"Mimi ni mzee sasa na maneno yangu pengine hudhaniwa ndoto za uzee. Ningetamani mambo mawili, moja la hakika lingine la kufikiriwa. La hakika tuwashawishi watanzania Rais wetu asipate kura ya kumkataa, mwenye kumkataa atupe sababu. La kufikirika ni kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba na lazima tuienzi.
Lakini twaweza kuiahirisha kwa muda ili kumpa Rais Magufuli kipindi kingine kimoja cha asante kisha baadaye tuendelee vilevile, kwa sababu kuna mengi aliyonayo Magufuli akiondoka (baada miaka kumi) nchi itayakosa” Ali Hassan Mwinyi, Rais wa pili wa Tanzania na Rais wa 3 wa Zanzibar.
View attachment 1503855