Mzee wetu Mohamed Said anastahili heshima na si kejeli

Mzee wetu Mohamed Said anastahili heshima na si kejeli

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Nasikitishwa sana na kejeli ambazo baadhi ya wana jf wanazifanya kwa mzee wetu mwenye historia adhim ya taifa letu la Tanzania.

Mzee Mohamed Said ni mmoja Kati ya wazee wanaoheshimika sana pale darisalama na tanzania kwa ujumla.

Mzee wetu huyu ana historia kubwa sana ya tanzania na watu mashuhuri sehemu mbalimbali duniani.

Wanajamiiforum baadhi mmekosa heshima kwa kumuhusianisha mzee huyu na udini nasema hii sio sawa.

Mimi ni mkristo mkatoliki japo kwasasa niko passive kwasababu ya mwenendo wa viongozi wa kanisa; ila nasema wazi mzee Mohamed Said hatumtendei haki Sasa akiwa hai sasa mnasubiri atangulie mbele ya haki ndio muanze unafiki wenu?

Binafsi natanguliza kongole kwa mzee huyu na Mungu aendelee kumpa umri mrefu ili tuendelee kufaidi hazina yake.

Mungu mbariki mzee wetu Mohamed said kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Amen.
 
Mods naomba muwape ban angalau ya siku moja watu wanaomkashifu mzee Mohamed Said ni mtu muhimu mno kwetu wapenda historia.

Kwangu Mimi mzee huyu ni muhimu kuliko paskal mayala.
 
Kuna siku Kikeke huyu wa bbc aliulizwa kama anatangaza mpira huku nayeye ana mahaba na timu mojawapo kati ya hizo znazocheza anafanyaje kutopendelea upande wwote?

Jamaa alijibu huwa anaweka unazi pembeni na kurudi kwenye weledi yaani professionalism, hapa ndo changamoto ya huyu mzee said ilipo, amesoma lakini hajaelimika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom