Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Kama kawaida yake mzee huyu huwa hapendi kumumunya maneno, muda wote yupo busy akifanya shughuli yake inayompatia kipato. Na hapa ndipo huwa anaamua kushusha nondo za ukweli.
Waliokuwa wabunge wa CHADEMA walivuta posho za kujikimu na kisha kuingia mitaani na kusingizia kuwa wameenda kujiweka karantini, ili kujikinga na janga la Corona virus. Na wengi wao walidanganya kuwa wapo Dodoma.
Lakini Paul Makonda mwanasiasa machachari wa CCM alipowatia jambajamba kuwa ndani ya masaa 24 atawaweka ndani. Kila mtu alipigwa na butwaa. Maana watu walidhani wabunge wa CHADEMA wapo karantini, kumbe wapo Dar na mikoa mingine wakila bata na kuzitafuna pesa za walipa kodi wavuja jasho ambazo walilipwa ili kuwawakilisha bungeni.
Mzee Shomari anasema wabunge wa CCM walikomaa mpaka mwisho na kuhakikisha wanapitisha bajeti. Wabunge wa CHADEMA hawakushiriki kabisa kupitisha bajeti ambayo ina manufaa kwa watanzania. Kwa sababu hii ni wazi kabisa mbunge yoyote anayegombea kupitia CHADEMA hastahili kuchaguliwa maana wapo kwa ajili ya pesa za kujikimu na kujaza matumbo yao. Hivyo mzee Shomari amewaasa watanzania wasimpe ubunge mgombea yoyote wa CHADEMA. Na inavyoonekana Oktoba ikifika watavuna usaliti waliofanya.