

Kuhusu mkataba wenyewe, Saida simlaumu kabisa hasa nikizingatia background yake lakini meneja wake anastahili lawama labda kama na yeye aliirukia kazi asiyo na ufahamu nayo!

Binafsi nishawahi kuiona mikataba miwili mitatu ya wasanii... ndo vile tu watoa mikataba na wapewa mikataba wote sawa tu! Mikataba karibu yote niliyopata kuiona ni ya kishenzi dhidi ya wasanii hususani kama msanii mwenyewe ndo anatafuta kutoka! Na mingi huwa haisemi faida mbalimbali zinazotokana na kazi za kisanii... wanaishia tu kutaja shows, mkito, mapato ya airtime!! Wala hawajui kwamba mtu anaweza kutumia track kutengeneza filamu... and if that happens, nani atapata nini... huwezi kukuta mambo kama hayo!
 
Wana jamvi naomba tuweke michango yetu hapa..kwayeyote mwenye uelewa kuhusu hili jambo..Kama mambo tunayoyasikia ni ya kweli hivi inawezekanaje mtu unaimba nyimbo halafu unakosa haki ya kuzitumia na wakati sauti ni yako na kila mtu analitambua hilo,mfano nasikia SAIDA KAROLI hawezi kutumia nyimbo zake popote pale kama MZEE MUTA akigoma,hebu nipeni ufafanuzi kidogo hapo maana bado niko 3G kuhusu hilo.
kama mkataba wao unataka hivyo ni sawa tu,Saida atakua kauza sauti kwa FM
 
Huwa namwonea huruma sana Saida Kalori, naona kama ni msanii mzuri ila anayenyonywa to the maximum
 
Ana kipaji,kpaji hakifi aachane nae aanze upya kuimba
 
Wasanii wabadilike sasa.. washtuke ..wajarib kuwatumia wanasheria wapo kibao mtaani hawana kazi... mutta hajafanya fair.. jasho la mtu haliliwi lazima imtokee puani..
Tena,i pray in the name of Jesus,soon imtokee puani voz alijua kuwa anamdhulumu!
 
Cha kwanza ambacho kingefanyika kwa Sasa ni yeye saida kurekodi wimbo mpya utakoa muweka barabarani, najua kutoka hapo pakuanzia patapatikana na saida atakaa kwenye ramani
 
Back
Top Bottom