Mzee ruksa awalipua viongozi mafisadi

Mzee ruksa awalipua viongozi mafisadi

..hoja ya kupinga vita ufisadi imeshatekwa nyara na CCM.

..wapiganaji wameonyesha their true colors kwa kumsafisha JK pale wanapodai kwamba anaongoza vita dhidi ya mafisadi.

..baada ya kumaliza hilo hapo juu wameanza kukipamba chama chao mbele ya wananchi kwamba hakikumbatii ufisadi.

NB:

..kwa baadhi yetu ufisadi[madawa ya kulevya, utoroshwaji madini, usambazaji noti bandia, ukwepaji kodi,...] ulishamiri sana wakati wa utawala wa Mzee Ruksa.

..leo hii magazeti kumuandika Mzee Ruksa ati amewalipua mafisadi ni kujaribu kuchezea akili za wananchi.
 
Tutaona mengi sana kila tunapoelekea kwenye uchanguzi mkuu, Tatizo moja ni kuwa CCM hawawezi kujitengeanisha na ufisadi na ndio maana wanajaribu kufuata maoni ya watu, Labda Dr. Slaa ndiye anaweza kusema kuwa Mwinyi yupo sahihi au vipi?? Lakini wote ni wamoja na Wanachofanya ni kublind Watanzania na kutuzuga, Mwakyembe, Selelii, Kilango Waseme ni nani Fisadi yupo CCM?? Kama kwa tabia hii Watanzania wanachanganyikiwa mithili ya kichaa vile, CCM watajane Mafisadi au ile Orodha ya Dr Slaa ndio wanakubaliano nayo
 
Kilicho mliza Kilango sio Ufisadi, Kilango anajua Sangara wanamwagwa Moshi na Sangara watagawanywa Same wiki ijayo anajua utamu wa Sangara wa Chadema kwa wananchi ulivyo.

Kilango alichuana vikali sana na Mziray ambaye alikuwa na vitendea kazi duni, Je atamweza Sangara na Chopa juu ya hiyo milima ya Pare. Kilango anakaa Dar es salaam na kwenda Same kusalimia tu na kutoa machozi.

Badala ya kulia aeleze ametimiza vipi ahadi zake, ili wananchi wajue mtaji wao. Uchungu wa mumewe kupigwa chini unamtoa machozi kila siku.

Mkuu Kinepi hapo kwenye boldface nakubaliana nawe vizuri sana.Hawa walishajiandaa kuchukua nchi na mumewe.Sasa Mkapa alipowapiga chini ndipo wakaanza kujifanya wana uchungu na nchi.Hakuna mpiganaji hapa ni opportunist tu huyu mama hana lolote.
 
MZee yote kwa yote tumia busara zako jaribu kukaa na kijana wako dr. hussein mueleweshe maana ya kuwajibika, ile iliyotokea mbagala hana jinsi ni lazima awajibike, kwa heshima yako anaweza akakuelewa
 
..
NB:

..kwa baadhi yetu ufisadi[madawa ya kulevya, utoroshwaji madini, usambazaji noti bandia, ukwepaji kodi,...] ulishamiri sana wakati wa utawala wa Mzee Ruksa.

..leo hii magazeti kumuandika Mzee Ruksa ati amewalipua mafisadi ni kujaribu kuchezea akili za wananchi.
Mkuu wangu hata sielewi kitu hapa nimetoka kapa..
Bila shaka unaelewa wazi kwamba Ubepaari una virusi vyake..na hivi vyote ulivyotaja ni vitu ambavcyo vilitakiwa kuwekewa kinga kabla hata ya kuingia Ubepari..
Bila shaka vilianza wakati wa Mwinyi, lakini sino sababu kabisa ya kusema magazeti yanasema vimelipuka wakati wa Mkapa wakati ndio ukweli wenyewe..Unachojaribu kupinga hapa hakina tofauti na baadhi ya watu wanaodai kwamba HIV ilianzia Uganda kuwa ndio sababu badala ya kufikiria tiba ya maradhi hayo kwa waathirika wetu..
Binafsi nadhani wakati wa kunyoosha vidole umepita, iwe hapa kijiweni au hao viongozi kwani kusema sana sii kutibu maradhi hata kidogo.. Tujiulize ni hatua gani hutumiwa kupambana na Pandemic.
1.Karantini na kuwatibu Wagonjwa...(kama dawa ipo), ambayo ni sawa na Kuwaondoa ktk Uongozi, kutaifisha mali zao, na kuwafunga mafisadi.
2. CHANJO kwa wananchi wote, ambayo ni sawa na kuweka sheria kali za kinga dhidi ya Ufisadi.
Hizi habari za viopngozi na sisi wananchi kuendelea kulaani Ufisadi wakati virusi vyake vinazidi kujijenga ndani ya cells za miili yetu ni kupoteza wakati na ubabaishaji wa siasa sizizojenga.
 
ndio maana huwa naikataa ile concept ya kwamba aliyekosea hawezi kufanya/kusema jambo jema........"eti hana moral nini sijui.......".....damn!......
 
  • ASEMA WALIOJIPENYEZA MADARAKANI, SASA WANAUMBUKA
Daniel Mjema, Same

RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi amelipua kombora jingine kwa viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, akisema kuwa walijipenyeza kwa bahati mbaya kushika uongozi, lakini sasa wanahaha.

Mwinyi anaongoza kamati ya watu watatu iliyoundwa na Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kuchunguza chanzo cha wanachama na viongozi wa chama hicho tawala kuchukiana kiasi cha kurushiana maneno makali wakati wa kikao hicho na kupendekeza hatua za kuchukuliwa.

Maneno hayo makali yalitokana na baadhi ya wanachama kutaka kulinyamazisha kundi ambalo limekuwa likijinadi kuwa linaongoza vita dhidi ya ufisadi ambayo watuhumiwa wa ufisadi waliitafsiri kuwa inakichafua chama na serikali yake.

Lakini jana Mwinyi alirusha maneno makali dhidi ya watuhumiwa hao wa ufisadi, akisema wameshikwa pabaya.

Mwinyi, ambaye aliongoza serikali ya awamu ya pili iliyoruhusu mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kiasi cha kupewa jina la Mzee Ruksa, alisema viongozi hao sasa wanafedheheka kutokana na kushikwa pabaya.

Ingawa hakutaka kufafanua alikuwa na maana gani, Mzee Mwinyi, ambaye alikuwa akizungumza kwenye kijiji cha Ndungu wilayani Same ambako alialikwa kuzindua wodi ya wazazi, alisema watu hao sasa wako kwenye wakati mgumu.

Mwinyi hakutaja majina ya viongozi ambao wameshikwa pabaya lakini katika siku za karibuni baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na maofisa waandamizi wa Benki Kuu (BoT) wamefikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ya ufisadi, ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya na kuisababishia hasara serikali, wizi na njama za wizi wa fedha za umma.

Kundi la watu hao limekuwa likisakamwa na wapiganaji hao wa vita ya ufisadi ambao wanataka viongozi wengi zaidi wafikishwe mbele ya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mwinyi alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye ni mmoja wa vinara wa vita ya ufisadi, kububujikwa na machozi kuonyesha jinsi anavyokerwa na tatizo la ufisadi nchini huku akiapa kuendeleza vita hiyo.

Mwinyi alisema Kilango amekuwa akikerwa na tatizo hilo kwa kuwa anaguswa sana na maendeleo ya wananchi.

"Hakuna mwenye shaka na uzuri na usafi wa uongozi wa Kilango... kiongozi mzuri lazima awe na sifa 10 ikiwamo huruma na hiyo ndiyo iliyomfanya Mama Kilango alie leo kuelezea machungu aliyonayo," alisema.

"Ndio maana unamuona Mama Kilango anabwata kule Bungeni kwa nguvu zake zote akiona kuna dalili za uhaini ambao utawapokonya watu wake maendeleo... anasema sikubali na nyote mnafahamu."

Akizungumza katika sherehe hizo Mzee Mwinyi alimwelezea Kilango kama kiongozi wa kweli mwenye kipawa adimu cha kuongoza Watanzania katika misingi ya uadilifu.

"Aliyekosa kipawa hicho hawi kiongozi mzuri... na kiongozi wa namna hiyo akijipenyeza kwa bahati mbaya ndio hao wanaofedheheka ni waliofanya ufisadi na sasa wameshikwa," alisema Mwinyi.

Alisema ufisadi si wa wana-CCM, lakini hutokea mmoja au wawili kama vile chuya isivyoweza kukosekana katika mchele mwingi na hiyo huwa ni hila ya chuya na si ya mchele wenyewe.

Kwa mujibu wa mzee Mwinyi, CCM na wanachama wake ni safi na kusisitiza kuwa uongozi ni fani na kipawa na kiongozi mwenye vitu hivyo viwili hajifichi kama ilivyo kwa Kilango.

Huku akitumia maneno ya "asante sana", "hongera sana" na "heko mama Kilango" kuonyesha anavyounga mkono msimamo wa mbunge huyo, Rais Mwinyi alimwelezea mbunge huyo wa Same Mashariki kuwa ni mtu anayeguswa na maendeleo ya Watanzania.

Kilango, ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu tangu Nec imalize kikao kilichoonekana kutaka kuwafumba midomo vinara wa vita ya ufisadi, alibubujikwa machozi alipokuwa akiwahutubia wananchi waliofurika katika sherehe za uzinduzi wa wodi hiyo.

Akizungumza kwa hisia kali, Kilango alisema hakuna jambo linalomuuma kama kuona kiongozi aliyechaguliwa na wananchi ili awatetee, anawageuka na kuwa mla rushwa na kuwaumiza wananchi waliomchagua.

Mbunge huyo aliapa kupambana na mafisadi na wala rushwa hadi kifo na akawataka wananchi wasidanganywe kuwa CCM inakumbatia rushwa.

"Msidanganywe na watu kuwa CCM inakumbatia wala rushwa, hiyo si kweli hata kidogo… mimi ni mbunge wenu wa CCM na siku zote nitapambana na rushwa na siku zote sijawahi kwenda nje ya katiba ya CCM," alisema Kilango.

Kilango, ambaye ni mke wa waziri mkuu wa zamani na mbunge wa jimbo la Mtera John Samuel Malecela, alisema kiapo cha CCM inatambua kuwa rushwa ni adui wa haki na ndio maana mwanachama ni lazima aape kuwa hatatoa wala kupokea rushwa wala kutumia cheo chake au cha mtu mwingine kwa maslahi binafsi.

Mwinyi alitumia mkutano kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Same Mashariki kwa kupata kiongozi mwenye sifa kamili za uongozi kama Mama Kilango na akazitekeleza kwa ukamilifu bila ubaguzi wa rangi, dini, kujuana au jinsia.

Awali akitoa taarifa ya ukarabati wa wodi ya wazazi na watoto ambayo imekarabatiwa kwa kiwango cha juu, mganga mkuu wa wilaya ya Same, Dk Charles Kifunta alisema ukarabati huo umegharimu Sh75 milioni.

Katika mradi huo ambao wananchi wa Ndungu walishirikishwa kwa asilimia 100, nguvu za wananchi ni sawa na Sh5 Milioni na fedha nyingine zilitolewa na Mama Kilango kupitia akaunti ya maendeleo.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi wa serikali, akiwemo mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Monica Mbega, mkuu wa wilaya ya Mwanga na kaimu mkuu wa wilaya ya Same, Athman Mdoe.

Ingawa kauli za Mwinyi hazikuwa wazi, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema ziliashiria kumuunga mkono Kilango na wabunge wenzake katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Wabunge wengine ambao tayari wameapa kula sahani moja na mafisadi ni pamoja na mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni spika wa Bunge la Jamhuri, Samuel Sita na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro.

Wengine wanaotajwa katika orodha ya wabunge hao ni pamoja na Lucas Selelii wa Nzega, Dk. Harrison Mwakyembe wa Kyela.

- Wakuu vipi heshima mbele sana, habari za masiku jamani? Nilikuwa nimebanwa kidogo na bado ninarudi huko maporini si unajua kampeni zimekaribia, na tunaangalia anga za 2015!

- Naona kijiwe ni bomba na kuna habari njema kama hizi za kufunguliwa kwa wodi ya kinamama wajawazito kwa ajili ya jimbo na mkoa, licha mikoa ya jirani, naona hilo halikuonekana kabisa katika hoja nyingi ndani ya hii thread, sometimes tujifunze kushukuru mambo mema kwa wananchi na taifa letu. Mama Kilango Bravo na ubarikiwe kwa hili.

Respect na Ninarudi Maporini tena ndugu zangu, alamsiki nilipita tu kidogo, Bwa! ha!.

Field Marshall Es!
 
Ukishatoa yale maji una fanya rinsing chupa inakuwa 'imesafishika'...si sumu haiwezi kupenya chupa?

haiwezi kusafishika yenyewe, labda kimiujiza, inabidi uisafishe vizuri kabisa kwa kutumia chemikali za ku nutralize hiyo sumu ...vinginevyo tupa chupa nunua mpya
 
  • ASEMA WALIOJIPENYEZA MADARAKANI, SASA WANAUMBUKA
Daniel Mjema, Same

RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi amelipua kombora jingine kwa viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, akisema kuwa walijipenyeza kwa bahati mbaya kushika uongozi, lakini sasa wanahaha.

Alisema ufisadi si wa wana-CCM, lakini hutokea mmoja au wawili kama vile chuya isivyoweza kukosekana katika mchele mwingi na hiyo huwa ni hila ya chuya na si ya mchele wenyewe.

Mbunge huyo aliapa kupambana na mafisadi na wala rushwa hadi kifo na akawataka wananchi wasidanganywe kuwa CCM inakumbatia rushwa. "Msidanganywe na watu kuwa CCM inakumbatia wala rushwa, hiyo si kweli hata kidogo… mimi ni mbunge wenu wa CCM na siku zote nitapambana na rushwa na siku zote sijawahi kwenda nje ya katiba ya CCM," alisema Kilango.

.

mafisadi hawakujipenyeza kwa bahati mbaya walialikwa na walikaribishwa kupitia mlango wa mbele wa CCM, kwa kupewa power ya kugombea majimboni na kupewa nyadhifa muhimu kabisa

Mimi naona hapo ni kinyume chake...gunia hili ni la chuya na punje mbili tatu za mchele

mbona hata hiyo katiba ya CCM inayosema usipokee wala kutoa rushwa hawaikumbatii? takrima sio rushwa?

Hivi hao wapiganaji wakiungana wajitoe CCM waanzishe chama chao itakuwaje?
 
Sidhani kama wapo siriazi kiasi hicho. Wanachofanya ni kuwaziba midomo wale wapiganaji kwa kujifanya wanawaunga mkono. Hana lolote, wale wale tuuuuuuuu
 
Jamani Vita dhidi ya ufisadi waanzilishi ni wakina nani?? CCM walikuwa wapi kipindi chote mpaka sakata la Mwembe yanga temeke?? CCM walete List yao ya Mafisadi labda ndio tunaweza kusema kuwa ni nani safi?? Je nani Fisadi ambaye anapiganiwa ndani ya CHAMA chao kizuri cha CCM
 
Waanzilishi ni CCM wenyewe!
 
Waanzilishi ni CCM wenyewe!
Hapana. Usijaribu kuandika historia upya. Makelele dhidi ya ufisadi yalianza kupigwa na Mzee Slaa. CCM wakamwita kila aina ya majina. Wakasema mambo BOT ni shwari. Au umesahau? Ni kwa nini Meghji alijiuzulu. Usijaribu kuandika historia na sisi watafuta ukweli tukiwa bado hai.
 
Menghji alijiuzulu? hii kali!
 
Nilikuwa nasoma kitabu cha Mwalimu cha freedom utashangaa sana kuona leo viongozi wetu wanajifanya wanafanya yale ya mwalimu lakini ni kinyume kabisa
 
Mzee Rukhsa is the father of change in Tanzania. It was necessary for him to take the country through that route due to the status we had. For those who can remember well: we used not have soap (we used ndulele for washing and some maganda ya miti), there was no garments even in the shops (you can rarely find the american scouts garments), people in southern TZ embarked to magamba ya miti for clothes, we went to school without shoes, the shorts had several virakas, it was a terrible situation. People were really poor. When Mwinyi came he didn't have option to loosen the nuts and lets people trade freely so that you can create a taxable society. When Mkapa came, he taxed the people as they can now pay taxes. So I salute Mzee Mwinyi.
 
Back
Top Bottom