Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi


Wewe unavojinasibisha kua ni Muislam na izo reasoning zako chunga sana usije kua umesharitadi nahisi huujui uislam vizuri kua makini, kwenye issue za dini usilete usomi wako,usilete reason zako wala nini kitu kilichokua kimepokelewa na kupitishwa kama hadith sio kitu chakurekebisha vinginevo utakua unapinga na ukipinga maanake unakataa mafunzo ya mtume wetu Muhammad s.a.w na unaweza jikuta hauna dini au mwingoni mwa wanafik ama wasio amini kisa kutafta kuonekana unathinking capacity kubwa umu JF,

Ukisema kuweka reasoning wapo waislam kwa kwafikra zao watasema sisi bas tunachoma maiti maana kipind cha mtume walikua na sehemu za kuzika saiv kuna population hatuna sehem za kuzika

Kuna wengine watasema sisi tunazika kwa kama MAGHOLOFA(sio kwenye ardhi) maana kwenye ardhi watu wanatumia miili sana kufanya SHIRKI au waislamu wengine walio kwenye nchi za BARIDI watasema si hatuziki maana maiti zetu hazioz uko jangwani ndo kuna joto kwaiyo mtu akifa wanampamba tu kwenye mabarafu mwisho utakuta kila bala ama nchi waislam wana namna yao ya kuzika na iyo itakua kufru kubwa maana nikuyaacha mafundisho ya mtume wetu Muhammad s.a.w

Mtume sio mjinga aliposema tuwahishe kuzika huo ndo utaratibu na uislam unasheria na kanuni zake worldwide yan ukimwona mtu tuu unajua uyu ni mwislamu bila hata ya kuuliza kama kweli anafata maagizo sheria na kanuni za dinni.


jifunze kua humble kusoma zaidi dini kwa maana watu walio soma zaidi hua wanasifa za upole na akiongea huongea points jikite kwenye ibada timiza maagizo ya mola wako af mengine utajua siku ya mwisho ukiwa mbele ya mola wako otherwize labda we sio Muislamu ama Muislamu jina.
 
Hapo laizzm gharama nazo ziwe kubwa.. matokeo yake kukalifishana kwenye michango ya malaki ya pesa...roho ishaenda kukutana na amali zake nyie manabaki kuranda randa na kukaa na mwili ulokuwa hauna tena faida
IMEANDIKWA!
[emoji116][emoji116]
Yoshua bin Sira.38:16-23
16Mwanangu, mlilie mtu aliyekufa;
lia kwa uchungu, kuonesha huzuni yako.
Uuzike mwili wake kwa heshima ipasavyo,
wala usipuuze mazishi yake.
17Lia kwa uchungu na kwa moyo,
hudhuria matanga kama anavyostahili marehemu,
omboleza siku mbili tatu usije ukasemwa;
kisha ufarijike kutokana na huzuni yako.
18Maana huzuni huweza kusababisha kifo,
na huzuni ya moyo hunyonya nguvu za mtu.
19Mtu akiondolewa duniani huzuni imekwisha,
lakini maisha ya maskini, huulemesha moyo.
20Usiruhusu moyo wako kutawaliwa na huzuni;
ifukuze huzuni, ukifikiria mwisho wako.
21Usisahau kwamba hakuna kurudi nyuma,
humsaidii marehemu chochote na unajidhuru mwenyewe.
22Kumbuka, utakufa kama alivyokufa,
jana yeye, kesho wewe.
23Marehemu anapowekwa kupumzika kaburini,
nako kumkumbuka kuachwe;
nawe usiendelee kumlilia roho yake ikisha ondoka.
 
Mungu akufungue ufahamu nduguu
Nguzo ya tano ya uislamu Hyo Broo
Sio kunufaisha Waaarabu bwana
 
Unaweza kuorodhesha majina ya au taja angalau watatu waliowahi kuzikwa kabla ya kufa? Nipo hapa nasubiri
Kwani unapopelekwa makabulini kwa takbira unaweza ukasema nipo häi msinipeleke!
Hapo udongo ukikukandamiza uko peke yako nani wa kuorodhesha wakati watu wamesha tawanyika wenye maradhi wanampa pole nyingi mjane[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Umeshindwa vizuri ila kumbuka zipo nchi zinatekeleza
Hizo ni nchi za kizombi zinazoishi karne ya 7. Ndio manaa hata ninyi wenyewe hamna ndoto za kuishi Iran wala Afghanistan, mna ndoto za kuishi Marekani na Ulaya ambako hizo sheria hazipo.

Nyie hapa Tanzania mnatekeleza amri nyingi za Alah kama swala, kufunga etc...

Mbona amri ya kuua wanaouacha uislam hamuitekelezi? Ni kwa sababu IMEPITWA NA WAKATI kwa kizazi cha karne hii.
 
Unatubu dhambi kwa kiumbe mwenzio yesu,huo ndio ushirikina na ukafiri kimbia haraka
Ungeweka ushahidi basi!; Na sio Unaropokwa na kuturushia [emoji15][emoji12]
 
Weka ushahidi wa ayat quran inawaagiza mkifa mkamūane ngama![emoji101][emoji101]
 
Ni ukengeufu hata biblia haijaainisha hvyo, imeainisha vilevile waislamu wanavyofanya
Bibilia gani imeainisha namna ya kuzika? Unajua Yakobo alisafirishwa siku ngapi mpaka akazikwa? Je umesoma walimuombolezea siku ngapi?? Kila mtu abaki na utaratibu wake katika kuzika hatuwezi fanana, Cha msingi hakikisha jina lako limeandikwa kwenye kitabu cha uzima, hakuna tuzo katika mazishi
 
Ni hivi, wewe sio MKRISTO
 
Kwani unapopelekwa makabulini kwa takbira unaweza ukasema nipo häi msinipeleke!
Hapo udongo ukikukandamiza uko peke yako nani wa kuorodhesha wakati watu wamesha tawanyika wenye maradhi wanampa pole nyingi [emoji38][emoji38][emoji38]
Maneno meeengi bila ushahidi ni kelele tu
 
Akhiiy kaa chini usome
Dini ya Uislamu haiongozwi kwa akili bali kwa kufuata Quran na Sunnah

Nb. Kama huna elimu katika yetu nyamaza kimya acha wajuzi wazungumze
 

Naona umekazana na uislam na uarabu kwanza nikuhakikishie kuwezi kuutenganisha uislamu na huarabu utafanya vyoote lakini utararudi kwenye asili ya dini na sehemu ilipopokelewa.

Rejea kwenye LUGHA ya Qurani tukufu.

Pili jua kua sio kwakua uislam umeanzia uko middle east ndo kilawaho wanachokifanya ndo uislam hapana[emoji777] au kila tunachokifanya kwenye uislamu ni uarabu hapana[emoji777]

Kuna vitu vimewekwa kua ni sahihi na vitu vingine kua sio sahihi, mungu alipomchagua mtume wake atokee huko alikua na maana yake(HEKMA) na sijui ulitaka amchague mtume kutoka africa walipokua wanavaa nusu utupu!!!

Note ”Mungu ndo mjuzi wa yale tunayoyajua na tusoyajua, hakika hata angechagua mtume wake kutoka yoyote basi ingekua sahihi”

Mfano kuhusu vazi la kanzu, Kanzu ya asili yenyewe inasifa zake, kuanzia rangi mpaka muundo (haina mambo mengi, ipo kama sanda),

Mfano, HEKMA iliopo kwenye ilo vazi ni kua kama wote tungevaa kanzu ya asili hakuna ambae angeonekana tajiri au masikini ndani ya msikiti, haina maneno yotote ivo hata ndani ya ibada unakua na concetration, wala wakati wa swali haitokupa shida wala kuwaza mambo mengine.

Em assum upo ndani ya ibada af mtu anakuja mbele yako kavaa jezi ya Yanga au sijui Arsenal na wewe ni shabik wa mpira automatic mawazo yataenda kwenye match badala ya kufanya ibada.

Kanzu Ilipendekezwa kupitia sifa zake na ndo maana likawa ndo vazi rasmi kuvaliwa kwa mtu aliyemuislamu na wala sio dhambi kuvaa tofauti as long as sifa za asili za mavazi (kike&me) yalioruhusiwa hujapunguza hata moja kwaiyo usitake kusema kanzu ni tamaduni za waarabu kwaiyo sisi waafrica haifai kisa baridi sijui joto sijui unataka tuvae suti?,

kanzu itabaki kua VAZI bora kwenye uislamu, Sisi tunafata Qurani na sunna, kama mtume alivaa kanzu au alifuturu tende bas jua kanzu itakua na bora kuliko mavazi mengine kwaiyo ni muhimu sana japo sio lazima kuvaa, pia kama mtume alipenda kufuturu tende bas kama unauwezo nivizuri na muhimu kufuturu tende kuliko kitu kingine ila sio lazima na ivoivo kwa vitu vingine kama kufuga ndevu, kulala, kuoga, and etc kwa sababu ni SUNNA.

Swali no 1
Swala la muda ni limehusiwa(kusisitizwa) kua tuwazike marehem mapema iwezekanavyo.
Tunaposema mapema ni kua kama hakuna sababu ya MSINGI yakutozika mfano kwa sasa;
*Police kesi (uchunguzi wa mwili)
*Usafi (Mfano mwili ulo na risasi unabidi utolewe risasi zote kwanza ndo uoshwe then uzikwe)
*Mgogoro wa kifamilia (kuna miili watu wanakua wanavutana wengine wanavutana kua marehem azikwe dini hii wengine wanakataa)
*Utaratibu wa hospital (Labda mwili unadaiwa) and etc

Sio izo sababu zenu za et kuna mtoto wake yuko marekani kwaiyo mpaka afike!
Sijui mwili lazima ulale kwake kwanza sijui kusafirisha au kwakua kuna fridge za kutunzia maiti kwaiyo ni sawa tuu kutunza maiti hata mwezi!!! and etc. Unataka kuturetea mambo yakiwafiri tuu mwisho utasema kupiga picha za mwili kama kumbukumbu ni sawa maana zamani walikua hawana camera, saivi tuweke qaswida msibani maana zamani hawakua na speakers kwaiyo saiv ni sawa!!!

Swali no 2.
Mtume hakuzikwa sikuiyoiyo kwanza tambua mtume NI HAKUZIKWA ingekua unanambia kuna hadithi ilo thibit kua mtume alipata msiba wakat akiwa hai na alichelewesha kuzika apo ningekuelewa maana hatujudge matendo baada ya mtume tunajudge kile alochofanya yeye sababu baada ya kufa huenda hata maswahaba wake wangeutupa mwili lakini iyo isingekua juu yake maana keshakufa na kama kufundisha keshafundisha kwaiyo kufwata ama kutofwata alichoelekeza ni juu yetu sisi sio yeye tena.

Pili mapokeo ya hadithi za kifo chake zipo nyingi ila nyingi zinaonesha kipindi umauti unamkuta alikua na upande wa ke na ilibid wapetikane upande wa me na walipotimia 6 wakiongozwa na Ali ibn Abi Talib maramoja walifanya taratibu zote za kuzikwa kama mafundisho ya dini yetu yanavyo hitaji, huwez kuzika ukiwa mtu mmoja

Kwaiyo unaona kua sababu ilo wapelekea kuchelewa kuzika sio ya kizembe wala mahitaj ya mtu binafsi au kundi la watu, ila kama uwezekano wakuzika ungekuepo mda huo bas angezikwa.


Mwisho nawasiwasi nahisi wewe sio muislamu huwezi kua muislamu af ulete izo reasoning zako kwenye dini na hayupo mwislamu wa ivo usiijite et we ni mwisilamu wa haina flani muislamu ni muislamu tuu wote tunaafata na kuamini kitabu kituqufu na mafundisho ya mtume fullstop.
 
Mzee Ngorika alipofariki, Mabasi yake Ngorika yaliyokua na route za Dar-Arusha Tanga-Arusha yakapotea.

Warithi wa Tashriff wajifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…