Mzee Siwa amekamilisha kazi yake ya kupanga safu sahihi kwa kesho nzuri, mliopo ofisini anzeni kuaga mpishe damu mpya na mawazo mapya

Mzee Siwa amekamilisha kazi yake ya kupanga safu sahihi kwa kesho nzuri, mliopo ofisini anzeni kuaga mpishe damu mpya na mawazo mapya

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mabadiliko yanayotokea sasa yanaanza kusuka upya mfumo wa utumishi wa umma. Tunategemea mapendekezo ya kiongozi aliyestaafu yanakwenda kuweka mwanzo mpya kwa mfumo wa utumishi.

Wapo wenye dola watakaotumbuliwa na kukabidhiwa wengine wanaoendana na mahitaji ya sasa. Ni muda muafaka kwa wakuu wa taasisi waliokata tamaa kukaa pembeni taasisi zisonge mbele.

Ufanisi na nidhamu kwenye mfumo wa utumishi umepungua. Watu wanafanyakazi kwa kumjaribu mama na viongozi waliopewa dhamana wanaogopa kufanya maamuzi ili waseme Rais ndiye kaelekeza.

Amkeni, hongera mzee Siwa tunaamini tathimini yako na mabadiliko uliyowaachia vijana yatamsaidia mama kuvuka salama katika harakati za Gen Z na ukosefu wa ajira.
 
Back
Top Bottom