Mzee Sumaye aliona mbali, siyo rahisi kufuta rushwa CCM ni heri ibatizwe kuwa Takrima!

Mzee Sumaye aliona mbali, siyo rahisi kufuta rushwa CCM ni heri ibatizwe kuwa Takrima!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Waziri mkuu mstaafu mzee Sumaye baada ya kuona siyo rahisi kuondoa rushwa kwenye uchaguzi ndani ya CCM aliipa jina jipya na zuri la Takrima.

Watu wakapiga sana kelele lakini ndio hivyo hadi leo huwezi kushinda uchaguzi CCM bila kutoa takrima.
Mgombea anagawa baiskeli kwa wajumbe wote wa mkutano wa uchaguzi, hiyo ni takrima na Takukuru haiwahusu.

Mambo ni mengi ngoja niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Suala la rushwa sio suala la kulichukulia poa hata kidogo hasa nyakati hizi za uchaguzi. Imefika wakati mheshimiwa rais wetu akisikia mtu yeyote yule katoa rushwa halafu kashinda basi ampige chini ampe hata aliyekuwa wa kumi huko ambaye ni muadilifu.

Kiukweli anayeweza kupambana na rushwa ndani ya ccm ni rais magufuli peke yake manake ana uthubutu wa kusema na haangalii makunyanzi.

Sasa kama.alivyo mvalia uso wa mbuzi mwananzila basi awavalie the same waliotoa rushwa na hata kwenye teuzi asiwafikirie. Hawa ni watu hatar sana wanaweza kuuzanchi na raia wake wakipewa madaraka.

Kigamboni naskia kuna mpambe wa mgombea alikuwa anagawa hela lkn waugwana wakamsoamesha namba asbh na.mapema
 
Mimi siamini kabisa kuwa Magufuli anapambana na rushwa, bali anatumia vita ya rushwa kukomoa mahasimu wake. Sana sana naona kuzuia uhuru wa vyombo vya habari kutangaza habari za rushwa,ili kuhadaa umma kuwa kaidhibiti rushwa ili kusaka sifa za kisiasa.

Kama kweli kungekuwa na vita ya rushwa, tungeona sio chini ya wanaccm 50 wakiwa mahakamani. Lakini kusubiri sijui kamati ya ccm ndio iengue watoa rushwa, ni hadaa ya mchana kweupe. Kama taasisi iliyoko kisheria kupambana na rushwa imeshindwa kuwapeleka watoa rushwa mahakamani, ujue kwenye hiyo kamati ya ccm ni siasa tu inaenda kuchezwa huko ndani illi kuwaengua wasiowataka kwa ajenda zao binafsi.
 
Halafu wanaccm ndio walikuwa wanasimama kuhadaa wananchi kuwa Magufuli kadhibiti rushwa. Hatimaye ukweli uko wazi kuwa rushwa ni jambo lisiloweza kudhibitiwa na ccm. Hii inaitwa Mungu hamfichi mnafiki.
Sisi tunataka rais ambaye ndiye hakimu wa mwisho aamue juu ya rushwa ndani ya ccm. Takukuru wanasubiria oda. Huoni kamishna wao jana kaambiw kapigwa ndio kanyanyuka kutumbua watu waliohusika kwenye ujenz wa majengo yao
 
Ngoja tuone watafanywaje.... Wakuu wa mkoa vijana wale wawili.. Maana nasikia wamezichanga balaa...
 
Sisi tunataka rais ambaye ndiye hakimu wa mwisho aamue juu ya rushwa ndani ya ccm. Takukuru wanasubiria oda. Huoni kamishna wao jana kaambiw kapigwa ndio kanyanyuka kutumbua watu waliohusika kwenye ujenz wa majengo yao

Ukiona hivyo ujue rais ndio mlinzi wa hiyo rushwa, na yoyote anayetuhumiwa kwa rushwa hana maslahi binafsi na rais. Vinginevyo mshauri aivunje hiyo pccb maana inakula hela ya bure, kwani kazi ya kupambana na rushwa anaifanya yeye.
 
Kuna Kigogo mmoja alipigwa mweleka akadai ,"Wajumbe hawataki tena vipeperushi vyenye wasifu wa wagombea bali wanataka vipeperushwa"
Mangula huyo, baada ya kushindwa uenyekiti wa mkoa, kule Iringa!
 
Ndugu zangu,
Rushwa ni mbaya sana maana Hawa viongozi hawatakuwa na uchungu wowote na Taifa. Watakuwa busy kurudisha pesa zao walizo poteza. Napendekeza yafuatayo
Mosi, CCM wabuni namna mpya ya kuwapata wajumbe wa kupiga kura. Hii ya sasa ni uchafu tupu
Pili, maslahi ya ubunge yapunguzwe kwa kiasi kikubwa. Haiwezekani graduate anapata mshahara laki 5 wakati hao wa kujua Kisoma na kuandika wapate 12M kwa mwezi. Hiki ndo chanzo Cha sarakasi zote.kiwango Cha mshahara na posho kishuke wapate chini ya 1M kwa mwezi, hutaona huu ujinga.
 
Ukiona hivyo ujue rais ndio mlinzi wa hiyo rushwa, na yoyote anayetuhumiwa kwa rushwa hana maslahi binafsi na rais. Vinginevyo mshauri aivunje hiyo pccb maana inakula hela ya bure, kwani kazi ya kupambana na rushwa anaifanya yeye.
Hii taasisi haina mrmno kwami kagi lugola licha ya kuthibitika kuwa anayo hatia je kawajibishwa?
 
Mimi siamini kabisa kuwa Magufuli anapambana na rushwa, bali anatumia vita ya rushwa kukomoa mahasimu wake. Sana sana naona kuzuia uhuru wa vyombo vya habari kutangaza habari za rushwa,ili kuhadaa umma kuwa kaidhibiti rushwa ili kusaka sifa za kisiasa.

Kama kweli kungekuwa na vita ya rushwa, tungeona sio chini ya wanaccm 50 wakiwa mahakamani. Lakini kusubiri sijui kamati ya ccm ndio iengue watoa rushwa, ni hadaa ya mchana kweupe. Kama taasisi iliyoko kisheria kupambana na rushwa imeshindwa kuwapeleka watoa rushwa mahakamani, ujue kwenye hiyo kamati ya ccm ni siasa tu inaenda kuchezwa huko ndani illi kuwaengua wasiowataka kwa ajenda zao binafsi.

Mwana ccm wa kwanza kukamatwa kwa RUSHWA YA UCHAGUZI NI ALIYEKUWA NAIBU SPIKA TULIA AKSON.

TAKUKURU WALIFUMBA MACHO, WALIZIBA MASIKIO ALIPOKUWA ANATOA RUSHWA KABLA HATA MUDA WA KUTANGAZA NIA HAUJAFIKA.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WALILALA USINGIZI.

POLISI WALISHANGILIA.
 
Kuna Kigogo mmoja alipigwa mweleka akadai ,"Wajumbe hawataki tena vipeperushi vyenye wasifu wa wagombea bali wanataka vipeperushwa"

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom