Mzee Mwinyi: Nilijilaumu kwa kuliachia Bunge hadi likapitisha hoja ya Serikali ya Tanganyika, Mtikila aliisumbua Serikali yangu

Mama Samia yeye ataandika kitabu akistaafu ndan yake atasema NAJILAUMU KWA KUMUACHIA NDUGAI KUWAKUMBATIA COVD19
Pigo lake la kwanza lazima liwe lile la match ya Simba dhidi ya Yanga. Atajilaumu sana.
 
Kama jiwe tulivyo aminishwa ni mwadilifu kumbe sivyo, kwamba ni zawadi kutoka kwa mola kumbe ni adhabu, na ndiye alitugawa watanzania na kuleta chuki za kivyama.
 
Huyu mzee ni mpuuzi. Nothing special.

Alivyoliacha bunge, kwahiyo alitaka alitaka alifanyeje bunge?
Bunge ni huru kinadharia, lakini kwenye utendaji halina uhuru wowote. Hakuna kitu serikali inataka ikashindwa kupata, kulazimisha wabunge kuwa wanatoka kwenye vyama kumetengeneza utumwa wa bunge. Leo hii Mama Samia ni mwenyekiti wa CCM na ni Rais pia; Ndugai hana cha kusema kwa Samia, akileta vyokovyoko Uspika ataukosa. Ndicho kilichomponza Sitta mzee wa speed and standards, aliitesa serikali ya Kikwete akisahau kuwa JK ni chairman, ilipofika kupitisha majina ya kugombea Uspika 2010, akamla kichwa.

Ndio point ya Mwinyi hiyo, kwamba angeweza kuwadhibiti kwenye chama wasipeleke "ujinga" bungeni.
 
Reactions: SMU
Ana confirm indirectly namna bunge letu "linavyosimamiwa" na serikali?

Kwani kikatiba yeye kama Rais alikua na mamlaka ya kuzuia au kuamua aina ya mijadala au hoja zinazoletwa bungeni na wabunge? Kuna la kujifunza hapa.
 
Mkuu ndani ya muda mfupi Magu alikuwa amesha-consolidate power kupindukia. Wabunge wote kawaweka yeye, anaendesha mahakama atajavyo yeye, media, wasanii, viongozi wa dini ?

Hii 10 tu, tulikuwa tunaelekea kiama. Na hata kama angeondoka 2025 bado angeweka mtu wake kibabe tu na hakuna mtu angemfanya chochote.
 
Nikikumbuka heka heka, Maarifa ya kujenga na kupangua hoja ya enzi zile ukimkuta Huku Malecela, kule Kolimba, Huku Mtikila, kule Njelu, kocha Mchezaji Kambarage, kule Pius Msekwa, Mama Getrude Mongela huku Sebastian Kinyondo kule Tuntemeke Sanga kule Kimbau wa Mafya…kweli zama zile hazirudi

Siku hizi tuna kina Ndugai, Kigwangala, Deo Sanga, Msukuma

Innalillah wainaa ilayh rajiuun!
 
Hahahaaaa....... Kigwangalla, Kibajaji, Musukuma yaani full comedy!
 
Hahaha alimuuliza malecera,moja jumlisha moja ni ngapi?akajibiwa mbili,akamwambia sasa wewe hiyo serikali tatu unazitoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…