Mzee Yusuph, waliokushauri wamekudanganya

Mzee Yusuph, waliokushauri wamekudanganya

Njaa sio udhuru wa kufanya maasia! Hawa makufar wanaokupamba humu wanafurahi kukuona umerudi kwenye "mila" zao! Kumbuka onyo hili: Hawatakaa watulie mpaka mufuate mila zao!!!,,,

Bro mtu akiwa na njaa kali na hakuna chakula kingine karibu anaruhusiwa kula hata nguruwe ili asife maana akifa njaa atakua ameudhulumu nafsi yake. Sahihi au sio sahihi?... je mzee Yusuf afe njaa au afanye awezalo kujinasua?
 
Duh hoja umeiweka mahala sio. Mzee yusuph hana njaa ya kufa...yeye ana njaa ya mafaniko aliyokuwa nayo ya mali na vitu. Hivyo njaa ya kufa sio njaa ya mzee yusuph
 
Labda sikuwepo dar live hiyo siku
Naimani ulitegemea ujio wako utatrend machochoro zote ila mwisho wa siku imekuwa kawaida sana tena umekuja kipindi watz wapo bize na morrison.

Mapokezi ya kawaida, show mbovu na umepoteza mvuto, na kilichobaki ni aibu na fedheha kwa upande wako. Kifupi muziki wa taarabu umeshakufa na kuzikwa muda mrefuuu na kamwe hautofufuka tena cz hauna mashabiki iwe bara iwe pwani na mambo ya vigodoro yalishafutwaga kitambo, na maukumbini tunaluka singeli za kina miss buza,

Najua global walikupamba tuh ili waingize pesa pale darLive ila kiukweli huna chamaana. Ndugu zako wakina Adija kopa, Isha mashauzi wameamia kwenye bfleva.
nb;

Mziki sio shule huwezi jipa likizo[emoji36]
 
Mtu kajaza watu karibia elfu 8 pale dar live halaf unaropoka eti kashuka kimziki
 
Back
Top Bottom