Mzee Yusuph, waliokushauri wamekudanganya

Mzee Yusuph, waliokushauri wamekudanganya

Mzee Yusufu piga mziki na usiwasikilize wanao kudhihaki.

Unatafuta ridhiki halali kabisa na limeridhiwa na Katiba ya Nchi.

Mungu amekupa kipaji cha Kuimba na uimbe ipate ridhiki yako.

Ongeza Ubunifu ili Uongeze Uwezo Wako

Riziki halali kwenye kazi haramu, huyo Mungu wenu ni yupi!!
 
Mzee Yusufu piga mziki na usiwasikilize wanao kudhihaki.

Unatafuta ridhiki halali kabisa na limeridhiwa na Katiba ya Nchi.

Mungu amekupa kipaji cha Kuimba na uimbe ipate ridhiki yako.

Ongeza Ubunifu ili Uongeze Uwezo Wako
kama alijua ni njia halali kwann aliamua kuikashifu, BTW anajua sio njia halali ila ni njaa tuh za kidunia
 
Hatakaa arudi kileleni ..na huo ndio mwisho wake...kakangeuka kiapo cha kumkataa shetani na kumrudia Mola wake..akafinywa kidogo tu akafinyika...MUNGU HAJARIBIWI
sheikh anasema bora hta ibilisi aliyemkataa mora wake moja kwa moja kuliko hyu anayemdhihaki laana zitamrudia
 
Hii mistari ungeingia studio utoe wimbo wa taarab
Ingependeza [emoji23][emoji23][emoji23]
Naimani ulitegemea ujio wako utatrend machochoro zote ila mwisho wa siku imekuwa kawaida sana tena umekuja kipindi watz wapo bize na morrison.

Mapokezi ya kawaida, show mbovu na umepoteza mvuto, na kilichobaki ni aibu na fedheha kwa upande wako. Kifupi muziki wa taarabu umeshakufa na kuzikwa muda mrefuuu na kamwe hautofufuka tena cz hauna mashabiki iwe bara iwe pwani na mambo ya vigodoro yalishafutwaga kitambo, na maukumbini tunaluka singeli za kina miss buza,

Najua global walikupamba tuh ili waingize pesa pale darLive ila kiukweli huna chamaana. Ndugu zako wakina Adija kopa, Isha mashauzi wameamia kwenye bfleva.
nb;

Mziki sio shule huwezi jipa likizo[emoji36]
 
Mi nilipoona tu show ya uzinduzi ni Dar Live Mbagala na sio Mlimani City afu kiingilio ni buku kumi na sio meza moja milioni nikajua jamaa hafiki mbali.. taarab ilishazikwa kitambo ipo uswahilini tu ambako hawaingii kwenye show wao wana burn cd na kupigia kwenye vigoro hawana hela.
Kwa ufupi Mzee alishauriwa vibaya
 
Taarab itabaki kuwa taarab
ina mashabiki wake,kama unavyoona reggae
kwenye vichwa vya mashabiki anatamba mzee, mimi binafsi ntaendelea kuwa shabiki la muziki wa taarab na mzee yusuph na wengine wote wanaoimba taarab
Naomba niimbie ule wimbo wa 'My Valentine'
 
Back
Top Bottom