Mzee Muta alivyomfunga miguu Saida Karoli

Mzee Muta alivyomfunga miguu Saida Karoli

Hilo la Watanzania ni sahihi kwa 100%... sisi ni wataalamu wa kukosoa; tena sio kukosoa ni kuponda lakini hatutoi way forward! Na tatizo kubwa kabisa hapa ni kwamba watu huwa tunataka kukosoa hata kwa mambo tusiyoyajua... tunatawaliwa zaidi na ushabiki kuliko weledi!!

Tukirudi kwa Saida na matanuzi... usimkatalie moja kwa moja huyo meneja wake hasa tukizungumzia suala la kufulia mapema kiuchumi! Hicho ndicho nilichokisema kwenye post yangu ya kwanza... kwamba, ukiwa signed kwenye music label unatakiwa kuwa akili kunkichwa!! Aliyekusaini ukimtaka akuweke hotelini na akijua thamani yako inalipa; atakuweka tu hotelini ili uendelee kuwa tegemezi! Ukipata dharura ya kwenda Dodoma ukamwambia umechoka huwezi kupanda gari kwahiyo akukodie helicopter... trust me; atakukodia! Na hata usipomtaka afanye hivyo, si ajabu yeye ndo akakushauri ufanye hivyo! At the end of the day, umeuza album au show ya ile nyingi, anaanza kutungua gharama zake moja baada ya nyingine... hadi ile ambayo alikununulia mishikaki ya kuku! Anajua asipofanya hivyo, anaweza kujikuta katika mkupuo mmoja tu wa malipo anatakiwa kukulipa mamilioni ya pesa kwa sababu hukuchukua chochote in advance... sasa bora akumegee kidogo kidogo! Sasa msanii mwenyewe ukiwa f'ara ukadhani maisha si ndo haya; hesabu umeumia!!!!

Kuhusu mkataba wenyewe, Saida simlaumu kabisa hasa nikizingatia background yake lakini meneja wake anastahili lawama labda kama na yeye aliirukia kazi asiyo na ufahamu nayo!

Binafsi nishawahi kuiona mikataba miwili mitatu ya wasanii... ndo vile tu watoa mikataba na wapewa mikataba wote sawa tu! Mikataba karibu yote niliyopata kuiona ni ya kishenzi dhidi ya wasanii hususani kama msanii mwenyewe ndo anatafuta kutoka! Na mingi huwa haisemi faida mbalimbali zinazotokana na kazi za kisanii... wanaishia tu kutaja shows, mkito, mapato ya airtime!! Wala hawajui kwamba mtu anaweza kutumia track kutengeneza filamu... and if that happens, nani atapata nini... huwezi kukuta mambo kama hayo!
Hofu yangu Saida anafukuzia kuvunja mkataba ili apate hela za diamond na Salome wake au nini....?? Coz zile nyimbo tyri zmebaki makapi zishanyonywa vyakutosha na huyu mzee Mutta. Namkumbka huyu mama nlivokuwa nachungulia drshan kwa jirani baada ya sauti yake iliyonipa kila nlichohitaji, nlkuwa mdogo lakini nlimjua na nlipenda Sauti yake, housgal watu akitafsiri wimbo baada wa mwingine. Alipenda kumshukuru aliemuita "ta muttha" bwana mutta.
Huyu mzee mungu anamuona nlimshangaa sana siku ile ameonekana kwenye media akiwa na meneja wa Diamond baada ya Salome kutoka nilitamani kusikia akisema chochote kuhusu "ma saida"

Bnafsi nlikuwa naskia mengi kuhusu dada yangu huyu kuwa jiji lilimzuzua kupelekea kumuacha mmewe aliyeanza nae maisha kisa sio level zake ambae alishirik kutunga na kuimba viitikio vya nyimbo za kazaa za huyu dada yangu.

Matumiz familia kubwa ya waliokuja kumuona na mambo mengine yalikuwa ni mambo ya kawaida kwa uyu dada aliotoka "obhighem" na kutua jiji la makamba enzi izo....hatua kubwa

Yote kwa Yote mzee muta ni mnyonyoji sana alimtumia na bila ukakasi hawa wanyonyaji wako tele na wanajuana na kuteteana. nilishangaa siku namsikia Ruge akimtetea mzee muta kuwa alimsaidia Saida kwa kumtoa ila watu wanamsakama muta.. (Kuweka kumbukumbu sawa hii ilikuwa siku ameitwa kwenye PB kuonglea ishu yake na Jide) maajab yaliyoje unaendesha hammer mwenzio hta baiskel hana...afu useme umemsaidia...km aliona matumizi mabovu kwnn haku opt ata kumnunulia nyumba kumuanzshia chchte au kumpa haki ya albam moja....

Mutta aache unafiki yule ni "nshomire" mwenzie vijiji jiran amlegezee hata kwa hiki kidogo cha diamond...awe muungwana amwachie hata ivyo vijisent vya Salome mpya wa Diamond.....

......................Am out.................
 
Mkuu, inawezekana na mimi ni mnyonyaji ninaetetea wanyonyaji lakini tatizo langu huwa napenda kuongelea mambo kutokana na uhalisia wake... how they happen in a real world rather than pretending I am living in a fantasy world!!

Kama ulivyosema, Mutta ni mnyonyaji... hilo halina ubishi hata chembe! Hata hivyo, kama tulivyosema; tasnia mzima ya burudani ni full unyonyaji... iwe Tanzania, Uchina, Arabia au Amerika... kote huko wamejaa wanyonyaji hususani kwenye tasnia ya burudani!Nilisema hapo kabla, hata Mike Tyson na ubabe wake wote... na usela wake wote wa kukulia Brooklyn, bado nae hakusalimika na mikono ya Don King!! Kuna mtu mmoja... ni Mmarekani Mzungu huyu! Wakati anahangaika kupenya kwenye mageti ya Hollywood, aliamua ku-opt kufanya kazi kama mlinzi wa getini kwenye studio ya 21st Century Fox! Now tell me, hivi mtu kama huyu kama angekutana na industrial insider akamwambia, "okay, I will give you an opportunity to act for no payment...!" Unadhani angekataa huyu?! Asikudanganye mtu... haya yapo kila mahali! Google kitu kinaitwa Zero Dollar Screenplay Option, or Dollar Screenplay option! Ni nini hii? Asikudanganye, hakuna kazi ngumu kama uandishi wa movie script! Sasa ilivyo kwa Hollywood, ni mara chache unaweza kuuza script papo kwa papo... wanaanza ku-option! ku-option maana yake ni kwamba, ikiwa mmekubaliana bei ya script ni $100,000; unaweza kulipwa 10% ya hiyo 100K! Hiyo 10% inaitwa Option Price! Lakini wakati mwingine inatokea Dollar option... what does it mean? Mwandishi "unalipwa" $1 (dolar 1) as option price na sometimes unaweza usipewe hata senti moja... hiyo ndiyo inaitwa Zero Dollar option! So, that's what is happening in the real world! Kwahiyo Mzee Mutta isn't an exceptional monster under the sun but the whole industry is full of monsters!

Sasa ili kukabiliana na hao monsters ndipo wasanii wanashauriwa kutumia wanasheria. Na ili kuhakikisha mambo yao hayakwami mahali, wanatakiwa pia kuwa na mameneja wanaoifahamu tasnia vizuri!! Kwamba ikiwa Saida alikuwa na matumizi mabovu kwanini basi Mzee Mutta haku-opt kumnunulia nyumba... huo ulikuwa ni wajibu wa Meneja wake; kuhakikisha hatoki nje ya mstari! Mzee Mutta alikuwa anafanya biashara na Saida... mmoja anatoa huduma za kipaji chake na mwingine anatoa huduma ya ku-transform hicho kipaji into money... hii ndiyo Mutta-Saida relationship! Katikati ya Mutta-Saida relationship ndipo anasimama meneja atakayehakikisha brand yake haiwi full exploited for nothing!!! Ni kama leo hii Ali Kiba na Sony... hapa kati kati kuna Rockstar4000... hawa ndio wanatakiwa kuhakikisha Kiba hawi exploited to nothing kwavile wasipofanya hivyo, Sony watam-exploit tu... wakikuona huna thamani tena wanakubwaga wanachukua mwingine! That's how these things work... hapa ndipo watu wanaposhindwa kumuelewa Sallam wa Diamond hadi watu wanamuhusisha na Uarabu wake!! Kumbe kimsingi, yeye kama Meneja anafahamu ana wajibu wa kuilinda brand yake!
 
Wengi mtamlaumu Saida lakini ukweli ni kuwa "Saida karoli hakuwa na elimu wala hakupata mchangamano na watu ambao wangembadilisha kifikra "...

Huyu mama alitolewa kwenye upigaji wa ngoma vilabuni huko bukoba na tuzo yake pekee ilikuwa ni pombe... Hadi anakuja kuchukuliwa na hao walaghai na kuanza kumfanyisha matamasha ya kiasili , sidhani kama hata malipo kiduchu aliyolipwa yalimtoa ushamba kutokana na kuwa hakuizoea pesa "....

Hadi anakuja kuwa msanii mkubwa , yeye hakuijua thamani yake kabisa na alipokuja kushtushwa ndipo ukawa mwisho wake maana alitelekezwa mjini hadi akaanza kuuza chips.....

Mutta sidhani kama ana utu maana kwa pesa za kuujaza uwanja wa taifa ilipaswa amnufaishe japo kidogo...

Yote kwa yote... Tayari Saida amekwishajua wapi alipokosea hivyo, hapaswi kudai hadhi na haki yake kwa mdomo Bali kwa vitendo
Afu majamaa fulani wakamrusha kwenye kipindi cha kuchekesha kipengele cha 'Umefulia'... Kisa wao maisha yalikuwa mazuri kwa Mehboob.
Tujikumbushe; Saida Karoli - Wikipedia
 
Back
Top Bottom