Mzee wa miaka 50 ajinyonga baada ya kufumaniwa akimbaka mjukuu

Mzee wa miaka 50 ajinyonga baada ya kufumaniwa akimbaka mjukuu

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
Wakuu,

Nini kifanyike mbona haya mambo yanazidi sana? Ni kwamba wanaume tumezidiwa sana na ugwadu au ni madomo zege sana hatuwezi kutongoza siku hizi? Au shida ni nini? Au ushirikina!

----
1725527454368.jpeg

Olomi inadaiwa kabla ya kujiua, mke wake alimfumania akimbaka mjukuu wake, hivyo alipiga yowe kuomba msaada ndipo alipomtaka mama huyo aondoke nyumbani na asipofanya hivyo atachukua uamuzi wa kumuua.

Inaelezwa baada ya mke wake kupata vitisho hivyo, aliondoka nyumbani na kwenda kutafuta sehemu nyingine ya kuishi.

Aliporejea Septemba 2, alikuta mlango upo wazi huku mwili wa mume wake ukining’inia juu ya kenchi ya nyumba akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha tukio hilo. Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia.

Mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye ni ndugu wa familia hiyo, Digna Olomi amesema akiwa nyumbani kwake alipata taarifa kuhusu tukio hilo.

"Jana (Septemba 2) nikiwa nyumbani nilipigiwa simu kwamba kuna mtu kajinyonga, hivyo nilimpigia simu diwani na mtendaji nikaenda nao eneo la tukio, tulipofika tulimkuta kajinyonga," amesema.

Amesema mke wa Olomi alimweleza alifukuzwa na mume wake kutokana na ugomvi kati yao na alimweleza asipomuua atajinyonga, hivyo ikabidi aondoke nyumbani.

Kuhusu taarifa za mwanamume huyo kudaiwa kumbaka mjukuu wake, amesema amezisikia.

“Kuna watu wanasema kuna jambo amefanya ambalo lingemfanya afie ndani (magereza) nikauliza ni nini watu wanasema kwamba amembaka mjukuu wa miaka sita," amesema.

Muswada wa sheria

Matukio hayo yameripotiwa zikiwa zimepita siku tatu tangu Bunge lilipopitisha muswada wa sheria zinazohusu ulinzi wa mtoto.

Muswada huo unaosubiri kutiwa saini na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa sheria kamili uliwasilishwa bungeni Agosti 30, 2024 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima.

Muswada huo unazifanyia marekebisho sheria tatu ambazo ni Sheria ya Makosa ya Kimtandao Sura ya 443, Sheria ya Mtoto, Sura ya 13 na Sheria ya Msaada wa Kisheria, Sura ya 21.

Miongoni mwa marekebisho hayo ni kuwapo adhabu ya kulipa fidia kwa waathirika, huku Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, ikisema suala la fidia kwa mtoto aliyeathirika na vitendo vya kikatili liwe la lazima kwa atakayetiwa hatia.

Mbali ya hilo, muswada umefanya marekebisho na kuanzisha mabaraza ya watoto katika kila kijiji, kata, wilaya, mkoa na katika ngazi ya Taifa ikiwa na lengo la kuanzisha majukwaa yatakayoweza kujua changamoto zinazowakabili watoto na kuwalinda dhidi ya unyanyasaji unaofanywa katika jamii.

Dk Gwajima alisema marekebisho yamepanua wigo wa makosa ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto kwa kuongeza makosa mengine sita, hatua inayolenga kuongeza ulinzi wa watoto dhidi ya uhalifu wa kingono ambao umeongezeka kwa kasi kutokana na kukua kwa teknolojia.


Chanzo: Mwananchi

Pia soma
- Kulikoni! kesi za ulawiti na unyanyasaji kushamiri lakini wahalifu hawapewi adhabu kali?
 
Mbona kama hili tukio linatia msahaka!!
Ama kwakua marehem hawezi kusema tena, basi ndio abebeshwe msalaba right...🤔
Anyways, siungi mkono matendo ya ubakaji lakini kwa tukio hili naona kama kuna jambo halijakaa sawa.
 
Aliporejea Septemba 2, alikuta mlango upo wazi huku mwili wa mume wake ukining’inia juu ya kenchi ya nyumba akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha tukio hilo. Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia.
Haya mambo yalikuwa Iringa sasa yamesambaa kila kona
 
Back
Top Bottom