Ufunuo wa Yohana 21:1-3 (KJV) Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Kwa majibu wa ufunuo hiyo makao ya wanadamu yatakuwa mbinguni
Soma pia hapa
Ufunuo wa Yohana 20:2-3, 5-7 (KJV) Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
Hapo ndipo lilipo tatizo lako. Umesoma lakini bado hujui ulichokisoma.
Mji Mtakatifu Jerusalemu utashuka kutoka mbinguni kwenda wapi? Hebu soma taratibu uelewe.
Mji Mtakatifu Jerusalemu utashuka kutoka mbinguni kuja duniani (dunia mpya). Ndani ya mji huo wakati unashuka utakuwa hakuna Mwanadamu ndani yake isipokuwa MUNGU peke yake. MUNGU atashuka duniani akiwa ndani ya Mji Mtakatifu kwa ajili ya kuja kufanya makao na Wanadamu ambao watakuwa duniani pamoja na KRISTO.
Ukisoma kitabu hicho hicho cha Ufunuo utaona wakati Shetani ataachiliwa kwa muda mchache, atawakusanya baadhi ya watu hapa duniani ili wakafanye vita na "kambi ya Watakatifu". Hiyo kambi ya Watakatifu itakuwa wapi kama sio hapa hapa duniani? Kama kambi itakuwa Mbinguni kwa MUNGU Shetani na jeshi lake la wanadamu wataweza vipi kupanda Mbinguni kwenda kuipiga kambi ya Watakatifu?
Mzee tuliza akili. Kitabu cha Ufunuo kinasema na moto utashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza majeshi ya Shetani. Sasa huo moto utashuka wapi kama majeshi ya adui yatakuwa Mbinguni na sio duniani?
Hebu tuhame hapo kidogo, nikupeleke kwenye kile kifungu kinachosema "Naye atawatawala Wanadamu kwa fimbo ya chuma". YESU KRISTO anakuja duniani kutawala kama MFALME wa dunia yote.
Tena imeandikwa " naye huyo MFALME atawafundisha kuzibadili silaha zao kuwa miundu".
Maana yake ni kwamba "miundu" unatumika katika kilimo, sasa watabadili silaha zao na kuwa mundu wakiwa Mbinguni kwa MUNGU? Mbinguni kuna mashamba ya kulima? Wanadamu wataenda Mbinguni wakiwa na silaha zao kisha watafundishwa kuzibadili wakiwa huko???
Hebu twende kwenye kitabu cha Danieli, hapo kuna kifungu kinasema "tazama nikaona jiwe kubwa lisilofanywa kwa mikono ya Mwanadamu likishuka kutoka mbinguni, likaipiga sanamu ile na kuivunja vipande vipande na hata mahala pa sanamu ile hapakuonekana tena. Kisha Jiwe lile likawa mlima mkubwa likaijaza dunia yote".
Sasa nikufafanulie kwa kifupi tu, "Jiwe" ni YESU KRISTO. Sanamu ile kubwa ni "falme, Serikali na tawala za duniani". Jiwe kulivunja vunja sanamu ni YESU KRISTO kuundoa kabisa utawala wa falme na serikali za Wanadamu duniani na Yeye kutawala kama MFALME. JIWE kugeuka na kuwa mlima mkubwa ulioijaza dunia yote ni UFALME wa MUNGU kuijaza dunia yote wakati YESU NDIYE HUYO MFALME.
Sasa jiulize swali dogo sana, kama Watakatifu wanaenda kuishi Mbinguni, kuna haja gani ya YESU KRISTO kuja duniani kutawala? Kuna haja gani ya Watakatifu kufufuliwa wakati tayari wamekufa na wanaishi Mbinguni?
Hivi, Biblia haisemi hata Daudi aliyependwa sana na MUNGU, amekufa na kuzikwa na hajapanda bado kwenda Mbinguni?
Hebu jiulize swali kama Daudi alipendwa sana na MUNGU, lakini Daudi alikufa na kuzikwa kaburini pake na Biblia inasema Daudi hajaenda Mbinguni bali anasubiri kufufuliwa, wewe nani ukifa uende Mbinguni? MUNGU anakupenda wewe sana kuliko alivyompenda Daudi?
Hebu tujikumbushe kidogo maneno ya YESU KRISTO. Alisema, "heri wenye haki maana watairithi dunia".
Kama wenye haki wataenda Mbinguni mbona YESU KRISTO hakusema wenye haki watairithi Mbingu ya MUNGU?
Rudi kwenye Agano la kwanza, soma kile kitabu cha Mwanzo, niambie "ahadi" aliyopewa baba wa imani mzee Ibrahimu. Je, "ahadi" aliyopewa na MUNGU sio kuirithi nchi?
Au Ibrahimu aliambiwa atairithi Mbingu?
Mzee Ibrahimu alikufa kabla hata ya kuipokea "ahadi" ya kuirithi nchi. Je, huoni kama ahadi ilikuwa ni ya wakati ujao na bado haijatimizwa?
Ibrahimu atafufuliwa baada ya YESU KRISTO kurudi duniani na ndipo atapokea ile "ahadi" ya kurithi nchi hapa hapa duniani na sio Mbinguni.
Kwa kumalizia hebu nenda kasome kitabu cha Ezekieli 37. Mifupa mingi sana itafufuliwa, hao waliofufuliwa wataishi tena na kujenga nyumba zao katika nchi zao.
Sasa jiulize, kama watu wataenda Mbinguni kuishi hao wanaofufuliwa kwanini watajenga nyumba zao za kuishi hapa duniani?
Hebu nimalize kwa kukuuliza, kuna mahali imeandikwa YESU KRISTO atakaporudi duniani atafanya makao yake ya KIFALME pale Jerusalemu na watu wa mataifa wataenda Jerusalemu kila mwaka kutoa sadaka kwa MFALME. Sasa kama maisha yatakuwa Mbinguni ni YESU KRISTO yupi huyo atakayekuwa akiishi Yerusalem kama MFALME?
Na ni akina nani hao watakao kwenda kila mwaka Yerusalem kutoa sadaka?