SoC01 Mzee na Kundi la Vijana

SoC01 Mzee na Kundi la Vijana

Stories of Change - 2021 Competition

ihama107

Member
Joined
Jul 22, 2021
Posts
6
Reaction score
3
BABU_Moment.jpg


Na ISMAIL MAYUMBA

Kundi la vijana wakiwa kwenye mgahawa ambao ulio wazi kiasi cha wapita njia kuwaona. Vijana wakiwa wanakula chakula na kufurahi na hata pale walipotosheka na chakula bado waliagiza kingine na kukichezea. Mzee akapita akiwa na mkongojo wake unaomsaidia kutembea. Akawaona na akatingisha kichwa chake na kuendelea na safari. Vijana wakaona kama ni dhihaka hivyo wakamuita na mzee akaja mpaka karibu yao.

'Mzee hii ni hela yetu na tumefanya jitahada kuipata na ni jasho letu. Kuna dhulma yoyote tukitumia jinsi tunavyotaka?' Mmoja wa vijana akamuuliza mzee

'Kwa ajili gani usitoe kwa yatima kile ambacho Mungu kakuongezea kwenye kile ulichokuwa unakihitaji' Mzee akamshauri

'Ni hesabu za kawaida sana mzee. Sisi tukiwapa wao watakuwa wenye kunufaika na kuongezeka kwa mali zao wakati sisi tutakuwa wenye kupungukiwa mali na mwishowe wao watakuwa matajiri na sisi tutakuwa maskini' Kijana mwengine akamjibu huku akichezea chakula

'Ujinga wenu hauna tofauti na yule mtu aliekataa kuchangia damu kuhofia damu yake itapungua na wale anaowachangia damu watakuwa ni wenye kunufaika' Mzee akaongea kwa hasira

Baada ya hayo maneno, mzee akaamua kuondoka na kuwaacha vijana kwenye bumbuwazi kwa sababu hawakumuelewa. Wote wakaamua kumuita kabla hajapotea kwenye mboni zao. Wakamuita na akarudi kuwasikiliza. Kwa heshima wakamuomba awafafanulie alichowaambia

'Mtu aliyekataa kuchangia damu akawa anamcheka mtu ambaye anachangia damu hospitalini kwa kigezo kuwa anapoteza damu yake na atakufa kwa kupungiwa damu mwilini. Baada ya daktari kusikiliza sababu za huyo mtu akamwambia kuwa kutoa damu yako haimaanishi kuwa utapungukiwa damu yako. Mwili una uwezo wa kutengeneza damu kwa kiwango ulichokitoa hivyo hufidia damu uliyoitoa. Kuchangia damu kuna faida kadha wa kadha kama kuainisha magonjwa mbalimbali, kupunguza chummvi mwilini kama unayo nyingi, kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kupunguza hatari ya kupata kansa na zingine nyingi. Na faida nyingine ni kuwa yule uliyemchangia damu atakushukuru kwa aina yake na atakuwepo kutoa msaada pale wewe unapohitaji damu au jamaa zako wa karibu. Kwani hakuna aijuaye kesho

Ninachomaanisha ni kwamba ukitoa mali zako kuwasaidia ambao hawana si kwamba utapungukiwa ila Mungu atakupa njia za kuirudisha hiyo mali na hata kukupa zaidi kwa mapenzi yake. Kadri unavyotoa Mungu anakupa baraka kwenye biashara zako na utakuwa mwenye kupata faida ya juu na ya halali. Hakuna ajuaye kesho! Unaweza ukawa tajiri leo na kesho ukawa maskini.

Kama ulikuwa mtu wa kusaidia watu ulivokuwa na mali basi utasaidiwa pale utakapopoteza mali zako na utapata heshima ile ile uliokuwa nayo pindi ulivokuwa na mali' Baada ya mzee kutoa maelezo hayo marefu, vijana wakawa wenye kujuta na kuahidi kubadilika na kusaidia watu wenye kutaka msaada.

MWANDISHI- ISMAIL MAYUMBA
MAWASILIANO- 0624000455
 
Upvote 3
Na imani mtaisoma kazi yangu ya uandishi na kunipigia kura ili niweze kuwa mshindi 🙏 🙏 🙏
 
Back
Top Bottom