Mzee Yusuph: Maisha yangu yamekuwa magumu baada ya kuacha muziki

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Aliyekuwa Msanii nguli wa Taarab nchini Mzee Yusuph amesema kwa sasa maishayake yamekuwa magumu baada ya kuacha muziki
Baada ya kuacha muziki anadai alijaribu shughuli nyingine ikiwemo kufungua duka Kariakoo lakini duka likafeli, lakini anasema maisha yamekuwa ya amani kuliko zamani na hata mtu akimuomba hela haogopi kumwambia hana kwa sababu hana kazi
Pia alipoacha muziki alikuwa ameshachukua milioni 25 za show na alipoulizwa itakuje na show alizochukua hela alisema Allah ndio atajua

 
Kila atakaekunifuata, ajikane mwenyewe, aubebe msalaba wake anifuate..

Itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote akaukosa uzima wa milele na nafsi yake kupotea?

Hayo ni maneno ya kwenye Biblia
 
Hizi site mbili za tofali kule chanika umefunga au bado zinapiga kazi,,,mzee yusuph hakuna mtu anaeuza tofali nying kama wewe wilaya hii ya ilala,,na ghorofa unajenga pale ofisin bado unasema mambo magumu?? Pale bonden buyun umempangia sijui nani yule nyumba sh 500,000 kwa mwezi[emoji16] [emoji16] [emoji16] nyumba ya yule mama anaefanya kazi ikulu bado kwel mambo mabaya?? Ha ha ha haya Mkuu ila jambo ulilofanya lina thawabu kwa Allah kuliko uliloacha
 

Kwakuwa 'umesikia'
ndo unaona inakupa haki ya kumdhalilisha kwa sababu tu umesikia?

Vyote ambavyo watu wanasema tunasikia vingekuwa vinatumika
kama ndio facts kuwahukumu watu wewe ungebaki salama?
 
Kwani alilazimishwa kuwacha kazi yake?asituzingue
 
Kwakuwa 'umesikia'
ndo unaona inakupa haki ya kumdhalilisha kwa sababu tu umesikia?

Vyote ambavyo watu wanasema tunasikia vingekuwa vinatumika
kama ndio facts kuwahukumu watu wewe ungebaki salama?
Ebu tufafanulie tujue huo udhalilishaji ni upi mkuu maana kufanya biashara mombasa, Pumba na lamu kama una leseni sioni kama ni tusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…