Naona wafia dini hapo juu wananiattack sana, naomba nitoe kauli yangu.
1.Hakuna sehemu niliyosema kuwa uislam uendeshwe kwa matakwa yangu
2. Hakuna nilipodeclare kwamba mimi ni msomi.
3. Hakuna mahali nilipozuia wafu kuzikwa haraka.
Ila nilitoa maoni yangu kulingana na Uislam na utamaduni wa Kiarabu kwamba hili jambo la kuwahisha kuzika nadhani ni kutokana na ukosefu wa teknolojia wakati huo kama mawasiliano, uhifadhi wa maiti na pia uchukuzi, ndio maana ikashauriwa kuwa maiti azikwe haraka, nimeandika neno imeshauriwa kwa sababu hakuna sehemu iliyoweka amri katika jambo hili.
Kuhusu uharaka wa kuzika hiyo ni perceptions za watu, kwa mfano mimi naweza kusema kuzika haraka ni ndani ya masaa mawili baada ya mtu kufa, mwingine akasema kuzika haraka ni baada ya masaa 24 ndugu wakishafika, mwingine anawesa kusema watoto wa marehemu wapo Marekani wanataka kushiriki ibada ya mazishi hivyo tutasubiri kwa siku tatu ili wafike, hiyo pia ni haraka kwa sababu hakuna maiti inayowekwa tu ndani halafu watu wakae nayo bila sababu.
Hayo yalikuwa ni maoni yangu, ssa tuje kwenu wafua dini mnijibu maswali haya mawili.
1. Tafsiri ya neno haraka nyinyi ni muda gani?
2. Mtume (S.a.w) alipofariki hakuzikwa siku hiyo hiyo, nini kilifanya wacheleweshe kuzika na je hapo hakukuwa na ulazima wa kufuata hiyo haraka mnayoipigia kelele.
NB:
Raha ya dini uamini kwa tafakuri sio kukaririshwa bila kufanya reasoning.
Kuna Uislam na kuna utamaduni wa kiarabu.
Naona umekazana na uislam na uarabu kwanza nikuhakikishie kuwezi kuutenganisha uislamu na huarabu utafanya vyoote lakini utararudi kwenye asili ya dini na sehemu ilipopokelewa.
Rejea kwenye LUGHA ya Qurani tukufu.
Pili jua kua sio kwakua uislam umeanzia uko middle east ndo kilawaho wanachokifanya ndo uislam hapana[emoji777] au kila tunachokifanya kwenye uislamu ni uarabu hapana[emoji777]
Kuna vitu vimewekwa kua ni sahihi na vitu vingine kua sio sahihi, mungu alipomchagua mtume wake atokee huko alikua na maana yake(HEKMA) na sijui ulitaka amchague mtume kutoka africa walipokua wanavaa nusu utupu!!!
Note ”Mungu ndo mjuzi wa yale tunayoyajua na tusoyajua, hakika hata angechagua mtume wake kutoka yoyote basi ingekua sahihi”
Mfano kuhusu vazi la kanzu, Kanzu ya asili yenyewe inasifa zake, kuanzia rangi mpaka muundo (haina mambo mengi, ipo kama sanda),
Mfano, HEKMA iliopo kwenye ilo vazi ni kua kama wote tungevaa kanzu ya asili hakuna ambae angeonekana tajiri au masikini ndani ya msikiti, haina maneno yotote ivo hata ndani ya ibada unakua na concetration, wala wakati wa swali haitokupa shida wala kuwaza mambo mengine.
Em assum upo ndani ya ibada af mtu anakuja mbele yako kavaa jezi ya Yanga au sijui Arsenal na wewe ni shabik wa mpira automatic mawazo yataenda kwenye match badala ya kufanya ibada.
Kanzu Ilipendekezwa kupitia sifa zake na ndo maana likawa ndo vazi rasmi kuvaliwa kwa mtu aliyemuislamu na wala sio dhambi kuvaa tofauti as long as sifa za asili za mavazi (kike&me) yalioruhusiwa hujapunguza hata moja kwaiyo usitake kusema kanzu ni tamaduni za waarabu kwaiyo sisi waafrica haifai kisa baridi sijui joto sijui unataka tuvae suti?,
kanzu itabaki kua VAZI bora kwenye uislamu, Sisi tunafata Qurani na sunna, kama mtume alivaa kanzu au alifuturu tende bas jua kanzu itakua na bora kuliko mavazi mengine kwaiyo ni muhimu sana japo sio lazima kuvaa, pia kama mtume alipenda kufuturu tende bas kama unauwezo nivizuri na muhimu kufuturu tende kuliko kitu kingine ila sio lazima na ivoivo kwa vitu vingine kama kufuga ndevu, kulala, kuoga, and etc kwa sababu ni SUNNA.
Swali no 1
Swala la muda ni limehusiwa(kusisitizwa) kua tuwazike marehem mapema iwezekanavyo.
Tunaposema mapema ni kua kama hakuna sababu ya MSINGI yakutozika mfano kwa sasa;
*Police kesi (uchunguzi wa mwili)
*Usafi (Mfano mwili ulo na risasi unabidi utolewe risasi zote kwanza ndo uoshwe then uzikwe)
*Mgogoro wa kifamilia (kuna miili watu wanakua wanavutana wengine wanavutana kua marehem azikwe dini hii wengine wanakataa)
*Utaratibu wa hospital (Labda mwili unadaiwa) and etc
Sio izo sababu zenu za et kuna mtoto wake yuko marekani kwaiyo mpaka afike!
Sijui mwili lazima ulale kwake kwanza sijui kusafirisha au kwakua kuna fridge za kutunzia maiti kwaiyo ni sawa tuu kutunza maiti hata mwezi!!! and etc. Unataka kuturetea mambo yakiwafiri tuu mwisho utasema kupiga picha za mwili kama kumbukumbu ni sawa maana zamani walikua hawana camera, saivi tuweke qaswida msibani maana zamani hawakua na speakers kwaiyo saiv ni sawa!!!
Swali no 2.
Mtume hakuzikwa sikuiyoiyo kwanza tambua mtume NI HAKUZIKWA ingekua unanambia kuna hadithi ilo thibit kua mtume alipata msiba wakat akiwa hai na alichelewesha kuzika apo ningekuelewa maana hatujudge matendo baada ya mtume tunajudge kile alochofanya yeye sababu baada ya kufa huenda hata maswahaba wake wangeutupa mwili lakini iyo isingekua juu yake maana keshakufa na kama kufundisha keshafundisha kwaiyo kufwata ama kutofwata alichoelekeza ni juu yetu sisi sio yeye tena.
Pili mapokeo ya hadithi za kifo chake zipo nyingi ila nyingi zinaonesha kipindi umauti unamkuta alikua na upande wa ke na ilibid wapetikane upande wa me na walipotimia 6 wakiongozwa na Ali ibn Abi Talib maramoja walifanya taratibu zote za kuzikwa kama mafundisho ya dini yetu yanavyo hitaji, huwez kuzika ukiwa mtu mmoja
Kwaiyo unaona kua sababu ilo wapelekea kuchelewa kuzika sio ya kizembe wala mahitaj ya mtu binafsi au kundi la watu, ila kama uwezekano wakuzika ungekuepo mda huo bas angezikwa.
Mwisho nawasiwasi nahisi wewe sio muislamu huwezi kua muislamu af ulete izo reasoning zako kwenye dini na hayupo mwislamu wa ivo usiijite et we ni mwisilamu wa haina flani muislamu ni muislamu tuu wote tunaafata na kuamini kitabu kituqufu na mafundisho ya mtume fullstop.