Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu shomari aungane na wenzake kisakata ball,sio siasa na maisha Yake ya kutegemea wakulima wahenyeke yeye anyonye,Mimi mzee Shomari nasikitika sana kuwa Chadema wanaweka mgombea urais ambae hana huruma kwa watu masikini na tusio na uwezo kama mimi. Mimi nauza kahawa,kuna mama mama ntilie, kuna wamachinga na wengi tu ambao kipato ni cha hali ya chini.
Serikali ya CCM imetujali kwa kudhibiti uuzwaji wa nafaka nje ya nchi ili watanzania masikini kama mimi mzee Shomari nisipate tabu ya kupata kununua nafaka kama mahindi na mchele kwa bei ya juu. Maana huko miaka ya nyuma nafaka zilikuwa zinasafirishwa na kuuzwa holela nchi za nje, kitendo ambacho kilfanya unga na mchele uwe na bei kubwa. Leo hii unga hapa nchini una bei ya wastani ya sh 1300, lakini kabla ya serikali ya Ccm kudhibiti uuzwaji holela wa mazao kwenda nje ya nchi ulifikia hadi bei ya sh 2000.
Sasa basi kama mgombea wa Chadema akiwa mkoani Rukwa anasema ataruhusu wakulima wauze nje mazao kama wanavyotaka,hajui kuwa kuna madhara kwa watumiaji wa ndani. Maana anajinadi ataruhusu wauze nchi yoyote wanayotaka bila kujali mahitaji ya ndani.
Je, Mgombea urais kama huyu anapaswa apewe kura hata moja? Kama anakuwa hajali watu wenye shida na kipato duni kama mzee Shomari! Maana kiogozi bora lazima ujali raia wako kwanza kuliko kujali manufaa ya kisiasa. Maana ukiruhusu wakulima kuuza nafaka wanavyopenda,je wanachi wako watatapa chakula kwa bei rahisi!
Mzee Shomari anakuzidi akili maana hujui kuwa serikali inadhibiti uuzwaji nafaka ili kudhibiti mfumuko wa bei wa nafaka?Huu ndiyo utaahira wa John. Anadhibiti kitu ambacho hakushiriki wala kusaidia kukizalisha. John kweli ni hamnazo.
Kwenye macho ya "saccos" zinajengwa na watu binafsi, baada ya serikali kuwekeza ktk maendeleo ya watu, na sio vitu.Daah kwa hoja hizi bado sana,
Anyway kwahiyo hiyo miundombinu tunayoiona mkipiga picha mkiwa ulaya kusambaza sumu imejengwa na watu binafsi??
Hata Usa ambalo ni taifa lilioendelea sio kila kero wameishaitatua. So sio mbaya mgombea ubunge kusema hilo tatizo litatuliwe.View attachment 1573162
Ukizungumzia nia njema anza na Hawa wa ccm...
Hivi kweli miaka nenda rudi ahadi zenu ni zile zile... Mnachaguliwa alafu leo mnawakejeli wananchi wanaokunywa matope kuwa hawana tatizo kabisa...
Really...!!
Ebu acheni kuwatumia common wananchi kiasi hicho...
Sio kila mzee ana busara na hekima maana hata wapumbavu huzeeka!Hivi vijana nani aliwadanganya kwamba uzee ni kinga ya ulongo
Ni mtu wa kufikirika tu ambapo huyu kijana wa lumumba kamtengeneza kichwani kwake ili amtumie kutengeneza propaganda mfu!Ukiona mtu hajiamini mpaka anaamua kumtengeneza mtu wa kufikirika kisha kumpa mawazo yake basi jua hana uwezo wa kushawishi!Who is mzee shomari?
Mbona anauza kahawa mitaa ya Temeke. Wala hajaundwa,kwani Lissu hajasema ataruhusu wakulima kuuza mazao nje bila kujali mfumuko wa bei wa chakula?Sio kila mzee ana busara na hekima maana hata wapumbavu huzeeka!
Ila huyu mzee ni wa kufikirika tu aliyeundwa hapo lumumba ili wamtumie kutengeneza propaganda zao mfu!
Ungesema tu ni mawazo yako na hoja ingeendelea kuanzia hapo!Ila kila siku kumsingizia mtu wa kufikirika mawazo yako ndio watu wanatoka kwenye hoja na kuanza kuhoji lengo lako ni nini!Mbona anauza kahawa mitaa ya Temeke. Wala hajaundwa,kwani Lissu hajasema ataruhusu wakulima kuuza mazao nje bila kujali mfumuko wa bei wa chakula?
Mbona mnaweweseka? Jioni naenda kunywa kahawa kuna nondo atanipa nitawapatia ili mjue yupo kweli.Ni mtu wa kufikirika tu ambapo huyu kijana wa lumumba kamtengeneza kichwani kwake ili amtumie kutengeneza propaganda mfu!Ukiona mtu hajiamini mpaka anaamua kumtengeneza mtu wa kufikirika kisha kumpa mawazo yake basi jua hana uwezo wa kushawishi!
Kiufupi huu ni mwendelezo wa propaganda mfu!
Sasa unalazimisha asiwepo? Kwani wewe akisema ukweli mzee Shomari unaumia nini? Usimuingilie mzee wa watu bureUngesema tu ni mawazo yako na hoja ingeendelea kuanzia hapo!Ila kila siku kumsingizia mtu wa kufikirika mawazo yako ndio watu wanatoka kwenye hoja na kuanza kuhoji lengo lako ni nini!
Mwenzako johnthebaptist alikuwa ana mzee wake wa kufikirika kama wewe ila akaona mbinu hiyo haizai matunda maana watu walijikita katika kumjadiki huyo mzee ambaye kila siku alikuwa na la kuongea!!!!
Jiamini na uandike hoja na ulete mezani!
Vijana mnakwama wapi huko lumumba?
kama magu alijaribu Lisu atashindwa niniHiyo nchi itayoongozwa na Lisu ni ya kusadikika.
Maajabu matupu.
Yaani jamaa hakusanyi kodi lakini atatoa huduma za afya bure , elimu bure, tutajua kingereza kama wazungu, atapandisha mishahara kila mwaka na hatajenga hata sentimita moja iwe ya daraja au bara bara.