Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Agl
Yohana 14:1-3 (KJV) Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
NIAMBIE YESU HAYO MAKAO KAENDA KUYAANDAA MBINGUNI AMA DUNIANI?
AU MAANA YAKO KAENDA KUYAANDAA KWA YERUSALEMU THEN ASHUKE NAO HADI MBINGUNI?
1 Wathesalonike 4:16-17 (KJV) Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
"Tutamlaki Bwana hewani" hiyo hewani itakuwa hapa duniani ama?
Soma pia mathayo 22:29-30
Yesu anawaambia huko mbinguni hakuna kuoa Wala kuolewa.
Karibu tujifunze. Nikufundishe nawe ukafundishe wengine.
Ahsantee sana
Kwanza nikupongeze unaijua jua biblia kiasi chake lkn Maelezo marefu yote hayo ya Nini mkuu?
Yohana 14:1-3 (KJV) Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
NIAMBIE YESU HAYO MAKAO KAENDA KUYAANDAA MBINGUNI AMA DUNIANI?
AU MAANA YAKO KAENDA KUYAANDAA KWA YERUSALEMU THEN ASHUKE NAO HADI MBINGUNI?
1 Wathesalonike 4:16-17 (KJV) Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
"Tutamlaki Bwana hewani" hiyo hewani itakuwa hapa duniani ama?
Soma pia mathayo 22:29-30
Yesu anawaambia huko mbinguni hakuna kuoa Wala kuolewa.
Karibu tujifunze. Nikufundishe nawe ukafundishe wengine.
Ahsantee sana
Hapo ndipo lilipo tatizo lako. Umesoma lakini bado hujui ulichokisoma.
Mji Mtakatifu Jerusalemu utashuka kutoka mbinguni kwenda wapi? Hebu soma taratibu uelewe.
Mji Mtakatifu Jerusalemu utashuka kutoka mbinguni kuja duniani (dunia mpya). Ndani ya mji huo wakati unashuka utakuwa hakuna Mwanadamu ndani yake isipokuwa MUNGU peke yake. MUNGU atashuka duniani akiwa ndani ya Mji Mtakatifu kwa ajili ya kuja kufanya makao na Wanadamu ambao watakuwa duniani pamoja na KRISTO.
Ukisoma kitabu hicho hicho cha Ufunuo utaona wakati Shetani ataachiliwa kwa muda mchache, atawakusanya baadhi ya watu hapa duniani ili wakafanye vita na "kambi ya Watakatifu". Hiyo kambi ya Watakatifu itakuwa wapi kama sio hapa hapa duniani? Kama kambi itakuwa Mbinguni kwa MUNGU Shetani na jeshi lake la wanadamu wataweza vipi kupanda Mbinguni kwenda kuipiga kambi ya Watakatifu?
Mzee tuliza akili. Kitabu cha Ufunuo kinasema na moto utashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza majeshi ya Shetani. Sasa huo moto utashuka wapi kama majeshi ya adui yatakuwa Mbinguni na sio duniani?
Hebu tuhame hapo kidogo, nikupeleke kwenye kile kifungu kinachosema "Naye atawatawala Wanadamu kwa fimbo ya chuma". YESU KRISTO anakuja duniani kutawala kama MFALME wa dunia yote.
Tena imeandikwa " naye huyo MFALME atawafundisha kuzibadili silaha zao kuwa miundu".
Maana yake ni kwamba "miundu" unatumika katika kilimo, sasa watabadili silaha zao na kuwa mundu wakiwa Mbinguni kwa MUNGU? Mbinguni kuna mashamba ya kulima? Wanadamu wataenda Mbinguni wakiwa na silaha zao kisha watafundishwa kuzibadili wakiwa huko???
Hebu twende kwenye kitabu cha Danieli, hapo kuna kifungu kinasema "tazama nikaona jiwe kubwa lisilofanywa kwa mikono ya Mwanadamu likishuka kutoka mbinguni, likaipiga sanamu ile na kuivunja vipande vipande na hata mahala pa sanamu ile hapakuonekana tena. Kisha Jiwe lile likawa mlima mkubwa likaijaza dunia yote".
Sasa nikufafanulie kwa kifupi tu, "Jiwe" ni YESU KRISTO. Sanamu ile kubwa ni "falme, Serikali na tawala za duniani". Jiwe kulivunja vunja sanamu ni YESU KRISTO kuundoa kabisa utawala wa falme na serikali za Wanadamu duniani na Yeye kutawala kama MFALME. JIWE kugeuka na kuwa mlima mkubwa ulioijaza dunia yote ni UFALME wa MUNGU kuijaza dunia yote wakati YESU NDIYE HUYO MFALME.
Sasa jiulize swali dogo sana, kama Watakatifu wanaenda kuishi Mbinguni, kuna haja gani ya YESU KRISTO kuja duniani kutawala? Kuna haja gani ya Watakatifu kufufuliwa wakati tayari wamekufa na wanaishi Mbinguni?
Hivi, Biblia haisemi hata Daudi aliyependwa sana na MUNGU, amekufa na kuzikwa na hajapanda bado kwenda Mbinguni?
Hebu jiulize swali kama Daudi alipendwa sana na MUNGU, lakini Daudi alikufa na kuzikwa kaburini pake na Biblia inasema Daudi hajaenda Mbinguni bali anasubiri kufufuliwa, wewe nani ukifa uende Mbinguni? MUNGU anakupenda wewe sana kuliko alivyompenda Daudi?
Hebu tujikumbushe kidogo maneno ya YESU KRISTO. Alisema, "heri wenye haki maana watairithi dunia".
Kama wenye haki wataenda Mbinguni mbona YESU KRISTO hakusema wenye haki watairithi Mbingu ya MUNGU?
Rudi kwenye Agano la kwanza, soma kile kitabu cha Mwanzo, niambie "ahadi" aliyopewa baba wa imani mzee Ibrahimu. Je, "ahadi" aliyopewa na MUNGU sio kuirithi nchi?
Au Ibrahimu aliambiwa atairithi Mbingu?
Mzee Ibrahimu alikufa kabla hata ya kuipokea "ahadi" ya kuirithi nchi. Je, huoni kama ahadi ilikuwa ni ya wakati ujao na bado haijatimizwa?
Ibrahimu atafufuliwa baada ya YESU KRISTO kurudi duniani na ndipo atapokea ile "ahadi" ya kurithi nchi hapa hapa duniani na sio Mbinguni.
Kwa kumalizia hebu nenda kasome kitabu cha Ezekieli 37. Mifupa mingi sana itafufuliwa, hao waliofufuliwa wataishi tena na kujenga nyumba zao katika nchi zao.
Sasa jiulize, kama watu wataenda Mbinguni kuishi hao wanaofufuliwa kwanini watajenga nyumba zao za kuishi hapa duniani?
Hebu nimalize kwa kukuuliza, kuna mahali imeandikwa YESU KRISTO atakaporudi duniani atafanya makao yake ya KIFALME pale Jerusalemu na watu wa mataifa wataenda Jerusalemu kila mwaka kutoa sadaka kwa MFALME. Sasa kama maisha yatakuwa Mbinguni ni YESU KRISTO yupi huyo atakayekuwa akiishi Yerusalem kama MFALME?
Na ni akina nani hao watakao kwenda kila mwaka Yerusalem kutoa sadaka?