Mzee Mwinyi: Nilijilaumu kwa kuliachia Bunge hadi likapitisha hoja ya Serikali ya Tanganyika, Mtikila aliisumbua Serikali yangu

Mzee Mwinyi: Nilijilaumu kwa kuliachia Bunge hadi likapitisha hoja ya Serikali ya Tanganyika, Mtikila aliisumbua Serikali yangu

Mama Samia yeye ataandika kitabu akistaafu ndan yake atasema NAJILAUMU KWA KUMUACHIA NDUGAI KUWAKUMBATIA COVD19
Pigo lake la kwanza lazima liwe lile la match ya Simba dhidi ya Yanga. Atajilaumu sana.
 
Mtikila alikuwa mchochezi aliye tumwa akatumika vilivyo.
Tabia kama hizo zisijirudie ktk tawala za sasa na zijazo.

kamwe asivumiliwe mtu au kikundi cha watu wenye nia ya kutugawa kwa misingi ya kiimani, rangi au kikabila.

Yunajifumza kuyoka ktk kitabu chake kuwa;

unaweza kuwa kiongozi mwadilifu lkn bado uadilifu wako ukachafuliwa kwa maksudi na watu wabaya na ukaonekana hufai mbele ya jamii, na kinyume chake kwa hila na hadaa viongozi wasio waadilifu wakaonekana kuwa waadilifu.
Kama jiwe tulivyo aminishwa ni mwadilifu kumbe sivyo, kwamba ni zawadi kutoka kwa mola kumbe ni adhabu, na ndiye alitugawa watanzania na kuleta chuki za kivyama.
 
Huyu mzee ni mpuuzi. Nothing special.

Alivyoliacha bunge, kwahiyo alitaka alitaka alifanyeje bunge?
Bunge ni huru kinadharia, lakini kwenye utendaji halina uhuru wowote. Hakuna kitu serikali inataka ikashindwa kupata, kulazimisha wabunge kuwa wanatoka kwenye vyama kumetengeneza utumwa wa bunge. Leo hii Mama Samia ni mwenyekiti wa CCM na ni Rais pia; Ndugai hana cha kusema kwa Samia, akileta vyokovyoko Uspika ataukosa. Ndicho kilichomponza Sitta mzee wa speed and standards, aliitesa serikali ya Kikwete akisahau kuwa JK ni chairman, ilipofika kupitisha majina ya kugombea Uspika 2010, akamla kichwa.

Ndio point ya Mwinyi hiyo, kwamba angeweza kuwadhibiti kwenye chama wasipeleke "ujinga" bungeni.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ana confirm indirectly namna bunge letu "linavyosimamiwa" na serikali?

Kwani kikatiba yeye kama Rais alikua na mamlaka ya kuzuia au kuamua aina ya mijadala au hoja zinazoletwa bungeni na wabunge? Kuna la kujifunza hapa.
 
Mkuu alikuwa bado kufikia level ya dikteta kamili. Aise Kuna watu walikuwa waovu walipokuwa madarakani, mfno; Bokassa, Idd Amin. Enzi za utawala wa Amini, alifuta Bunge, badala yake akawa na Baraza la kijeshi lililoamua hatma ya Jambo. Brigedia Isack Maliyamungu au Isack Lugola, alikuwa mtu wa kutisha sana, ambaye kwa mjibu wa maandishi yaliyopo, alikuwa anaua hovyo hovyo watu.
Mkuu ndani ya muda mfupi Magu alikuwa amesha-consolidate power kupindukia. Wabunge wote kawaweka yeye, anaendesha mahakama atajavyo yeye, media, wasanii, viongozi wa dini ?

Hii 10 tu, tulikuwa tunaelekea kiama. Na hata kama angeondoka 2025 bado angeweka mtu wake kibabe tu na hakuna mtu angemfanya chochote.
 
Nikikumbuka heka heka, Maarifa ya kujenga na kupangua hoja ya enzi zile ukimkuta Huku Malecela, kule Kolimba, Huku Mtikila, kule Njelu, kocha Mchezaji Kambarage, kule Pius Msekwa, Mama Getrude Mongela huku Sebastian Kinyondo kule Tuntemeke Sanga kule Kimbau wa Mafya…kweli zama zile hazirudi

Siku hizi tuna kina Ndugai, Kigwangala, Deo Sanga, Msukuma

Innalillah wainaa ilayh rajiuun!
Mtikila alianzisha hoja za serikali ya Tanganyika..
Lengo ilikuwa kumdhoofisha Mwinyi..

Kina Njelu kasaka wakaikubali..

Malecela alivyokuwa PM pengine Kwa tamaa ya madaraka akaikubali
Pengine aliona Mwinyi atarudi Zenji..yeye ata take over..

Leo tunagundua kumbe Mwinyi ni Mtanganyika...

Nyerere wakati anavunja G 55 alisema kuna watu hawataki Muungano Kwa sababu ya Wazanzibari wengi ni waislam..

Je bara hakuna waislam?

Nyerere ndo akamkomalia Malecela ajiuzulu na Kolimba ..

Leo hakuna anaejua ingekuwaje
 
Hahahaaaa....... Kigwangalla, Kibajaji, Musukuma yaani full comedy!
 
Mtikila alianzisha hoja za serikali ya Tanganyika..
Lengo ilikuwa kumdhoofisha Mwinyi..

Kina Njelu kasaka wakaikubali..

Malecela alivyokuwa PM pengine Kwa tamaa ya madaraka akaikubali
Pengine aliona Mwinyi atarudi Zenji..yeye ata take over..

Leo tunagundua kumbe Mwinyi ni Mtanganyika...

Nyerere wakati anavunja G 55 alisema kuna watu hawataki Muungano Kwa sababu ya Wazanzibari wengi ni waislam..

Je bara hakuna waislam?

Nyerere ndo akamkomalia Malecela ajiuzulu na Kolimba ..

Leo hakuna anaejua ingekuwaje
Hahaha alimuuliza malecera,moja jumlisha moja ni ngapi?akajibiwa mbili,akamwambia sasa wewe hiyo serikali tatu unazitoa wapi?
 
Back
Top Bottom