Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Huyu ni Mzee Ignasi Safari Swai mzaliwa na Mkazi wa Kijiji cha Momwe Kata ya Mrao Keryo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro,ambae ameamua kutoa sehemu Kubwa ya ardhi yake anayoimiliki na kuikabidhi kwa Serikali ili pajengwe zahanati itakayosaidia Kutoa huduma za kiafya kwa wananchi wa Kijiji hicho na vijiji jirani.
Mzee Swai anasema matamanio yake nikuona wananchi wenzake ikiwemo na yeye mwenyewe wanafikiwa na huduma za afya kwa ukaribu zaidi hivyo anafurahi kuona Serikali imeridhia na kuanza ujenzi wa Zahanati hiyo haraka ambapo tayari imekwisha kutoa Tsh. Milioni 20 zakuanza ujenzi.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wananchi wakati wakimkabidhi mzee Swai Cheti cha heshima na Shukurani, Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mwl. Raymond Mangwala amemuelekeza afisa ardhi wa wilaya kuanza kulitafutia eneo hilo hati ya umiliki kwa haraka