Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Haki daima huwa ni ya asili ni vigumu kuzuia isidaiwe. Sheria ya maisha ya binadamu huonesha ukweli huo. Marekani walidhani kuwa kumuua Martin Luther King na Malcolm X watakuwa wamefanikiwa kunyamazisha ujumbe wao.
Likawa ni kosa lililofanywa na CIA, wakaibuka wapigania haki wengine wa miaka ya 1970 na 80 na moto ukawa ni ule ule waliojaribu kuuzima kwa kuwanyima haki ya kuishi wamarekani weusi wawili. Sauti ya haki ni ya Mungu ni vigumu sana kuipoteza, sana sana yanakuwa ni yale mambo ya kumpiga teke chura unachokifanya ni kumuongezea tu mwendo.
Mapambano ya kudai haki huwa na kawaida moja ya ajabu sana. Kwamba yule anayezimwa milele asiweze kusikika hupata mrithi mwenye maarifa na uelewa kumzidi yeye anakuja kuzisumbua mamlaka zile zile zilizodhani zimemaliza kila kitu.
Sauti ya Mzee Shamte huko Unguja na Pemba inaweza kuwa imezimwa na mamlaka zilizoingia madarakani kihalali, ilitaka kujitanua sauti ile ili iweze kuwafumbua macho wenye nchi yao lakini mifumo ikamuwahi mzee wa watu na kwa sasa ni kimyaaaa.
Awamu ya nane huko Zanzibar iliingia uongozini kwa pesa nyingi za waarabu. Mlungula ulitembea haswa kipindi kile cha uchaguzi wa 2020, na waliokuwa wakiutoa ni waarabu. Sasa pesa ina kawaida ya kutaka irudi kwa namna moja au nyingine.
Ukikubali kununulika, lazima kuna siku inakuja inabidi utii kile unachoambiwa na aliyekununua. Ukitabasamu wakati unapokea chochote chenye harufu nzuri lazima kuna siku utatakiwa utoke nje wakati wa jua kali na mamilioni ya macho yakikutazama halafu ukatakiwa kuifanyia kazi ile pesa iliyopewa ndani ya vyumba vyenye viyoyozi vya mahoteli makubwa.
Kuwapa wakodishaji wa ardhi (kama wanavyoitwa) haki ya kukodisha kwa miaka 99 ni suala la hatari sana kwa uhuru mzima wa nchi husika. Na haya maneno ni ujumbe wa Mzee Shamte aliyenyamazishwa na baadae akaja kuombe msamaha.
Tunarudi kule kule katika suala la haki kuwa ni la asili (nature). Nafsi ya Shamte ipo kimya japo sio kwa kupenda mwenyewe, itaibuka nafsi nyingine yenye elimu, busara, upeo na hekima ya kidunia kuliko ile ya Mzee Shamte na itaongea na kuweka kila kitu hadharani. Ndio asili inavyotuambia siku zote.
Alikuwepo hayati Mapalala na mamlaka za nchi zilipomzima akaibuka hayati Mtikila na alipozimwa milele asiweze kuongea tena wamezaliwa kina Fatuma Karume na wanaharakati wengi wanaotumia majukwaa ya kupashana habari katika kuitetea haki wanayoona kama vile mfumo wetu unajaribu kuiminya.
Mzee Shamte kuwa kimya, maana yake wataibuka wengine machachari na wenye uchungu mkubwa zaidi.