SI KWELI Mzee Warioba amesema taarifa za uwepo wa Polepole Tanzania zinaukakasi, puuzeni

SI KWELI Mzee Warioba amesema taarifa za uwepo wa Polepole Tanzania zinaukakasi, puuzeni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
photo_2025-10-08_15-03-32.jpg
 
Tunachokijua
Jaji Joseph Sinde Warioba alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Novemba 5, 1985 hadi Novemba 9, 1990. Pia ni Mwanasheria, Mwanasiasa na Jaji maarufu anayeheshimika Kitaifa na Kimataifa kwa mchango wake mkubwa katika masuala ya Sheria na Utawala Bora.

Kadhalika aliwahi kuwa Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ya Bahari ya Hamburg, Ujerumani yenye makao yake makuu nchini Ujerumani kuanzia 1996 hadi 1999.

Oktoba 6, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa taarifa zikieleza kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ametekwa na watu wasiojulikana hadi kufikia leo Oktoba 08, 2025 hakukuwa na taarifa yoyote kuhusu kupatikana kwake.

Madai

Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa grafiki za Mwananchi kuwa Mzee Warioba amesema "taarifa za uwepo wa Polepole Tanzania zinaukakasi, puuzeni"


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichoripoti taarifa hiyo, Vilevile Jaji Warioba hajaonekana wala kusikika akitoa kauli hiyo.

Vilevile ufuatiliaji umebaini grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa na Mwananchi kama inavyoonekana wala chanzo chochote kingine cha kuaminika.

Aidha wanaosambaza grafiki hiyo hawaelezi hi wapi na lini Jaji Warioba aliyazungumza maneno hayo kuhusu sakata la Polepole.

Ni muhimu kuhakiki taarifa kabla ya kuamini na kusambaza kwa wengine ili kuzuia Upotoshaji.​
Maswali mengine ww una smartphone kwann usipite kwenye kurasa za kijamii za mwananchi ukahakiki unakuja kujaza server jf tu kweli akili ni nywele kila mtu na zake
 
Hao Mwananchi wanasemaje kwenye habari kamili? title za habari kwenye magazeti sio mara zote huakisi habari kamili
 
Jamani JF imefungiwa, sasa hawa Mwananchi wame Access bipo page hii?
Wonderful enough, bado JF administration wanaleta Jamii Check wakati wamefungiwa.
Hapo JF mmechemsha!
Maxence Melo
 
Chanzo cha taarifa ni wewe mwenyewe na bado unaetaka watu wazipuuze niwewe mwenyewe dah!

Wewe siyo miongoni mwa wale waandamanaji wa Mexico kweli 🤣🤣
 
Back
Top Bottom