"historia hii ilivyobadili historia ya TANU"
Historia ipi ilibadili historia ya TANU ??? Historia ya TANU ilibadili historia ya TANU?
Na ni nani aliyepata ghadhabu kwa sababu ya hiyo historia, mkoloni ???
Taso,
Ghadhabu inajidhihirisha kwenye kauli na maneno yako makali.
Ghadhabu ni dalili ya kushindwa hoja.
Mwenye hoja akasiriki.
Unauliza historia ipi imebadili historia ya TANU.
Kabla ya kuandika kitabu uliwajua viongozi wa harakati za uhuru kama Hamza Mwapachu na Sheikh Hassan bin Ameir kwa kukutajia najina mawili tu?
Kuna mahali popote ulipatapo kusoma historia zao?
Achilia mbali Abdul Sykes na Chief David Kidaha Makwaia mazungumzo yao kati ya 1950 - 1952 nyumbani kwa Abdul Sykes ya kuunda TANU.
Ulipatapo kusoma popote Chief Kidaha akihusishwa na kuundwa kwa TANU?
Dr. Michael Lugazia je?
Dr. Luciano Tsere, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Wilbard Mwanjisi na Dr. Vedasto Kyaruzi?
Vipi kuhusu Schneider Abdillah Plantan?
Mtoto wa Chief Mohosh kutoka Kwa Likunyi, Imhambane Mozambique unajua kama yeye na Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ndiyo walioutoa uongozi wa wazee ili kuingiza vijana kudai uhuru?
Aliyetolewa urais wa TAA ni Thomas Saudtz Plantan kaka yake Schneider.
Tuwaache hawa Wazulu.
Mkenya Dome Budohi na Mnyasa Denis Phombea kadi zao za TANU No. 5 na 6.
Ulipata popote kuwasoma popote?
Ulipata kuujua udugu uliokuwapo baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere udugu uliojengeka katika kupigania uhuru wa Tanganyika kiasi Mwalimu baada ya kujiuzulu kazi aliishi nyumbani kwa Abdul?
Hustaajabu?
Ulipata kusoma popote pale kuwa Nyerere alipokelewa na Abdul Sykes na aliwahi kugombea nafasi ya urais wa TAA na Abdul Sykes?
Ulipata hata siku moja kusoma mahali popote kuwa Abdul alikutana na Jomo Kenyatta Nairobi katika mkutano wa siri?
Abdul alikuwa na umri wa miaka 26.
Au ulijua kama Abdul Sykes aliacha nyaraka zinazoeleza historia nzima ya mapambano ya kupambana na ukoloni wa Waingereza?
Ulipatapo popote pale kusikia haya?
Unadhani baada ya mimi kueleza haya yote historia imebakia ile ile?
Kweli, kweli tuifute historia hii yote?
Hii ndiyo faida ya kuzaliwa Gerezani na kuzaliwa katika kipindi kile na kuzaliwa na wazee hawa.
Historia ya babu yangu ndiyo historia yangu simuhitaji Mzee Pius Msekwa anifunze historia yangu na akikosea kuieleza mimi namsahihisha kuwa haikuwa hivyo ilikuwa hivi.