What can I do for you?
Kwa kadri ya uelewa wangu, ungetakiwa kujibu kutokana na mazungumzo mliyokuwa mnayazungumza kwa wakati huo.
Mfano; kama ulikuwa unamuelezea juu ya hali yako ngumu ya kimaisha basi ungetakiwa kumueleza ni kwa namna gani angeweza kukusaidia ili hali hiyo itengamae
Kama mlikuwa mnazungumza juu ya nia yako ya kusafiri kwenda nje, basi umuambie ni kitu gani angeweza kukusaidia. Labda, jinsi ya kupata visa, taarifa muhimu jinsi ya kufanikisha, mahali pazuri pa kufinikia, nk.
Au labda mazungumzo yalikuwa njia ya kukutana na wachuchu wa huko kwao. Basi angekupa hints za kufanya.
Haimaanishi kukusaidia kifedha kama unavyowaza.